bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 7
1 Corinthians 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 8 →
1
Mambo, mliyoniandikia, nayajibu hivi: Ni vizuri, mtu asipogusa mwanamke.
2
Lakini kwa ajili ya ugoni kila mtu awe na mkewe mwenyewe, hata kila mwanamke awe na mumewe mwenyewe.
3
Mume ampe mkewe yampasayo, naye mke ampe mumewe yayo hayo.
4
Mke siye mwenye mwili wake, ila mumewe; vilevile naye mume siye mwenye mwili wake, ila mkewe.
5
Msinyamane, isipokuwa mmepatana kukaa hivyo kitambo kidogo, mjipatie siku za kufunga na za kuomba. Kisha mwandamane tena, Satani asipate kuwajaribu, kwani hamwezi kuvumilia pasipo kukoma.
6
Haya nayasema, kama ninavyoyatambua mimi, lakini siyo ya kuagiza.
7
Kupenda napenda, watu wote wawepo kama mimi mwenyewe; lakini kila mtu amegawiwa na Mungu kipaji chake yeye, mmoja hivyo, mwenzake hivyo.
8
Lakini wasiooa na wajane nawaambia: Itawafalia, wakikaa kama mimi.
9
Lakini kama hawawezi kujivumiliza, na waoe. Kwani kuoa ndiko kuzuri kuliko kuchomwa na tamaa.
10
Nao waliokwisha oana nawaagiza, tena si mimi, lakini ni Bwana: Mke asiachane na mumewe!
11
Lakini mke akiwa ameachana na mumewe, sharti akae pasipo kuolewa au apatanishwe tena na mumewe! Naye mume asiachane na mkewe!
12
Nao wengine nawaambia mimi, si Bwana: Aliye ndugu akiwa na mke asiyemtegemea Mungu, naye mkewe anapenda kukaa naye, asimwache!
13
Naye mwanamke akiwa na mume asiyemtegemea Mungu, naye mumewe anapenda kukaa naye, asimwache mumewe!
14
Kwa maana mume asiyemtegemea Mungu hutakaswa na mkewe; naye mke asiyemtegemea Mungu hutakaswa naye aliye ndugu. Ikiwa sivyo, watoto wenu wangekuwa wachafu, lakini sasa wametakata.
15
Lakini wale wasiomtegemea Mungu wakitaka kuvunja unyumba, na wauvunje! Hapo aliye ndugu, akiwa mume au akiwa mke, hakuna kifungo tena kinachomzuia; kwani ninyi Mungu amewaitia mapatano.
16
Kwani wajuaje, wewe mke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mume, kama utamwokoa mkeo?
17
Kwa hiyo nasema: Kila mtu avishike, Bwana alivyomgawia, kila mtu aendelee hivyo, alivyokuwa hapo, Mungu alipomwita! Hivyo ndivyo, ninavyoagiza katika wateule wote.
18
Mtu akiitwa alipokwisha kutahiriwa asivifiche! Mtu akiitwa akiwa hajatahiriwa, asitahiriwe!
19
Kule kutahiriwa siko, nako kutotahiriwa siko, ila kuyashika maagizo ya Mungu ndiko.
20
Kila mtu hivyo, alivyokuwa alipoitwa, na akae vivyo hivyo!
21
Kama ulikuwa mtumwa ulipoitwa, usivionee uchungu! Lakini ukiweza kujikomboa jikomboe!
22
Kwani mtumwa aliyeitiwa kuwa wa Bwana amekwisha kukombolewa na Bwana. Vivi hivi mwungwana aliyeitwa ni mtumwa wa Kristo.
23
Mmenunuliwa pakubwa. Msiwe tena watumwa wa watu!
24
Ndugu zangu, kila mtu hivyo, alivyokuwa hapo alipoitwa, sharti akae vivyo hivyo kwa Mungu!
25
Kwa ajili ya wanawali sikupata agizo la Bwana, ninawaambia, ninayoyatambua kwa hivyo, nilivyogawiwa na Bwana kuwa mwelekevu.
26
Nionavyo kuwa vizuri, ni hivi: kwa ajili ya shida hii, tuliyo nayo inamfaa mtu kukaa hivyo, alivyo:
27
ukiwa umejifunga kuwa na mke usitafute kufunguliwa! Usipokuwa umejifunga kuwa na mke usitafute mke!
28
Lakini hata ukioa hukosi, naye mwanamwali akiolewa hakosi. Lakini wafanyao hivyo huipatia miili maumivu, nayo ndiyo, mimi ninayoyataka kuwaponya
29
Lakini nasema hivi, ndugu zangu: Siku zimepunguka. Hapo panaposalia nao wenye wake sharti wawe, kama hawana! Nao wenye kulia wawe kama wasiolia!
30
Nao wenye furaha wawe kama wasiofurahi! Nao wenye kununua wawe, kama hawana kitu!
31
Nao wenye kuvitumia vya ulimwengu huu wawe, kama wanajitumilia bure tu! Kwani ulimwengu huu, jinsi ulivyo sasa, unatoweka.
32
Nataka, msipatwe na masumbuko. Asiyeoa huyasumbukia mambo ya Bwana, apate kumpendeza Bwana.
33
Aliyeoa huyasumbukia mambo ya ulimwenguni, apate kumpendeza mkewe; hivyo amekwisha kugawanyika.
34
Nayo ya mke na ya mwanamwali ni yaleyale: mke asiye na mume naye mwanamwali huyasumbukia mambo ya Bwana, apate kutakata mwilini na rohoni. Lakini mwenye mume huyasumbukia mambo ya ulimwenguni, apate kumpendeza mumewe.
35
Lakini haya nayasema, kwa kuwa yanawafaa; siyasemi, niwategee kitanzi, ila nayasemea kwamba: Yenu yote yaendelee, kama yapasavyo, mfulize kumkalia Bwana pasipo kuzuiliwa.
36
Lakini mtu akiona, ya kama haimfai mwanawe wa kike, akiwa mtu mzima pasipo kuolewa, -nayo hufikia hapohapo-, basi, na afanye, kama atakavyo! Hakosi, na amwoze!
37
Lakini aliyeushikiza moyo wake ukashupaa vizuri, usiteseke, yuko na nguvu ya kuyashinda mapenzi yake mwenyewe; basi, mtu aliye hivyo akijipa moyo wa kumkataza mwanawe wa kike kuolewa, atafanya vizuri.
38
Hivyo amwozaye mwanawe wa kike anafanya vizuri, lakini asiyemwoza mwanawe wa kike anafanya vizuri kumpita yule.
39
Mke yuko na mwiko siku zote za kuishi kwake mumewe; lakini mumewe anapokufa, amefunguliwa kuolewa naye ye yote, ampendaye, ikiwa tu, kama Bwana atakavyo.
40
Lakini vitakavyomfaa kupita hivi ni kukaa hivyo, alivyo. Hivyo ndivyo, nionavyo mimi; lakini najiwazia, ya kwamba nami ninayo Roho ya Mungu.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16