bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Psalms 18
Psalms 18
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 19 →
1
(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi Mtumishi Wa Mungu Aliyomwimbia Mungu Wakati Mungu Alipomwokoa Mkononi Mwa Sauli Na Adui Wengine) Nakupenda wewe, Ee BWANA, nguvu yangu.
2
BWANA ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu.
3
Ninamwita BWANA anayestahili kusifiwa, nami nimeokoka kutoka kwa adui zangu.
4
Kamba za mauti zilinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea.
5
Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili.
6
Katika shida yangu nalimwita BWANA, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika mbele zake, masikioni mwake.
7
Dunia ikatetemeka na kutikisika, misingi ya milima ikayumbayumba, ilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.
8
Pua zake zilitoa moshi, moto uteketezao ulitoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake.
9
Alizipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.
10
Alipanda kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo.
11
Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika, chandarua chake kumzunguka, mawingu meusi ya mvua angani.
12
Kutokana na mwanga mkali wa uwepo wake mawingu yalisogea, ikanyesha mvua ya mawe na umeme wa radi.
13
BWANA alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.
14
Aliipiga mishale yake na kutawanya adui, naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza.
15
Ee BWANA, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako, sakafu ya bahari ikaonekana, misingi ya dunia ikawa wazi.
16
Akanyosha mkono wake kutoka juu, akanishika, akanitoa kutoka katika maji mengi.
17
Akaniokoa kutoka adui yangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu, waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.
18
Walinishambulia siku ya taabu yangu, lakini BWANA alikuwa msaada wangu.
19
Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
20
BWANA alinitendea sawa sawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.
21
Kwa maana nimezishika njia za BWANA, sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
22
Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake.
23
Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi.
24
BWANA amenilipa sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake.
25
Kwa yeye aliye mwaminifu unajionyesha kuwa mwaminifu, kwa asiye na hatia unajionyesha kutokuwa na hatia.
26
Kwa aliye safi unajionyesha kuwa safi, lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi.
27
Wewe huwaokoa wanyenyekevu lakini huwashusha wenye kiburi.
28
Wewe, Ee BWANA, unaifanya taa yangu iendelee kuwaka, Mungu wangu hulifanya giza langu kuwa mwanga.
29
Kwa msaada wako nitashinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta.
30
Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, neno la BWANA ni kamili. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.
31
Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya BWANA? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu?
32
Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.
33
Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu.
34
Huifundisha mikono yangu kupigana vita, mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.
35
Hunipa ngao yako ya ushindi, mkono wako wa kuume hunitegemeza, huinama chini ili kuniinua.
36
Hupanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze.
37
Niliwafuatia adui zangu na nikawapata, sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.
38
Niliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena, walianguka chini ya miguu yangu.
39
Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita, adui zangu uliwafanya wasujudu miguuni pangu.
40
Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, nami nikawaangamiza adui zangu.
41
Walipiga yowe kuomba msaada, lakini hapakuwepo na ye yote wa kuwaokoa; walimlilia BWANA, lakini hakuwajibu.
42
Niliwaponda wakawa kama mavumbi yanayopeperushwa na upepo, nikawamwaga nje kama tope barabarani.
43
Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu; umenifanya kuwa kiongozi wa mataifa, watu ambao sikuwajua wananitumikia.
44
Mara wanisikiapo hunitii, wageni hunyenyekea mbele yangu.
45
Wote wanalegea, wanatoka katika ngome zao wakitetemeka.
46
BWANA yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu!
47
Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, awatiishaye mataifa chini yangu,
48
aniokoaye na adui zangu. Uliniinua juu ya adui zangu; uliniokoa toka watu wajeuri.
49
Kwa hiyo nitakusifu katikati ya mataifa, Ee BWANA; nitaliimbia sifa jina lako.
50
Humpa mfalme wake ushindi mkuu, huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake, kwa Daudi na uzao wake milele.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66
67
68
69
70
71
72
73
74
75
76
77
78
79
80
81
82
83
84
85
86
87
88
89
90
91
92
93
94
95
96
97
98
99
100
101
102
103
104
105
106
107
108
109
110
111
112
113
114
115
116
117
118
119
120
121
122
123
124
125
126
127
128
129
130
131
132
133
134
135
136
137
138
139
140
141
142
143
144
145
146
147
148
149
150