bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 24
1 Samuel 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 25 →
1
Ikawa, Sauli aliporudi kwa kuwafuatia Wafilisti, wakampasha habari kwamba: Tazama, Dawidi yuko Engedi nyikani!
2
Ndipo, Sauli alipochukua watu 3000 waliochaguliwa katika Waisiraeli wote, akaenda kumtafuta Dawidi na watu wake kwenye miamba ya minde.
3
Alipofika njiani kwenye mazizi ya kondoo na mbuzi, kulikuwako pango; Sauli akaingia humo kuifunika miguu yake. Namo humo pangoni ndani Dawidi alikuwamo akikaa na watu wake.
4
Watu wa Dawidi wakamwwambia: Basi, leo hivi ni siku hiyo, Bwana aliyokuambia: Utaniona mimi, nikimtia mchukivu wako mkononi mwako, umfanyizie yaliyo mema machoni pako. Dawidi akainuka, akakata pindo la kanzu yake Sauli, asivijue.
5
Lakini baadaye moyo ukamkung'uta Dawidi, kwa kuwa amelikata pindo la kanzu ya Sauli;
6
akawaambia watu wake: Bwana na anizuie kabisa nisimfanyizie bwana wangu, Bwana aliyempaka mafuta, jambo kama hilo la kuuinua mkono wangu, nimguse tu! Kwani Bwana alimpaka mafuta yeye.
7
Kwa maneno haya Dawidi akawazuia watu wake, hakuwapa ruhusa kumwinukia Sauli. Kisha Sauli akaondoka mle pangoni, akaenda zake.
8
Baadaye Dawidi naye akaondoka, akatoka mle pangoni, akapaza zauti nyuma yake Sauli kwamba: Bwana wangu mfalme! Sauli alipotazama nyuma, Dawidi akamwinamia mara mbili na kumwangukia chini.
9
Kisha Dawidi akamwambia Sauli: Mbona unayasikiliza maneno ya watu kwamba: Tazama, Dawidi anakutakia mabaya?
10
Tazama! Leo hivi macho yako yanaweza kuona, ya kuwa Bwana amekutia mkononi mwangu mle pangoni. Lakini watu waliposema, nikuue, jicho langu likakuonea uchungu, nikasema: Sitaukunjua mkono wangu, nimguse tu bwana wangu, kwani Bwana alimpaka mafuta.
11
Baba yangu, tazama, uone nawe! Pindo la kanzu yako limo mkononi mwangu! Kwani nilipolikata hili pindo la kanzu yako, sikukuua. Kwa kuliona ujue, ya kuwa mkononi mwangu hamna kibaya wala kipotovu, wala sijakukosea. Mbona wewe unaniwinda, unipate?
12
Bwana na atuamue, mimi na wewe! Yeye Bwana na anilipizie kwako! Lakini mkono wangu hautakuinukia.
13
Ni hivyo, kama fumbo la kale linavyosema: Kwao waovu hutoka uovu, lakini mkono wangu hautakujia.
14
Mfalme wa Waisiraeli ametoka kumtafuta nani? Wewe unamkimbiza nani? Ni mbwa mfu au kiroboto kimoja tu!
15
Basi, Bwana na atuhukumu na kutuamua mimi na wewe akitutazama! Kisha na anigombee huu ugomvi wangu na kuniponya mkononi mwako!
16
Ikawa, Dawidi alipokwisha kumwambia Sauli maneno haya, Sauli akasema: Kumbe hii si sauti yako, mwanangu Dawidi? Kisha Sauli akapaza sauti na kulia machozi.
17
Akamwambia Dawidi: Wewe u mwenye wongofu kuliko mimi, kwani wewe umenifanyizia mema mimi niliyekufanyizia mabaya.
18
Wewe umeuonyesha leo huo wema, ulionifanyizia, usiponiua, Bwana aliponitoa na kunitia mkononi mwako.
19
Je? Mtu akimwona mchukivu wake atamwacha, ajiendee, pasipo kumfanyizia kibaya? Bwana na akulipe na kukupatia mema kwa hayo, uliyonifanyizia leo.
20
Sasa tazama! Ninajua, ya kuwa utapata kuwa mfalme, nao ufalme wa Waisiraeli utashupaa kwa nguvu za mkono wako.
21
Sasa uniapie ukimtaja Bwana, ya kuwa hutawaangamiza wao wa uzao wangu watakaokuwa nyuma yangu, wala hutalitowesha jina langu katika mlango wa baba yangu.
22
Dawidi akamwapia Sauli haya, kisha Sauli akaenda nyumbani kwake, naye Dawidi akapanda gengeni pamoja na watu wake.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31