bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 4
1 Corinthians 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 5 →
1
*Hivyo kila mtu atuwazie sisi kuwa watumikizi wa Kristo na watunzaji wa mafumbo yake Mungu.
2
Tena kwa watunzaji halitafutwi jingine, ni hili tu, ajulike kuwa mwelekevu.
3
Kwangu mimi si kitu, nikihukumiwa nanyi au na wengine wanaohukumu kimtu; nami mwenyewe sijihukumu,
4
kwani sinacho kibaya, ninachokijua moyoni. Lakini kwa hivyo si mwongofu; ila atakayenihukumu ni Bwana.
5
Kwa hiyo msihukumu neno lo lote siku hizi, mpaka Bwana atakapokuja; yeye ndiye atakayeyatia mwangani yaliyofichwa gizani; tena ndiye atakayeyafumbua waziwazi mawazo ya mioyo. Hapo ndipo, kila mtu atakapoonea sifa yake kwa Mungu.*
6
Ndugu, kwa ajili yenu nimeyasema haya kama mfano wa mimi na Apolo, mpate kujifundishia kwetu sisi, msijikweze kupapita hapo palipoandikwa kwamba: Mtu asijitutumue kuwa mkuu kuliko mwenziwe na kumpunguza mwingine!
7
Je? Yuko anayekupatia wewe macheo zaidi? Unacho kitu gani, usichopewa? Lakini kama umepewa, wajivuniaje, kama hukupewa?
8
Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata mali nyingi, mkatwaa nao ufalme, msiopewa na sisi. Tunataka sana, mwe wafalme, nasi tupate kuwa wafalme wenzenu.
9
Maana naona, ya kuwa Mungu ametuweka sisi mitume kuwa wa mwisho, kama watu wanaopaswa na kuuawa, kwani sisi ndio wanaotazamwa nao wa ulimwengu wote: malaika, hata watu.
10
Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi m wenye akili kwa kuwa naye Kristo. Sisi tu wanyonge, ninyi m wanguvu. Ninyi mwatukuzwa, lakini sisi twabezwa.
11
Mpaka saa hii ya sasa maumivu yetu yako, ni haya: njaa na kiu na uchi na mapigo na kukosa kikao;
12
twasumbuka tukifanya kazi na mikono yetu sisi. Tukitukanwa twaombea mema; tukifukuzwa twavumilia;
13
tukisingiziwa twabembeleza. Tumekuwa kama taka za ulimwengu, kama kifusi chao wote hata sasa hivi.
14
Siyaandiki haya, niwatie soni, ila nawaonya kama watoto wangu, ninaowapenda.
15
Kwani ingawa mnao wafunzi maelfu katika Kristo, lakini hamnao baba wengi. Kwani mimi ndiye niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa kuwapigia hiyo mbiu njema.
16
Kwa hiyo nawaonya, mniige mimi.
17
Kwa sababu hii nimemtuma Timoteo kwenu, huyu ni mtoto wangu mpendwa na mwelekevu katika Bwana. Yeye atawakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama ninavyowafundisha wateule wote po pote.
18
Lakini wako wanaojivuna, kwamba mimi siji kwenu.
19
Lakini nitakuja kwenu upesi, Bwana akitaka; ndipo, nitakapozitambua nguvu zao, wanazojivunia, si maneno yao tu.
20
Maana ufalme wa Mungu sio wa kujisemea, ila uko na nguvu.
21
Mnataka nini? Nije kwenu nikishika fimbo, au nije mwenye upendo na roho ya upole?
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16