bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 31
1 Samuel 31
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
1
Wafilisti walipopigana na Waisiraeli, watu wa Waisiraeli wakawakimbia Wafilisti kwa madonda waliyopigwa, wakaanguka wakafa kule mlimani kwa Gilboa.
2
Wafilisti wakawafuata na kuandamana na Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua wana wa Sauli: Yonatani na Abinadabu na Malkisua.
3
Mapigano yakawa makali hapo, Sauli alipokuwa; wapiga mishale walipomwona, akaumizwa sana nao wapiga mishale.
4
Ndipo, Sauli alipomwambia mchukua mata yake: Uchomoe upanga wako, unichome nao, hao wasiotahiriwa wasije kunichoma na kunichezea vibaya! Mchukua mata yake alipokataa kwa kuogopa sana, Sauli akausimika upanga, akauangukia.
5
Mchukua mata yake alipoona, ya kuwa Sauli amekufa, naye akauangukia upanga wake, akafa pamoja naye.
6
Ndivyo, Sauli alivyokufa na wanawe watatu na mchukua mata yake na watu wake wote, wote pia siku hiyohiyo.
7
Watu wa Waisiraeli waliokaa ng'ambo ya huko ya hilo bonde na ng'ambo ya huko ya Yordani walipoona, ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia nao; kisha Wafilisti wakaja, wakakaa humo.
8
Ikawa kesho yake, Wafilisti walipokuja kuwapambua waliouawa wakamwona Sauli na wanawe watatu, jinsi walivyokufa mlimani kwa Gilboa.
9
Wakamkata kichwa, wakampambua mata yake, wakatuma wajumbe kwenda po pote katika nchi ya Wafilisti na kuyatangaza penye nyumba ya vinyago vyao, hata kwa watu.
10
Mata yake wakayaweka nyumbani mwa Maastaroti, nao mzoga wake wakautungika bomani kwa mji wa Beti-Sani.
11
Wenyeji wa Yabesi wa Gileadi walipoyasikia, Wafilisti waliyomfanyizia Sauli,
12
Wakaondoka watu wote walioweza kupiga vita, wakaenda usiku wote, wakauchukua mzoga wa Sauli, nayo mizoga ya wanawe pale bomani kwa Beti-Sani, kisha wakarudi na kuipeleka Yabesi, wakaiteketeza huko kwa moto.
13
Kisha wakaichukua mifupa yao, wakaizika chini ya miombo kwao Yabesi, wakafunga mfungo siku saba.
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31