bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Corinthians 10
2 Corinthians 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 11 →
1
Nawaonya ninyi kwa upole na kwa utu wa Kristo mimi Paulo mwenyewe niliye mnyenyekevu kwenu nikiwaona, nikawatolea makali nikiwa mbali!
2
Nawaomba, msinishurutishe kuyatumia hayo makali nitakapofika. Mwenyewe nadhani, yafaa kuwaendea na nguvu wale wachache wanaotudhania, ya kwamba sisi huendelea na kufuata tamaa za miili.
3
Kwani hata tunapoendelea katika miili hatujigombei, kama miili itakavyo.
4
Kwani mata ya magombano yetu si ya kimwili, lakini yako na nguvu ya Kimungu, yaweza kubomoa ngome kama hapo, yanaponyenyekeza mawazo yote
5
ya kujikweza na kuuinukia utambuzi wa Mungu, au yanapoteka mawazo yote, yaje kumtii Kristo.
6
Nasi tuko tayari kumlipiza kila mtu asiyetii, hapo mtakapokuwa mmemaliza kutii.
7
Yatazameni yanayoonekana machoni! Mtu akijishikiza kwa kwamba: Ni wa Kristo, na atie hili nalo moyoni la kwamba: Kama yeye alivyo wa Kristo, vivyo hivyo nasi!
8
Ikiwa nafuliza kujivunia nguvu yetu, Bwana aliyotupa, tuwajenge, tusiwajengue, napo hapo sitashindika kuwa mwongo,
9
wala sitafanana na mtu anayewaogopesha tu kwa barua.
10
Kwani wako wanisengenyao kwamba: Barua zake ni ngumu zenye nguvu, lakini akiwapo kwa mwili ni mnyonge, nayo maneno yake hubezeka.
11
Aliye hivyo na alifikiri hili: tunavyovisema kwa barua tusipokuwapo, ndivyo, tutakavyovitimiza tutakapokuwapo.
12
Kwani hatujipi moyo wa kujihesabu au kujifananisha nao walioko, wakijisifu wenyewe. Lakini hao hakuna, wajuacho maana, kwani kipimo chao cha kujipima ndio wenyewe tu, nao mfano wa kujifananisha nao ndio wenyewe tu.
13
Lakini sisi hatutaki kujivuna pasipo kipimo, ila kipimo chetu ni mpaka, Mungu aliotukatia; hivyo tulifika hata kwenu.
14
Kwani hatujitanui wenyewe kama wasiowafikia, maana hata kwenu ni sisi waliotangulia kuwatangazia Utume mwema wa Kristo.
15
Nasi hatuupiti mpaka, tujivunie masumbuko yao wengine, lakini kumtegemea Mungu kutakapokulia kwenu, papo hapo tunangojea mipaka yetu, tuliyowekewa, ikuzwe kuipita ile ya kwenza,
16
tupate kuutangaza Utume mwema hata kwao wakaao mbali kuwapita ninyi. Lakini hatutafuti majivuno tukiingia nchi iliyoisha kupigiwa hiyo mbiu njema na wengine.
17
Lakini mwenye kujivuna na ajivunie kuwa wa Bwana!
18
Kwani anayejisifu mwenyewe siye mkweli, ila yule anayesifiwa na Bwana.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13