bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 19
1 Samuel 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 20 →
1
Sauli akala njama na mwanawe Yonatani na watumishi wake wote ya kumwua Dawidi. Lakini Yonatani, mwana wa Sauli, alikuwa amependezwa sana na Dawidi.
2
Kwa hiyo Yonatani akampasha Dawidi habari kwamba: Baba yangu Sauli anatafuta njia ya kukuua; sasa ujiangalie kesho! Kaa mafichoni na kujificha kabisa!
3
Mimi nitatoka, nisimame kando yake baba yangu huko shambani, utakakokuwa, niseme na baba yangu kwa ajili yako, nipate habari za kukupasha wewe.
4
Kisha Yonatani akamsemea mema kwa baba yake Sauli kwamba: Mfalme asije kumkosea mtumishi wake Dawidi! Kwani hakukukosea neno, ila amekufanyizia mema sana.
5
Alipokwenda kumwua yule Mfilisti alijitoa mwenyewe; ndipo, Bwana alipowapatia Waisiraeli wote wokovu mkubwa, nawe ukaviona, ukafurahi. Mbona unataka kujikosesha kwa kumwaga damu ya mtu asiyekosa ukimwua Dawidi bure tu?
6
Sauli akakiitikia kinywa cha Yonatani, yeye Sauli akaapa kwamba: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, hatauawa kabisa!
7
Kisha Yonatani akamwita Dawidi, akamsimulia maneno haya yote; kisha Yonatani akampeleka Dawidi kwa Sauli, akakaa kwake kama siku zote za mbele.
8
Vita vilipoendelea kuwapo, Dawidi akatoka kupigana na Wafilisti, akawapiga pigo kubwa, nao wakamkimbia.
9
Ndipo, ile roho mbaya ya Bwana ilipomjia Sauli, naye alikuwa anakaa nyumbani mwake akishika mkuki wake mkononi, naye Dawidi alikuwa akimpigia zeze kwa mkono wake.
10
Sauli akataka kumchoma Dawidi ukutani kwa mkuki, lakini Dawidi akajiepusha, Sauli asimpate, mkuki ukauchoma ukuta tu. Ndipo, Dawidi alipokimbia kwa hivyo, alivyopona. Usiku huo
11
Sauli akatuma wajumbe kwenda kuivizia nyumba ya Dawidi, wapate kumwua asubuhi. Lakini mkewe Mikali akampasha Dawidi habari kwamba: Usipojiponya usiku huu, utauawa kesho!
12
Kisha Mikali akamshusha Dawidi dirishani, akaenda zake na kukimbia; ndivyo, alivyopona.
13
Kisha Mikali akakichukua kinyago cha nyumbani, akakilaza kitandani, kichwani pake akaweka mto wa manyoya ya mbuzi, akakifunika kwa nguo.
14
Sauli alipotuma wajumbe kumchukua Dawidi, akawaambia: Ni mgonjwa.
15
Sauli akawatuma wale wajumbe tena kumtazama Dawidi akiwaambia: Mleteni kwangu, akilala kitandani, nipate kumwua!
16
Wajumbe walipoingia nyumbani wakakiona kile kinyago, kimelala kitandani, nao mto wa manyoya ya mbuzi uko kichwani pake.
17
Sauli akamwuliza Mikali: Kwa sababu gani umenidanganya hivyo, ukamwacha mchukivu wangu, apone? Mikali akamwambia Sauli: Ameniambia: Niache, nijiendee! Mbona unataka nikuue?
18
Naye Dawidi alipopona kwa kukimbia akaenda Rama kwa Samweli, akamsimulia yote, Sauli aliyomfanyizia, kisha wakaenda yeye na Samweli, wakakaa Nayoti.
19
Sauli akapashwa habari za kwamba: Tazama, Dawidi yuko Nayoti kule Rama!
20
Ndipo, Sauli alipotuma wajumbe kumchukua Dawidi. Hao walipoona kundi la wafumbuaji wakifumbua mambo, naye Samweli akisimama kwao kama kiongozi wao, ndipo, roho ya Mungu ilipowajia wajumbe wa Sauli, nao wakafumbua mambo.
21
Walipompasha Sauli habari hizi, akatuma wajumbe wengine, lakini nao wakaja kufumbua mambo. Ndipo, Sauli alipoendelea kutuma wajumbe mara ya tatu, lakini nao wakaja kufumbua mambo.
22
Kisha naye mwenyewe akaenda Rama; alipofika penye shimo kubwa la maji lililoko Seku akauliza kwamba: Samweli na Dawidi wako wapi? Wakamwambia: Utawaona Nayoti kule Rama.
23
Alipokwenda Nayoti kule Rama, yeye naye roho ya Mungu ikamjia; ndipo, alipokwenda hapo njiani na kufumbua mambo, hata akifika Nayoti kule Rama.
24
Ndipo, yeye naye alipoyavua mavazi yake, naye akafumbua mambo mbele ya Samweli, akalala chini mwenye uchi mchana huo wote na usiku huo wote, kwa hiyo watu husema: Kumbe Sauli naye yumo katika wafumbuaji!
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31