bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Corinthians 9
1 Corinthians 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 10 →
1
Je? Mimi sikukombolewa? Mimi si mtume? Mimi sikumwona Bwana wetu Yesu Kristo? Nanyi ham kazi yangu, niliyomfanyizia Bwana?
2
Nisipokuwa mtume wa wengine, lakini ninyi ndimi mtume wenu. Kwani ninyi m muhuri inayoujulisha utume wangu, ya kuwa ni wa Bwana.
3
Makanio yangu kwao wanaoniulizauliza ndiyo haya ya kwamba:
4
Je? Hatuna ruhusa ya kula na ya kunywa yo yote?
5
Hatuna ruhusa pote, tunapokwenda, kuchukua na mke aliye ndugu, kama wanavyofanya mitume wengine na ndugu za Bwana, hata Kefa?
6
Au labda mimi na Barnaba peke yetu hatuna ruhusa ya kuwapo pasipo kazi?
7
Yuko askari aendaye vitani na kujilipa mwenyewe? Yuko mpanda mizabibu asiyekula matunda yao? Au yuko mchunga kundi asiyetumia maziwa ya kundi kuwa kitoweo?
8
Haya nayasema kimtu? Maonyo nayo hayayasemi yayo hayo?
9
Kwani imendikwa katika Maonyo ya Mose: Ng'ombe mwenye kupura ngano usimfunge kinywa! Hapo Mungu anataka kuwapatia ng'ombe?
10
Hapasemi kabisa kwa ajili yetu sisi? Kweli imeandikwa kwa ajili yetu sisi kwa kufaa, mkulima alimie kingojeo, naye mwenye kupura apurie kingojeo cha kugawiwa.
11
Kama sisi tumewapandia ya kutunza roho, ni vikubwa gani, sisi tukivuna yenu ya kutunza miili?
12
Ikiwa wengine wamepata ruhusa ya kula matumio yenu, hayatupasi sisi kuliko wale? Lakini hatukuitumia hiyo nguvu yetu, ila twayavumilia yote, kwamba Utume mwema wa Kristo tusiuzuie kamwe.
13
Hamjui, ya kuwa hao watumikiao Patakatifu hula yatokayo Patakatifu? Nao wachinja ng'ombe za tambiko hugawiwa fungu lao hapo chinjioni?
14
Vivyo hivyo naye Bwana aliwaagiza watangazaji wa Utume mwema, wajilishe huo Utume mwema.
15
Lakini mimi sikuyatumia mambo hayo hata moja. Nami sikuyaandika haya, kwamba yanitimilie hivyo; maana ningependa kufa kuliko kutenguliwa hilo tukuzo langu.
16
Kwani nikiipiga hiyo mbiu njema sinalo la kujivunia, maana nitashurutishwa. Kwani nisipoipiga hiyo mbiu njema ningepatwa na mambo.
17
Kwani nikiyafanya kwa kuyapenda, napata mshahara; lakini nikiyafanya pasipo kupenda, nako ndiko kuutimiza utunzaji niliopewa.
18
Basi, mshahara wangu ndio nini? Ni huu: nautangaza Utume mwema pasipo upato, nisiyatangue matumio yangu yaliyomo katika huo Utume mwema.
19
Maana mimi niliyekombolewa katika utumwa wote nimejigeuza kuwa mtumwa wao wote, kusudi walio wengi niwapate, wanifuate.
20
Kwao walio Wayuda nimekuwa kama Myuda, niwapate Wayuda. Kwao wenye miiko nimekuwa kama mwenzao mwenye miiko, tena miiko sinayo, ni kwamba tu, niwapate wenye miiko nao.
21
Kwao wasiojua maonyo nimekuwa kama mwenzao asiyejua maonyo, tena sipo pasipo Maonyo yake Mungu, kwani nayakalia Maonyo yake Kristo; huko ni kwamba tu, niwapate nao wasiojua maonyo.
22
Kwao walio wanyonge nimekuwa kama mnyonge mwenzao, niwapate walio wanyonge nao. Hivyo wote nimejifananisha nao katika mambo yo yote, nipate po pote wenye kuokoka.
23
Hayo nayafanya yote kwa ajili ya Utume mwema, nami nipate kugawiwa bia yake.
24
*Hamjui: Penye mashindano wote hupiga mbio, lakini atakayepewa tunzo ni mmoja tu? Nanyi pigeni mbio hivyo, kusudi mpewe!
25
Lakini kila aendaye kushindania hujinyima yote; hao hujinyima, wapewe kilemba kiangamiacho, lakini ninyi mjinyime, mpewe kilemba kisichoangamika!
26
Basi, nami napiga mbio hivyo, si kama sijui, ninavyokimbilia; napigana, lakini si kama anayejipigia tu.
27
Ila nauponda mwili wangu, mpaka nguvu zake ziishie kama za mtumwa, maana mimi ninayetangazia wengine nisije kuwa mwenye kutupwa.*
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16