bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 21
1 Samuel 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 22 →
1
Dawidi akaja Nobe kwa mtambikaji Ahimeleki; Ahimeleki akashikwa na woga, akamwendea Dawidi njiani, akamwuliza: Mbona unakuja peke yako, usiwe na mtu wa kufuatana na wewe?
2
Dawidi akamwambia mtambikaji Ahimeleki: Mfalme ameniagiza neno na kuniambia: Mtu asilijue hili neno, ninalokutuma nililokuagiza! Wako vijana, niliowaagiza, waje mahali fulani.
3
Una chakula gani sasa? Kama ni mikate mitano, nipe, niende nayo, au cho chote kingine kinachoonekana!
4
Mtambikaji akamjibu Dawidi akisema: Sinayo mikate ya kula, ila iko mikate mitakatifu tu; ingewezekana, kama vijana wale wangalijiangalia, wasiguse wanawake.
5
Dawidi akamjibu mtambikaji akimwambia: Tangu jana na juzi tumenyimwa wanawake; napo, nilipotoka, miili ya vijana hao ilikuwa mitakatifu, nayo hii njia yetu ni ya kujiendea tu, pasipo shaka wametakata miili yao hata leo.
6
Ndipo, mtambikaji alipompa ile mikate mitakatifu, kwani haikuwako mikate mingine, isipokuwa ile mikate, aliyowekewa Bwana, nayo huondolewa machoni pa Bwana, wakiweka hapo mikate mingine yenye moto; ni siku ileile, hiyo ya mbele inapochukuliwa.
7
Siku ile kukawako mmoja wao watumishi wa Sauli, naye alikuwa ametengwa, akae machoni pa Bwana, jina lake Doegi wa Edomu aliyekuwa mkuu wa wachungaji wa Sauli.
8
Kisha Dawidi akamwuliza Ahimeleki: Hunao mkuki au upanga? Kwani sikuchukua upanga wangu wala mata yangu mengine, kwani shauri la mfalme lilikuwa la haraka.
9
Mtambikaji akamwambia: Upanga wa yule Mfilisti Goliati, uliyemwua katika Bonde la Mkwaju, uko, umezingwa na nguo, uko nyuma ya kisibau cha mtambikaji; kama unataka kuuchukua, jichukulie! Kwani hakuna mwingine, usipokuwa huo. Dawidi akasema: Hakuna mwingine wa kufanana nao, nipe, niuchukue!
10
Kisha Dawidi akaondoka, akamkimbia Sauli siku hiyo, akaja kwa Akisi, mfalme wa Gati.
11
Watumishi wa Akisi wakamwambia: Kumbe huyu siye Dawidi, mfalme wa nchi ile? Siye yeye, waliyemwimbia na kuitikiana na kumchezea kwamba: Sauli ameua elfu lake, lakini Dawidi ameua maelfu yake kumi?
12
Dawidi alipoyafikisha maneno haya moyoni mwake, akamwogopa sana Akisi, mfalme wa Gati.
13
Kwa hiyo akayageuza mawazo yake mbele yao, akawa kama mwenye wazimu huko kwao, akaipiga milango ya lango la mji kama ngoma, nayo mate yake akayachuruzisha madevuni mwake.
14
Akisi akawaambia watumishi wake: Mnamwona mtu huyu kuwa mwenye kichaa, sababu gani mmemleta kwangu?
15
Je? Mimi nimekosa wenye kichaa, mkimleta huyu, anitolee wazimu wake? Ananijiliaje nyumbani mwangu?
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31