bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 8
1 Corinthians 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 9 →
1
Mambo ya nyama za tambiko twayajua kwamba: Sote tumeyatambua; tena: Utambuzi huleta majivuno, lakini upendo hujenga.
2
Lakini mtu akijiwazia, ya kuwa amekwisha kutambua kitu, basi, yeye hajautambua bado utambuzi upasao.
3
Lakini mtu akimpenda Mungu, huyo ametambuliwa naye.
4
Kwa ajili ya kula nyama za tambiko tunajua: hakuna, kinyago kifaliacho humu ulimwenguni, tena hakuna aliye Mungu pasipo mmoja.
5
Kweli viko viitwavyo miungu, kama vya mbinguni au vya ulimwenguni, kwa hiyo miungu yao ni mingi nao mabwana zao ni wengi,
6
lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja, ni Baba. Yote yametoka kwake, nasi tu watu wake. Tena Bwana ni mmoja, Yesu Kristo; vyote viliumbwa naye yeye, hata sisi tumeumbwa naye.
7
Lakini sio wote walio wenye utambuzi huu. Kwa hivyo, walivyozoea kutambikia mizimu, hata sasa wako wanaozila zile nyama, zikiwa za tambiko, lakini mioyo yao iliyo minyonge huchafuliwa kwa kujua maana.
8
Tena hakuna, vyakula vinavyotupatia kwake Mungu. Ikiwa tukila, hakuna tunachoongezewa; ikiwa hatuli, hakuna tunachopungukiwa.
9
Mwangalie tu, matumio yenu yasikwaze wanyonge!
10
Maana wewe uliyeyatambua hayo ukikaa hapo, wanapotambikia mizimu, ule nyama machoni pa mwenzio aliye mnyonge kwa kutojua maana vema, je? Hatahimizwa moyoni mwake, mpaka naye azile nyama zile za tambiko?
11
Hivyo kwa ajili ya utambuzi wako mnyonge anaponzwa, naye ni ndugu, ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
12
Mkiwakosea ndugu hivyo na kuiponza mioyo yao iliyo minyonge kwa kutojua maana vema, basi, mnamkosea Kristo mwenyewe.
13
Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, sitakula nyama kale na kale, maana nisimkwaze ndugu yangu.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16