bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
/
Ezekiel 48
Ezekiel 48
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
← Chapter 47
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
1
Basi, haya ndiyo majina ya makabila hayo; toka mwisho wa pande za kaskazini, karibu na njia ya Hethloni, hadi maingilio ya Hamathi, hadi Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, yaani, upande wa kaskazini karibu na Hamathi, watakuwa na upande wa mashariki, na upande wa magharibi; Dani fungu moja.
2
Tena mpakani mwake Dani, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Asheri, fungu moja.
3
Na mpakani mwa Asheri, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Naftali, fungu moja.
4
Na mpakani mwa Naftali, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Manase, fungu moja.
5
Na mpakani mwa Manase, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Efraimu, fungu moja.
6
Na mpakani mwa Efraimu, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Reubeni, fungu moja.
7
Na mpakani mwa Reubeni, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Yuda, fungu moja.
8
Na mpakani mwa Yuda, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi, yatakuwapo matoleo mtakayotoa, upana wake mianzi elfu ishirini na tano, na urefu wake sawasawa na moja la mafungu hayo, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; na mahali patakatifu ni katikati yake.
9
Matoleo hayo, mtakayomtolea BWANA, urefu wake ni mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake elfu kumi.
10
Matoleo hayo matakatifu yatakuwa kwa ajili ya makuhani; upande wa kaskazini urefu wake mianzi elfu ishirini na tano, na upande wa magharibi upana wake mianzi elfu kumi, na upande wa mashariki upana wake mianzi elfu kumi, na upande wa kusini urefu wake mianzi elfu ishirini na tano; na mahali patakatifu pa BWANA patakuwa katikati yake.
11
Patakuwa kwa makuhani wa wana wa Sadoki, waliotakasika, waliofuata maagizo yangu, wasioasi, wana wa Israeli walipoasi, kama Walawi walivyoasi.
12
Na matoleo hayo ya nchi yatolewayo, yatakuwa kwao kitu kitakatifu sana, karibu na mpaka wa Walawi.
13
Na kuukabili mpaka wa makuhani, Walawi watakuwa na fungu, urefu wake mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake mianzi elfu kumi; urefu wote utakuwa mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake mianzi elfu kumi.
14
Wala hawatauza sehemu yake, wala kuibadili, wala hawatawapa wengine malimbuko ya nchi; maana ni matakatifu kwa BWANA.
15
Na mianzi elfu tano iliyosalia katika upana, kuikabili hiyo elfu ishirini na tano, itatumiwa na watu wote, kwa huo mji, na kwa maskani, na kwa viunga, na huo mji utakuwa katikati yake.
16
Na vipimo vyake ni hivi; upande wa kaskazini mianzi elfu nne na mia tano, na upande wa kusini mianzi elfu nne na mia tano, na upande wa mashariki mianzi elfu nne na mia tano, na upande wa magharibi mianzi elfu nne na mia tano.
17
Nao mji utakuwa na malisho; upande wa kaskazini mianzi mia mbili na hamsini, na upande wa kusini mianzi mia mbili na hamsini, na upande wa mashariki mianzi mia mbili na hamsini, na upande wa magharibi mianzi mia mbili na hamsini.
18
Na mabaki ya urefu wake yaelekeayo matoleo matakatifu, upande wa mashariki yatakuwa mianzi elfu kumi, na upande wa magharibi mianzi elfu kumi; nayo yatakuwa sawasawa na matoleo matakatifu; na mazao yake yatakuwa ni chakula cha watu wafanyao kazi humo mjini.
19
Na hao wafanyao kazi mjini, wa kabila zote za Israeli, watailima nchi hiyo.
20
Matoleo yote yatakuwa mianzi elfu ishirini na tano, kwa mianzi elfu ishirini na tano; mtatoa matoleo matakatifu, nchi ya mraba, pamoja na milki ya mji.
21
Nayo mabaki yake yatakuwa ya huyo mkuu, upande huu na upande huu wa matoleo matakatifu, na milki ya mji, kuikabili hiyo mianzi elfu ishirini na tano ya matoleo, kuelekea mpaka wa mashariki; tena upande wa magharibi kuikabili hiyo mianzi elfu ishirini na tano, upande wa kuelekea mpaka wa magharibi; sawa na yale mafungu, hayo yatakuwa ya huyo mkuu; na matoleo matakatifu na mahali patakatifu pa nyumba patakuwa katikati yake.
22
Tena tokea milki ya Walawi, na tokea milki ya mji, kwa kuwa ni katikati ya nchi iliyo ya mkuu, katikati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benyamini, itakuwa ya mkuu.
23
Na katika habari za kabila zilizosalia; toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Benyamini, fungu moja.
24
Tena mpakani mwa Benyamini, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Simeoni, fungu moja.
25
Tena mpakani mwa Simeoni, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Isakari, fungu moja.
26
Na mpakani mwa Isakari, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Zabuloni, fungu moja.
27
Na mpakani mwa Zabuloni, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Gadi, fungu moja.
28
Na mpakani mwa Gadi, upande wa kusini kuelekea kusini, mpaka wake utakuwa toka Tamari, mpaka maji ya Meriba-Kadeshi, mpaka kijito cha Misri, mpaka bahari kubwa.
29
Hiyo ndiyo nchi mtakayowagawanyia makabila ya Israeli, kuwa urithi wao, na hayo ndiyo mafungu yao, asema Bwana MUNGU.
30
Na matokeo ya mji ndiyo haya; upande wa kaskazini, mianzi elfu nne na mia tano, kwa kipimo;
31
na malango ya mji yatatajwa kwa majina ya makabila ya Israeli, malango matatu upande wa kaskazini; lango la Reubeni, moja; lango la Yuda, moja; na lango la Lawi, moja.
32
Na upande wa mashariki, mianzi elfu nne na mia tano, kwa kipimo; na malango matatu; lango la Yusufu, lango la Benyamini; lango la Dani.
33
Na upande wa kusini, mianzi elfu nne na mia tano kwa kupima; na malango matatu; lango la Simeoni; lango la Isakari, lango la Zabuloni.
34
Na upande wa magharibi, mianzi elfu nne na mia tano; pamoja na malango yake matatu; lango la Gadi, lango la Asheri; na lango la Naftali.
35
Kuuzunguka ni mianzi elfu kumi na nane; na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, BWANA yupo hapa.
← Chapter 47
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48