bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 10
1 Samuel 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 11 →
1
Ndipo, Samweli alipokitwaa kichupa cha mafuta, akayamiminia kichwa chake, akamnonea midomo na kumwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyokupaka mafuta, uwe mkuu wao walio fungu lake.
2
Utakapotoka kwangu leo, utaona watu wawili penye kaburi la Raheli mpakani mwa Benyamini huko Selsa, nao watakuambia: Wale punda wa kike, uliokwenda kuwatafuta, wameonekana. Tazama, baba yako ameyaacha mambo ya punda kwa kuwahangaikia ninyi akisema: Mwanangu nimfanyie nini?
3
Utakapoondoka huko kwenda zako na kufika penye mvule wa Tabori, huko watu watatu watakutana na wewe, nao wanapanda kwenda Beteli kwa Mungu, mmoja anachukua wana mbuzi watatu, mmoja mikate mitatu, mmoja kiriba cha mvinyo.
4
Nao watakuamkia na kukupa mikate miwili, nawe utaipokea mikononi mwao.
5
Baadaye utafika kwenye kilima cha Mungu, ngome ya Wafilisti iliko. Utakapofika huko penye mji huo utakuta kikosi cha wafumbuaji wanaoshuka kilimani pa kutambikia wakitanguliwa na mapango na matoazi na mazomari na mazeze, nao wanakwenda wakifumbua maneno.
6
Ndipo, roho ya Bwana itakapokujia, ufumbue pamoja nao; ndivyo, utakavyogeuzwa kuwa mtu mwingine.
7
Hapo, hivyo vielekezo vitakapokutukia, fanya, mkono wako utakayoyaona! kwani Mungu yuko na wewe.
8
Kisha shuka kunitangulia kwenda Gilgali! Nami utaniona, nikishuka kuja kwako kutoa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na kuchinja ng'ombe za tambiko za shukrani. Utangoja siku saba, hata nitakapokuja kwako, nikujulishe utakayoyafanya.
9
Ikawa, Sauli alipogeuka, atoke kwake Samweli, ndipo, Mungu alipougeuza moyo wake kuwa mwingine. Navyo vielekezo vile vyote vikatukia siku ile.
10
Walipofika kule Gibea, wakaona kikosi cha wafumbuaji kilichokuja kukutana naye; ndipo, roho ya Mungu ilipomjia, naye akafumbua mambo katikati yao.
11
Ikawa, wote waliomjua zamani zote walipomwona, ya kuwa anafumbua mambo pamoja na wafumbuaji, ndipo, watu hao waliposemezana kila mtu na mwenzake: Hivi vya mwana wa Kisi vinakuwaje? Kumbe Sauli naye yumo katika wafumbuaji?
12
Mtu wa huko akajibu: Je? Baba yao ni nani? Kwa hiyo likawa fumbo la kwamba: Kumbe Sauli naye yumo katika wafumbuaji!
13
Alipokwisha kufumbua mambo akaja kilimani pa kutambikia.
14
Mjomba wake Sauli akamwuliza yeye na kijana wake: Mlikwenda wapi? Akajibu: Kuwatatufa wale punda wa kike; lakini tusipowaona tukaenda kwa Samweli.
15
Mjomba wake Sauli akasema: Nisimulie, Samweli aliyowaambia!
16
Sauli akamwambia mjomba wake: Ametupasha habari, ya kuwa wale punda wa kike wameonekana; lakini lile neno la ufalme, Samweli alilolisema, hakumsimulia.
17
Kisha Samweli akawaita watu kuja kwake Bwana huko Misipa.
18
Akawaambia wana wa Isiraeli: Hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mungu wa Isiraeli: Mimi niliwatoa Waisiraeli Misri, nikawaponya mikononi mwa Wamisri namo mikononi mwa wafalme wote waliowasumbua ninyi.
19
Nanyi siku hii ya leo mmemkataa Mungu wenu aliyewaokoa katika mabaya na katika masongano yenu yote mkimwambia: Tuwekee mfalme, atutawale! Sasa jipangeni hapa machoni pake Bwana kwa mashina yenu na kwa maelfu yenu!
20
Samweli alipokwisha kuyafikisha mashina yote, wakipiga kura, likashikwa shina la Benyamini.
21
Kisha alipolifikisha shina la Benyamini milango kwa milango, ukashikwa mlango wa Matiri, kisha akashikwa Sauli, mwana wa Kisi. Lakini walipomtafuta hawakumwona.
22
Ndipo, walipomwuliza Bwana tena: Mtu huyu amefika kweli huku? Bwana akajibu: Mtazameni, amejificha kwenye mizigo!
23
Wakapiga mbio kwenda kumchukua huko. Alipokuja kusimama katikati ya watu aliwapita watu wote kwa urefu wa kichwa, kikianza kupimwa mabegani.
24
Samweli akawaambia watu wote: Mmemwona, Bwana aliyemchagua? Kwani kwao watu wote hakuna afananaye naye. Ndipo, wote walipopiga yowe za kumshangilia kwamba: Pongezi, mfalme!
25
Kisha Samweli akawaambia watu haki yake mfalme, akaiandika katika kitabu, akakiweka hapo pake Bwana; kisha Samweli akawaaga watu wote, waende zao kila mtu nyumbani kwake.
26
Naye Sauli akaenda zake nyumbani kwake huko Gibea, nao vijana wenye nguvu, Mungu aliowahimiza mioyoni, wakamsindikiza.
27
Lakini watu wasiofaa kitu wakasema: Huyu atatuokoaje? Wakambeza, hawakumletea matunzo. Lakini yeye akawa, kama hakuyasikia, waliyoyasema.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31