bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 17
1 Samuel 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 18 →
1
Wafilisti wakavikusanya vikosi vyao kwenda vitani, wakakusanyika Soko katika nchi ya Yuda, wakapiga makambi Efesi-Damimu katikati ya Soko na Azeka.
2
Sauli naye na watu wa Waisiraeli wakakusanyika, wakapiga makambi kwenye Bonde la Mkwaju, wakajitengeneza kuja kupigana na Wafilisti.
3
Wafilisti wakawa wamesimama mlimani ng'ambo ya huko, nao Waisiraeli wakawa wamesimama ng'ambo ya huku, bonde likiwa katikati yao.
4
Katika makambi ya Wafilisti kukatokea jitu, jina lake Goliati wa Gati, urefu wake ulikuwa mikono sita na nusu.
5
Alikuwa amevaa kofia ya shaba kichwani, tena kifuani fulana ya chuma, nao uzito wa hiyo fulana ulikuwa sekeli 5000, ndio frasila 5 za shaba.
6
Miguuni alikuwa amevaa shaba vilevile penye miundi, namo mabegani kikingio cha shaba.
7
Uti wa mkuki wake ulikuwa nguzo kama mti wa mfuma nguo, nayo ncha ya chuma ya mkuki wake ilikuwa sekeli 600, ndio nusu kubwa ya frasila ya chuma; naye mchukua ngao humtangulia.
8
Akaja kusimama mbele akipaza sauti sana na kuwaita Waisiraeli waliojipanga, akawaambia: Mbona mmetoka, mkajipanga kupiga vita? Mimi si Mfilisti? Nanyi sio watu wa Sauli? Chagueni mtu wa kwenu, ashuke kuja kwangu!
9
Akiweza kupigana na mimi na kunishinda, basi, tutakuwa watumwa wenu; lakini mimi nikimweza na kumshinda, ninyi mtakuwa watumwa wetu, mtutumikie.
10
Kisha huyo Mfilisti akasema: Siku hii ya leo nimewabeza Waisiraeli waliojipanga, nikiwaambia: Nipeni mtu, tupigane naye!
11
Sauli na Waisiraeli wote walipoyasikia hayo maneno ya huyo Mfilisti wakaingiwa na vituko, wakaogopa sana.
12
Dawidi alikuwa mwana wa yule mtu wa Efurata, ndio Beti-Lehemu wa Yuda, jina lake Isai, aliyekuwa mwenye wana wanane; siku zile za Sauli mwenyewe alikuwa mzee mwenye miaka kuliko wengine.
13
Lakini wana watatu wakubwa wa Isai walikuwa wamemfuata Sauli kwenda vitani, nayo majina yao hawa wanawe watatu waliokwenda vitani ni haya: wa kwanza ni Eliabu, wa pili Abinadabu, wa tatu Sama.
14
Naye Dawidi alikuwa mdogo; kwa kuwa wale wakubwa watatu walikuwa wamemfuata Sauli,
15
Dawidi akatoka mara kwa mara kwake Sauli kwenda kuchunga kondoo wa baba yake huko Beti-Lehemu, kisha akarudi.
16
Lakini yule Mfilisti akatoka asubuhi na jioni siku 40 akija kujisimamisha papo hapo.
17
Kisha Isai akamwambia mwanawe Dawidi: Wapelekee kaka zako mzigo huu wa bisi na hii mikate kumi. Upige mbio, uifikishe upesi kambini kwa kaka zako!
18
Navyo hivi vikate kumi vya maziwa yaliyoganda umpelekee mkuu wa elfu, upate kuwatazama kaka zako, kama hawajambo, nao na wakupe kitu cha kwao, ukilete!
19
Kwani Sauli nao hao na Waisiraeli wote walikuwako kule kwenye Bonde la Mkwaju wakipigana na Wafilisti.
20
Kesho yake Dawidi akaamka na mapema akimwachia mwangaliaji mwingine kondoo na mbuzi, akavichukua alivyopewa, akaenda zake, kama Isai alivyomwagiza; akafika penye magari, vikosi vilipotoka kujipanga na kupiga yowe za vita.
