bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Ezekiel 21
Ezekiel 21
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 22 →
1
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema:
2
“Mwanadamu, uelekeze uso wako juu ya Yerusalemu na uhubiri dhidi ya mahali patakatifu. Tabiri dhidi ya nchi ya Israeli
3
uiambie: ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Mimi niko kinyume nawe. Nitautoa upanga wangu kwenye ala yake na kumkatilia mbali mwenye haki na mwovu.
4
Kwa sababu nitamkatilia mbali mwenye haki na mwovu, upanga wangu utatolewa alani mwake uwe dhidi ya kila mtu kuanzia kusini hadi kaskazini.
5
Ndipo watu wote watajua ya kuwa Mimi Mwenyezi Mungu nimeutoa upanga wangu kwenye ala yake, nao hautarudi humo tena.’
6
“Kwa hiyo lia kwa uchungu, mwanadamu! Lia kwa uchungu mbele yao kwa moyo uliopondeka na kwa huzuni nyingi.
7
Nao watakapokuuliza, ‘Kwa nini unalia kwa uchungu?’ Utasema hivi, ‘Kwa sababu ya habari zinazokuja. Kila moyo utayeyuka na kila mkono utalegea, kila roho itazimia na kila goti litalegea kama maji.’ Habari hizo zinakuja! Hakika zitatendeka, asema Bwana Mungu Mwenyezi.”
8
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia, kusema:
9
“Mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: “ ‘Upanga, upanga, ulionolewa na kusuguliwa:
10
umenolewa kwa ajili ya mauaji, umesuguliwa ili ung’ae kama miali ya radi! “ ‘Je, tuifurahie fimbo ya utawala ya mwanangu Yuda? Upanga unadharau kila fimbo kama hiyo.
11
“ ‘Upanga umewekwa tayari ili kusuguliwa, ili upate kushikwa mkononi, umenolewa na kusuguliwa, umewekwa tayari kwa mkono wa muuaji.
12
Piga kelele na uomboleze, ee mwanadamu, kwa kuwa upanga u dhidi ya watu wangu; u dhidi ya wakuu wote wa Israeli. Wametolewa wauawe kwa upanga pamoja na watu wangu. Kwa hiyo pigapiga kifua chako.
13
“ ‘Lazima kuwe na kujaribiwa. Itakuwaje basi ikiwa fimbo ya ufalme ya Yuda inayodharauliwa na upanga haitakuwepo tena? asema Bwana Mungu Mwenyezi.’
14
“Hivyo basi, mwanadamu, tabiri na ukapige makofi. Upanga wako na upige mara mbili, naam, hata mara tatu. Ni upanga wa mauaji, upanga wa mauaji makuu, ukiwashambulia kutoka kila upande.
15
Ili mioyo ipate kuyeyuka na wanaouawa wawe wengi, nimeweka upanga wa mauaji kwenye malango yao yote. Lo! Umetengenezwa umetemete kama miali ya radi, umeshikwa kwa ajili ya kuua.
16
Ee upanga, kata upande wa kuume, kisha upande wa kushoto, mahali popote makali yako yatakapoelekezwa.
17
Mimi nami nitapiga makofi, nayo ghadhabu yangu itapungua. Mimi Mwenyezi Mungu nimesema.”
18
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema:
19
“Mwanadamu, weka alama njia mbili ambazo upanga wa mfalme wa Babeli utapitia, njia hizo zikianzia katika nchi hiyo hiyo. Weka kibao pale ambapo njia zinagawanyika kuelekea mjini.
20
Weka alama njia moja kwa ajili ya upanga upate kuja dhidi ya Raba ya Waamoni na nyingine upate kuja dhidi ya Yuda na Yerusalemu iliyozungushiwa ngome.
21
Kwa kuwa mfalme wa Babeli sasa amesimama katika njia panda, katika makutano ya njia mbili, akipiga ramli: anapiga kura kwa kutumia mishale, anataka shauri kwa sanamu zake, anachunguza maini ya wanyama.
22
Upande wake wa kuume inakuja kura ya Yerusalemu, ambapo ataweka magogo ya kubomoa, ili kuamrisha mauaji, kupiga ukelele wa vita, kuweka magogo ya kubomoa dhidi ya malango, kupandisha kilima hadi kuta zako, na kujenga husuru dhidi yako.
23
Itakuwa kama kupiga ramli kwa uongo kwa wale watu ambao wameapa kumtii yeye. Lakini mfalme wa Babeli atawakumbusha kuhusu uovu wao na kuwachukua mateka.
24
“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: ‘Kwa sababu ninyi mmefanya uovu wenu ukumbukwe kwa kuasi waziwazi, mkidhihirisha dhambi zenu katika yale yote mnayoyafanya: kwa kuwa mmefanya hivi, mtachukuliwa mateka.
25
“ ‘Ee mtawala kafiri na mwovu wa Israeli, ambaye siku yake imewadia, ambaye wakati wake wa adhabu umefikia kilele chake;
26
hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Vua kilemba, ondoa taji. Kwa kuwa mambo hayatakuwa vile yalivyokuwa. Aliye mnyonge atakwezwa, na aliyekwezwa atashushwa.
27
Mahame! Mahame! Nitaufanya mji kuwa mahame! Hautajengwa upya hadi aje yule aliye mwenye taji kwa haki; huyo ndiye nitakayempa.’
28
“Nawe, mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kuhusu Waamoni na matukano yao: “ ‘Upanga, upanga, umefutwa kwa ajili ya kuua, umesuguliwa ili kuangamiza na unametameta kama miali ya radi!
29
Wakati wanatoa maono ya uongo juu yako, na wanapobashiri uongo juu yako, upanga utawekwa kwenye shingo za wapotovu watakaouawa, wale siku yao imewadia, wakati wa adhabu yao ya mwisho.
30
“ ‘Urudishe upanga kwenye ala yake! Katika mahali ulipoumbiwa, katika nchi ya baba zako, huko nitakuhukumu.
31
Nitamwaga ghadhabu yangu juu yako na kupuliza moto wa hasira yangu dhidi yako; nitakutia mikononi mwa watu wakatili, watu stadi katika kuangamiza.
32
Mtakuwa kuni za kuwashia moto, damu yenu itamwagwa katika nchi yenu, wala hamtakumbukwa tena; kwa maana Mimi Mwenyezi Mungu nimesema.’ ”
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48