bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 16
1 Samuel 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 17 →
1
Bwana akamwambia Samweli: Utamsikitikia Sauli mpaka lini? Nami ndiye niliyemtangua, asiwe mfalme wa kuwatawala Waisiraeli. Jaza pembe yako mafuta, nikutume kwa Isai wa Beti-Lehemu! Kwani nimejionea mfalme katika wanawe.
2
Samweli akasema: Nitakwendaje? Sauli akivisikia ataniua. Bwana akasema: Chukua mori ya ng'ombe mkononi mwako, useme: Nimekuja kumtambikia Bwana!
3
Mwalike Isai, naye aje kwenye tambiko hilo! Nami nitakujulisha utakayoyafanya, unipakie mafuta yeye, nitakayekuonyesha.
4
Samweli akayafanya, Bwana aliyomwambia. Alipofika Beti-Lehemu, wazee wa mji wakamjia njiani na kutetemeka, wakamwamkia kwamba: Kuja kwako ni kwema?
5
Akawaitikia: Ni kwema, nimekuja kumtambikia Bwana: jieueni, nanyi mje pamoja nami kutambika! Isai na wanawe akawaeua mwenyewe, alipowaalika nao kuja kutambika.
6
Ikawa, walipokuja, alipomwona Eliabu akasema moyoni: Labda ni yeye atakayepakwa mafuta mbele yake Bwana.
7
Lakini Bwana akamwambia Samweli: Usiitazame sura yake wala ukubwa wa umbo lake! Kwani nimemkataa; maana Bwana havitazami vile, mtu anavyovitazama, kwani mtu huvitazama vilivyopo machoni, lakini Bwana huvitazama vilivyomo moyoni.
8
Kisha Isai akamwita Abinadabu, akampitisha machoni pa Samweli, naye akasema: Huyu naye siye, Bwana aliyemchagua.
9
Kisha Isai akampitisha Sama, lakini akasema: Huyu naye siye, Bwana aliyemchagua.
10
Vivyo hivyo Isai akawapitisha wanawe wote saba machoni pa Samweli, lakini Samweli akamwambia Isai: Hawa sio, Bwana aliowachagua.
11
Kisha Samweli akamwuliza Isai: Wanao wote ni hao tu? Akasema: Amesalia yule mdogo, naye anachunga kondoo. Samweli akamwambia Isai: Tuma, wamlete! Kwani hatutakaa mezani, mpaka atakapofika hapa.
12
Basi, akatuma, wakamleta, naye alikuwa mwekundu mwenye macho mazuri na umbo jema. Ndipo, Bwana alipomwambia: Haya! Umpake mafuta! Kwani huyu ndiye.
13
Samweli akaichukua pembe yake ya mafuta, akampaka mafuta katikati ya kaka zake. Ndipo, Roho ya Bwana ilipomjia Dawidi kuanzia siku hiyo, ikamkalia siku zote. Kisha Samweli akaondoka kwenda Rama.
14
Royo yake Bwana ikaondoka mwake Sauli, nayo roho mbaya iliyotoka kwa Bwana ikamhangaisha.
15
Ndipo, watumishi wa Sauli walipomwambia: Tazama, roho mbaya ya Mungu inakuhangaisha!
16
Wewe bwana wetu na uwaagize watumishi wako wanaokutumikia, watafute mtu aliye fundi wa kupiga zeze. Napo, itakapokujia ile roho mbaya ya Mungu, basi, akikupigia zeze kwa mkono wake, utaona vema.
17
Sauli akawaambia watumishi wake: Nitafutieni mtu anayejua vema kupiga zeze, kamleteni kwangu!
18
Mmoja wao wale vijana akajibu akisema: Nimemwona mwana wa Isai wa Beti-Lehemu, ya kuwa anajua kupiga zeze, tena ni fundi wa vita menye nguvu za kupigana vitani na za kusemea watu, ni mtu mzuri wa kupendeza, naye Bwana yuko pamoja naye.
19
Ndipo, Sauli alipotuma wajumbe kwa Isai na kumwambia: Mtume mwanao Dawidi achungaye kondoo, aje kwangu!
20
Isai akatoa punda wa kuchukua mzigo wa chakula na kiriba cha mvinyo, tena akampa mwana mbuzi mmoja, akavituma kwa Sauli mkononi mwa mwanawe Dawidi.
21
Ndivyo, Dawidi alivyokwenda kwake Sauli, akamfanyizia kazi. Sauli akampenda sana, akawa mchukua mata yake.
22
Sauli akatuma kwa Isai kwamba: Dawidi na akae kwangu, kwani macho yangu yanamwona kuwa mpole.
23
Ikawa kila mara, ile roho ya Mungu ilipomjia Sauli, Dawidi akalichukua zeze lake, akalipiga kwa mkono wake; ndipo, Sauli alipotulia na kuona vema, ile roho mbaya ikaondoka kwake.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31