21
Nao Waisiraeli wakajipanga ng'ambo ya huku, nao Wafilisti ng'ambo ya huko, wakaelekeana.
22
Dawidi akautua ule mzigo, akauacha mkononi mwake mlinda mizigo, akakimbilia hapo, walipojipanga, alipofika akaamkiana na kaka zake.
23
Akingali katika kusema nao, mara hapo, Wafilisti walipojipanga, lile jitu likatokea, jina lake Goliati, Mfilisti wa Gati, akayasema maneno yaleyale; Dawidi naye akayasikia.
24
Watu wote wa Waisiraeli walipomwona mtu huyo wakamkimbia wote, kwani wakaogopa sana.
25
Kukawa na mtu wa Kiisiraeli akasema: Mmemwona huyo mtu aliyepanda? Hupanda tu kuwatweza Waisiraeli. Mtu atakayempiga mfalme atampa mali nyingi, hata mwanawe wa kike atampa, awe mkewe, nao mlango wa baba yake utafunguliwa, usitoe kodi kwao Waisiraeli.
26
Dawidi akawauliza wale watu waliosimama pamoja naye akisema: Mtu akimpiga huyo Mfilisti na kuiondoa soni kwao Waisiraeli atafanyiziwa nini? Kwani huyo Mfilisti asiyetahiriwa ni mtu gani akiwatweza wapiga vita wa Mungu aliye Mwenye uzima?
27
Watu wale wakamwambia neno lilelile la kwamba: Hivi ndivyo, atakavyofanyiziwa mtu atakayempiga.
28
Kaka yake Eliabu aliposikia, alivyosemezana na wale watu, makali yake Eliabu yakawaka moto kwa kumkasirikia Dawidi, akamwuliza: Umeshukia nini? Tena hivyo vikondoo vyetu umemwachia nani huko nyikani? Mimi ninayajua majivuno yako na ubaya wa moyo wako, kwani umeshuka tu kutazama vita.
29
Dawidi akamwuliza: Nimekosa nini sasa? Hilo si neno la kuuliza tu?
30
Kisha akaondoka hapo pake, akaja pengine kuulizana na watu neno lilo hilo, nao wakamjibu maneno yayo hayo ya kwanza.
31
Watu walipoyasikia, Dawidi aliyoyasema, wakaja kwa Sauli kumsimulia habari hizo, kisha wakamchukua.
32
Dawidi akamwambia Sauli: Mtu asipotelewe na moyo kwa ajili yake yeye! Mtoto wako atakwenda kupigana na huyo Mfilisti.
33
Sauli akamwambia Dawidi: Hutaweza kumwendea huyo Mfilisti, upigane naye, kwani u kijana, naye yeye ni mpiga vita tangu utoto wake.
34
Dawidi akamwambia Sauli: Mtoto wako alipokuwa anachunga kondoo wa baba yake, basi, simba au chui walipokuja kukamata kondoo kundini,
35
nikatoka kuwafuata, nikawapiga, nikawaopoa vinywani mwao; kama aliniinukia, nikamkamata ndevu zake, nikampiga, hata nikamwua.
36
Kama mtoto wako alivyowapiga simba na chui, vivyo hivyo hata huyo Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwani amewatweza wapiga vita wa Mungu aliye Mwenye uzima.
37
Kisha Dawidi akasema: Bwana aliyeniponya mikononi mwa simba namo mikononi mwa chui ndiye atakayeniponya namo mkononi mwa huyo Mfilisti. Ndipo, Sauli alipomwambia Dawidi: Basi, nenda! Bwana awe nawe!
38
Sauli akamvika Dawidi mavazi yake ya vitani, kichwani pake akamtia kofia ya shaba, akamvika hata fulana ya chuma.
39
Dawidi akajifunga nao upanga wake juu ya hayo mavazi ya vitani. Lakini alipotaka kwenda, kwani alikuwa hajavijaribu, Dawidi akamwambia Sauli: Siwezi kwenda nayo haya, kwani sikuyajaribu bado; kisha Dawidi akayavua, akayaweka,
40
akaichukua fimbo yake mkononi mwake, akajichagulia mtoni vijiwe vitano vilivyoviringana vizuri, akavitia katika mkoba, aliokuwa nao, maana ni mfuko wake, akashika nalo kombeo, kisha akamwendea yule Mfilisti.
