bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 6
1 Corinthians 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 7 →
1
Inakuwaje, mtu wa kwenu aliye na jambo na mwenziwe akijipa moyo wa kuja kushtaki mbele yao walio wapotovu, asije mbele yao walio watakatifu?
2
Au hamjui, ya kuwa watakatifu watauhukumu ulimwengu? Ikiwa ulimwengu utahukumiwa nanyi, isiwapase kuamulia mambo yaliyo madogo?
3
Hamjui, ya kuwa tutahukumu malaika? Nayo ya huku nchini yasitupase?
4
Mkitaka kushtakiana mambo ya huku nchini, inakuwaje, mkiwaketisha katika kiti cha uamuzi wale wanaobezwa kwa wateule?
5
Haya nayasemea kuwatia soni. Je? Kwenu hakuna hata mmoja mwenye werevu wa kweli awezaye kuamua ndugu na mwenzake?
6
Kwenu sharti ndugu na ndugu washtakiane, kisha wapelekane kwao wasiomtegemea Mungu?
7
Kweli hayo mambo yote ya kushtakiana ninyi kwa ninyi ni kukosa utimilifu. Sababu gani hamtaki kupotolewa? Tena sababu gani hamtaki kunyang'anywa?
8
Lakini ninyi mwapotoana, mwanyang'anyana wenyewe, tena m ndugu!
9
Au hamjui, ya kuwa wapotovu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msipotelewe! Wagoni na watambikia vinyago na wavunja unyumba na walegevu na wenye kulalana
10
na wezi na wenye choyo na walevi na wenye matusi na wanyang'anyi, hao wote hawatautwaa ufalme wa Mungu.
11
Hata kwenu wako walio hivyo. Lakini mmeoshwa, tena mmetakaswa, mkaupata wongofu uliomo katika Jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho ya Mungu wetu.
12
Kwangu mimi hakuna cho chote chenye mwiko, lakini sivyo vyote vifaavyo: kwangu mimi hakuna cho chote chenye mwiko, lakini kitakachonishinda sikitaki kamwe.
13
Vyakula ni vya tumbo, nalo tumbo ni la vyakula; naye Mungu atavitowesha vyote viwili. Lakini mwili sio wa ugoni, ila wa Bwana, yeye Bwana ni mwenye mwili.
14
Mungu alimfufua Bwana, vivyo hivyo atatufufua hata sisi kwa nguvu yake.
15
Hamjui, ya kuwa miili yenu ni viungo vyake Kristo? Je? Nivichukue viungo vyake Kristo, nivigeuze kuwa vya ugoni? La, sivyo!
16
Au hamjui, ya kuwa mwenye kugandamiana na mke mgoni amekwisha kuwa mwili mmoja naye? Maana asema: Hao wawili watakuwa mwili mmoja.
17
Lakini mwenye kugandamiana na Bwana watakuwa roho moja.
18
Ukimbieni ugoni! Kosa lo lote, mtu atakalolifanya, liko nje ya mwili wake, lakini mgoni huukosea mwili wake mwenyewe.
19
Au hamjui, ya kuwa miili yenu ni nyumba yake Roho Mtakatifu awakaliaye? Ndiye, mliyepewa na Mungu, ninyi ham wenye ninyi.
20
Mmenunuliwa pakubwa, kwa hiyo mtukuzeni Mungu miilini na rohoni mwenu! Maana ni yake Mungu.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16