bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 3
1 Corinthians 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 4 →
1
Nami ndugu, sikuweza kusema nanyi, kama m wenye Roho, m wenye miili tu, m vitoto vichanga katika mambo ya Kristo; kwa hivyo nimesema nanyi kitoto.
2
Nimewanyonyesha maziwa, sikuwalisha vyakula vigumu, maana hamjaviweza bado. Lakini hata sasa hamviwezi bado,
3
kwa sababu mngali bado wenye miili tu. Maana ukiwako kwenu wivu na ugomvi, basi, ninyi ham wenye miili tu? Huu mwenendo wenu sio wa kimtu?
4
Maana mmoja akisema: Mimi wa Paulo, na mwingine: Mimi wa Apolo, basi, ninyi ham wa kimtu?
5
Apolo ni nani? Paulo ni nani? Tu watumishi waliowafundisha kumtegemea Bwana, kila mmoja wetu, kama Bwana alivyompa:
6
mimi nilipanda, Apolo akanywesha, lakini Mungu ndiye aliyeotesha.
7
Kwa hiyo apandeye siye, wala anyweshaye siye, ila Mungu aoteshaye ndiye.
8
Lakini apandaye naye anyweshaye sisi tu wamoja, lakini tutapata kila mmoja wake mshahara wa masumbuko yake mwenyewe.
9
Maana sisi tunasaidiana kazi na Mungu, ninyi m shamba lake Mungu, tena m jengo lake Mungu.
10
Kwa werevu wa kweli, niliogawiwa na Mungu, mimi niliweka msingi kama fundi aliye mwenye ubingwa wa jengo; lakini mwingine anajenga juu yake. Lakini kila aangalie, jinsi anavyojenga juu yake!
11
*Kwani hakuna anayeweza kuweka msingi mwingine pasipo ule uliokwisha kuwekwa, ulio Yesu Kristo.
12
Lakini mtu akijenga juu ya msingi huo kama dhahabu au fedha au mawe yenye bei kubwa au miti au nyasi au mabua,
13
basi, kila mtu kazi yake itatokea waziwazi. Siku ile itaipambanua, maana itafunuliwa kwa kuunguzwa na moto; ni ule moto utakaoumbua, kazi ya kila mtu ilivyo.
14
Jengo la mtu, alilolijenga juu yake likikaa, atapokea mshahara wake;
15
kama jengo la mtu linateketea, atapotelewa nalo, lakini mwenyewe ataokolewa, lakini itakuwa kama kuokolewa motoni.
16
Hamjui, ya kuwa ninyi m nyumba ya Mungu, ya kuwa Roho wa Mungu hukaa ndani yenu?
17
Mtu akiiangamiza nyumba yake Mungu, Mungu atamwangamiza yeye. Maana nyumba yake Mungu ni takatifu, ndiyo ninyi.
18
Mtu asijidanganye! Ikiwa mtu wa kwenu anajiwazia kuwa mwenye werevu wa kweli katika ulimwengu huu, sharti apumbae, apate kuwa mwerevu wa kweli!
19
Kwani huo werevu wa ulimwengu huu ni upumbavu kwa Mungu, maana imeandikwa: Wenye ubingwa huwanasa katika werevu wao mbaya.
20
Na tena: Bwana huyatambua mawazo ya wenye werevu kuwa ya bure.
21
Kwa hiyo mtu asijivune kwa wenziwe! Kwa maana yote ni yenu,
22
akiwa Paulo au Apolo, akiwa Kefa, au ukiwa ulimwengu, kukiwa kuishi au kufa, yakiwa yaliyopo au yatakayokuwapo, yote ni yenu.
23
Lakini ninyi m wake Kristo, naye Kristo ni wake Mungu.*
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16