41
Yule Mfilisti naye akaja kumfikia Dawidi karibu, naye mchukua ngao akamtangulia.
42
Yule Mfilisti alipochungulia, amwone Dawidi, akambeza, kwa kuwa ni kijana bado, tena ni mwekundu na mwenye umbo zuri.
43
Ndipo, yule Mfilisti alipomwambia Dawidi: Mimi ni mbwa, ukinijia na fimbo? Kisha Mfilisti akamwapiza Dawidi na kuitaja miungu yake.
44
Mfilisti akamwambia Dawidi: Njoo kwangu! Nyama za mwili wako nitawapa ndege wa angani na nyama wa porini!
45
Lakini Dawidi akamwambia Mfilisti: Wewe unanijia na kushika upanga na mkuki na ngao, lakini mimi ninakujia katika Jina la Bwana Mwenye vikosi, aliye Mungu wao wapiga vita vya Waisiraeli, uliyemtukana!
46
Siku hii ya leo Bwana amekutia mkononi mwangu, nikupige, nikukate kichwa mwilini pako, nayo mizoga ya vikosi vya Wafilisti siku hii ya leo nitawapa ndege wa angani na nyama wa porini, watu wote wa nchini wapate kujua, ya kuwa aliye Mungu yuko kwao Waisiraeli.
47
Nao wote wa mkutano huu watajua, ya kuwa Bwana haokoi kwa nguvu za upanga wala za mkuki, kwani vita hivi ni vyake Bwana, naye amewatia mikononi mwetu.
48
Ikawa, yule Mfilisti alipoinuka, aje kumfikia Dawidi karibu, Dawidi naye akapiga mbio, afike upesi hapo, walipojipanga, akutane na yule Mfilisti.
49
Dawidi akautia mkono wake upesi mkobani, akatoa humo kijiwe, akakitupa kwa kombeo, akampiga yule Mfilisti pajini, nacho kijiwe kikaingia pajini ndani; ndipo, alipoanguka kifudifudi hapo chini.
50
Hivyo ndivyo, Dawidi alivyomshinda yule Mfilisti kwa kombeo na kwa kijiwe, akampiga yule Mfilisti na kumwua pasipo kushika upanga mkononi mwake yeye Dawidi.
51
Kisha Dawidi akapiga mbio, akasimama pake yule Mfilisti, akauchukua upanga wake akiuchomoa alani mwake, akamwua kabisa na kukikata kichwa chake; Wafilisti walipoona, ya kuwa fundi wao wa vita amekufa, ndipo, walipokimbia.
52
Lakini watu wa Waisiraeli na Wayuda wakainuka, wakaondoka na kupiga yowe, wakawakimbiza Wafilisti mpaka kufika Gai na malango ya Ekroni, nao Wafilisti walioumizwa wakaanguka njiani kwenda Saraimu, hata Gati na Ekroni.
53
Kisha wana wa Isiraeli wakarudi walipokwisha kuwafukuza sana Wafilisti, wakayateka yaliyokuwapo makambini mwao.
54
Dawidi akakichukua kichwa chake yule Mfilisti, akakipeleka Yerusalemu, lakini mata yake akayaweka hemani mwake.
55
Sauli alipoona, Dawidi alivyotoka, akutane na yule Mfilisti, akamwuliza Abineri, mkuu wa vikosi: Huyu kijana ni mwana wa nani? Abineri akasema: Hivyo roho yako, mfalme, ilivyo nzima, sijui.
56
Mfalme akamwambia: Uliza, kama hili jana ni mwana wa nani?
57
Dawidi aliporudi akiisha kumwua yule Mfilisti, Abineri akamchukua, akampeleka kwa Sauli, akikishika kichwa chake yule Mfilisti mkononi mwake.
58
Sauli akamwuliza: Wewe kijana, u mwana wa nani? Dawidi akasema: Ni mwana wa mtumishi wako Isai wa Beti-Lehemu.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31