bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 11
1 Samuel 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 12 →
1
Nahasi wa Waamoni akapanda, akapiga makambi huko Yabesi katika nchi ya Gileadi. Ndipo, watu wote wa Yabesi walipomwambia Nahasi: Fanya agano nasi, tukutumikie!
2
Mwamoni Nahasi akawaambia: Basi, nitapatana nanyi hivyo: nitawachoma ninyi kila mtu jicho lake la kuume, niwatweze Waisiraeli wote.
3
Wazee wa Yabesi wakamwambia: Tupe siku saba, tutume wajumbe kwenda katika mipaka yote ya Waisiraeli! Asipopatikana mwokozi wetu, tutakutokea.
4
Wajumbe walipofika Gibea kwa Sauli na kuyasema maneno hayo masikioni pa watu, watu wote wakalia na kupaza sauti zao.
5
Naye Sauli alikuwa anarudi malishoni akiwafuata ng'ombe; hapo Sauli akauliza: Watu wanalilia nini? Wakamsimulia habari, watu wa Yabesi walizozileta.
6
Ndipo, roho ya Mungu ilipomjia Sauli, alipozisikia habari hizo, makali yake yakawaka moto.
7
Akakamata ng'ombe wawili, akawakatakata, akawatuma wale wajumbe kwenda katika nchi zote za Waisiraeli na kuwapelekea watu vipande vya nyama kwamba: Kila mtu asiyetoka kumfuata Sauli na Samweli ng'ombe wake watafanyiziwa hivyo. Ndipo, watu walipoguiwa na kituko cha Bwana, wakatoka kama mtu mmoja.
8
Alipowakagua huko Bezeki, wana wa Isiraeli walikuwa 300000, nao watu wa Yuda 30000.
9
Wakawaambia wale wajumbe waliokuja: Hivi ndivyo, mtakavyowaambia watu wa Yabesi katika nchi ya Gileadi: Kesho, jua likianza kuwa kali, mtaona wokovu. Hao wajumbe waliporudi na kuwapasha habari hii, watu wa Yabesi wakafurahi.
10
Nao watu wa Yabesi wakawaambia wale: Kesho tutawatokea, mtufanyizie yote yaliyo mema machoni penu.
11
Kesho yake Sauli akawagawanya watu wake kuwa vikosi vitatu, wakaingia katikati ya makambi penye zamu ya kungoja, kuche, wakawapiga Waamoni, hata jua lilipokuwa kali mchana huo. Nao waliosalia wakatawanyika, wasisalie kwao wawili tu waliokuwa pamoja.
12
Ndipo, watu walipomwambia Samweli: Wako wapi waliosema: Huyu Sauli awe mfalme wetu? Watoeni watu hawa, tuwaue!
13
Lakini Sauli akasema: Asiuawe mtu wa kwetu siku hii ya leo! Kwani leo Bwana amewapatia Waisiraeli wokovu.
14
Samweli akawaambia watu: Njoni, twende Gilgali, tuurudishie ufalme upya!
15
Watu wote wakaja Gilgali, kisha wakamweka Sauli machoni pake Bwana huko Gilgali kuwa mfalme wao wakachinja huko machoni pake Bwana ng'ombe za tambiko za shukrani, naye Sauli akachangamka sanasana pamoja na Waisiraeli wote.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31