bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Kings 2
1 Kings 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 3 →
1
Siku za kufa kwake Dawidi zilipofika karibu, akamwonya mwanawe Salomo akisema:
2
Mimi sasa ninakwenda njia inayowapasa wote wa huku nchini; nawe jipe moyo, uwe mtu wa kiume!
3
Yaangalie mambo ya Bwana Mungu wako, ayatakayo, yaangaliwe, ukizishika njia zake na kuyaangalia maongozi yake na maagizo yake na maamuzi yake na mashuhuda yake, kama yalivyoandikwa katika Maonyo ya Mose. Ndivyo, utakavyofanikiwa katika matendo yako yote po pote, utakapojielekezea.
4
Hivyo ndivyo, naye Bwana atakavyolitimiza neno lake, aliloniambia kwamba: Wanao watakapoziangalia njia zao, waendelee mbele yangu kikweli kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, basi, kwako hakutakoseka mtu atakayekaa katika kiti cha kifalme cha Waisiraeli.
5
Wewe nawe unayajua, Yoabu, mwana wa Seruya, aliyonifanyizia, nayo, aliyowafanyizia wale wakuu wawili wa vikosi vya Waisiraeli, Abineri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa Yeteri, akiwaua na kulipiza damu za vita siku za utengemano, hizo damu za vita akazimwagia mshipi wake, aliouvaa viunoni mwake, navyo viatu vyake, alivyovivaa miguuni pake.
6
Umfanyizie kwa werevu wako ulio wa kweli usipoacha, mvi zake zishuke kuzimuni na kutengemana.
7
Lakini wana wa Barzilai wa Gileadi uwafanyizie vema, wawe miongoni mwao wanaokula mezani pako. Kwani hivyo ndivyo, walivyonijia mimi, nilipomkimbia ndugu yako Abisalomu.
8
Tena tazama, unaye Simei, mwana wa Gera, aliye mtu wa Benyamini wa Bahurimu; ameniapiza kwa kiapo kibaya zaidi siku ile, nilipokwenda Mahanaimu. Naye halafu aliposhuka kuniendea huko Yordani, nikamwapia na kumtaja Bwana kwamba: Sitakuua kwa upanga.
9
Sasa wewe usimwache kuwa kama mtu asiyekosa! Kwani wewe ndiwe mtu mwerevu wa kweli, utayajua, utakayomfanyizia, uzitelemshe mvi zake kuzimuni, zikiwa zenye damu.
10
Kisha Dawidi akalala na baba zake, akazikwa mjini mwa Dawidi.
11
Nazo siku, Dawidi alizokuwa mfalme wa Waisiraeli, ni miaka 40; Heburoni alishika ufalme miaka 7, namo mle Yerusalemu alishika ufalme miaka 33.
12
Salomo akakaa katika kiti cha kifalme cha baba yake Dawidi, nao ufalme wake ukapata kushupaa sana.
13
Adonia, mwana wa Hagiti, akaja kwa Bati-Seba, mamake Salomo, naye akamwuliza: Kuja kwako ni kwema? Akajibu: Ndio, ni kwema.
14
Kisha akasema: Nina neno la kusema na wewe; akamwambia: Liseme!
15
Akasema: Unajua, ya kuwa ufalme ulikuwa wangu, nao Waisiraeli wote walikuwa wakinielekezea nyuso zao, niwe mfalme; lakini tena ufalme ukageuka kuwa wa ndugu yangu, kwani ulikuwa wake kwa agizo la Bwana.
16
Sasa mimi ninaomba kwako ombo moja, nawe usiutweze uso wangu! Akamwambia: Sema!
17
Akasema: Sema na mfalme Salomo, kwani hatautweza uso wako, anipe Abisagi wa Sunemu, awe mke wangu.
18
Bati-Seba akasema: Basi, mimi nitakusemea kwake mfalme.
19
Bati-Seba alipokuja kwa mfalme Salomo kumsemea Adonia kwake, mfalme akaondoka na kumwendea njiani, akamwinamia, kisha akakaa katika kiti chake cha kifalme; kisha mfalme akamwekea mama yake kiti cha kifalme, akakaa kuumeni kwake.
20
Kisha akasema: Mimi ninakuomba ombo moja lililo dogo, nawe usiutweze uso wangu! Mfalme akamwambia: Omba, mamangu! Kwani sitautweza uso wako.
21
Akasema: Ndugu yako Adonia na apewe Abisagi wa Sunemu, awe mkewe.
22
Mfalme Salomo akajibu akimwambia mama yake: Ni kwa sababu gani, ukimwombea Adonia, apewe Abisagi wa Sunemu? Umwombee nao ufalme! Kwani yeye ni ndugu yangu aliye mkubwa kuliko mimi. Waombee nao akina mtambikaji Abiatari na Yoabu, mwana wa Seruya!
23
Kisha mfalme Salomo akaapa na kumtaja Bwana akisema: Mungu na anifanyie hivi na hivi, tena aendelee hivyo, neno hilo, Adonia alilolisema, lisipokuwa la kuiangamiza roho yake!
24
Sasa kwa hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, aliyenitia nguvu akinikalisha katika kiti cha kifalme cha baba yangu Dawidi, akanitengenezea nyumba, kama alivyosema, basi, kwa sababu hiyo Adonia sharti afe leo hivi!
25
Mfalme Salomo akatuma kulitia jambo hilo mkononi mwake Benaya, mwana wa Yoyada, naye akampiga, hata akafa.
26
Naye mtambikaji Abiatari mfalme akamwambia: Nenda Anatoti shambani kwako! Kwani wewe unapaswa na kufa; lakini leo hivi sitakuua, kwa kuwa ulilichukua Sanduku la Bwana Mungu mbele ya baba yangu Dawidi, tena ukateseka katika mateso yote yaliyompata baba yangu.
27
Ndivyo, Salomo alivyomfukuza Abiatari, asiwe tena mtambikaji wa Bwana; akalitimiza lile neno la Bwana, alilolisema la mlango wa Eli kule Silo.
28
Habari hizi zikamfikia Yoabu, maana Yoabu alikuwa ameandamana na Adonia, ingawa Abisalomu hakuandamana naye kumfuata; ndipo, Yoabu alipokimbilia Hemani mwa Bwana, akazishika pembe za meza ya Bwana.
29
Mfalme Salomo akaambiwa: Yoabu amekimbilia Hemani mwa Bwana, yumo humo kandokando ya meza ya Bwana. Ndipo, Salomo alipomtuma Benaya, mwana wa Yoyada, akamwambia: Nenda, umpige!
30
Benaya akaingia Hemani mwa Bwana, akamwambia: Hivi ndivyo, mfalme anavyosema: Toka! Akasema: Sitoki, kwani nitajifia hapa. Benaya akarudi kwake mfalme, akamwambia neno hilo la kwamba: Hivyo ndivyo, Yoabu alivyosema, ndivyo alivyonijibu.
31
Mfalme akamwambia: Fanya, kama alivyosema, umpige hapo, kisha mzike! Ndivyo, utakavyoziondoa kwangu na kwa mlango wa baba yangu manza za zile damu, Yoabu alizozimwaga bure.
32
Tena ndivyo, Bwana atakavyomrudishia zile damu zake kichwani pake, alizozimwaga na kupiga watu wawili waliokuwa waongofu na wema kuliko yeye akiwaua kwa upanga, baba yangu Dawidi asivijue, yule Abineri, mwana wa Neri, mkuu wa vikosi vya Isiraeli, na Amasa, mwana wa Yeteri, mkuu wa vikosi vya Yuda.
33
Damu zao na zikirudie kichwa cha Yoabu na vichwa vya vizazi vyake kale na kale! Lakini kwake Dawidi na kwa vizazi vyake na kwa mlango wake na kwa kiti chake cha kifalme na kuweko kale na kale na matengemano yatokayo kwa Bwana!
34
Ndipo, Benaya, mwana wa Yoyada, alipopanda, akampiga na kumwua, kisha akazikwa nyumbani mwake nyikani.
35
Mfalme akamweka Benaya, mwana wa Yoyada, kuwa mkuu wa vikosi mahali pake, naye mtambikaji Sadoki mfalme akamweka kuwa mahali pa Abiatari.
36
Kisha mfalme akatuma, akamwita Simei, akamwambia: Jijengee nyumba humu Yerusalemu, ukae humo! Usitoke humo kwenda huko wala huko!
37
Itakuwa hivi: siku, utakapotoka na kukivuka kijito cha Kidoroni, ujue kabisa, ya kuwa utakufa papo hapo, damu yako iwe kichwani pako.
38
Simei akamwambia mfalme: Neno hili ni jema; kama bwana wangu mfalme alivyosema, ndivyo, mtumwa wako atakavyofanya. Kisha Simei akakaa Yerusalemu siku nyingi.
39
Ikawa, miaka mitatu ilipopita, watumwa wawili wa Simei walimkimbilia Akisi, mwana wa Maka, mfalme wa Gati; watu wakamwambia Simei kwamba: Tazama, watumwa wako wako Gati.
40
Ndipo, Simei alipomtandika punda wake, akaenda Gati kwa Akisi kuwatafuta watumwa wake; kisha Simei akaenda zake, akawaleta watumwa wake toka Gati.
41
Salomo akaambiwa, ya kuwa Simei ametoka Yerusalemu kwenda Gati na kurudi.
42
Ndipo, mfalme alipotuma kumwita Simei, akamwambia: Je? Sikukuapisha na kumtaja Bwana na kukushuhudia kwamba: Siku, utakapotoka na kwenda huko au huko, ujue kabisa, ya kuwa utakufa papo hapo? Nawe hukuniambia: Neno hili ni jema, nimesikia?
43
Mbona hukukishika kiapo cha Bwana, wala agizo, nililokuagiza?
44
Mfalme akamwambia Simei: Mwenyewe unayajua mabaya yote, moyo wako uliyoyawaza, uliyomtendea baba yangu Dawidi; sasa Bwana atayarudisha hayo mabaya yako kichwani pako.
45
Lakini mfalme Salomo atakuwa amebarikiwa, nacho kiti cha kifalme cha Dawidi kitakuwa chenye nguvu mbele ya Bwana kale na kale.
46
Kisha mfalme akamwagiza Benaya, mwana wa Yoyada, kwenda; naye akatoka, akampiga, hata akafa. Ndivyo, ufalme ulivyopata nguvu mkononi mwa Salomo.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22