bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Corinthians 11
2 Corinthians 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 12 →
1
Ingefaa, mnivumilie, nikitumia upuzi kidogo; najua, mtanivumilia.
2
Kwani wivu, ninaouona kwa ajili yenu, ni wa Kimungu; maana naliwaposea ninyi mume mmoja, ni Kristo, niwapeleke kwake kuwa mwanamwali mwenye kutakata.
3
Lakini kama nyoka alivyomdanganya Ewa kwa werevu wake mbaya, ninao woga wa kwamba: Vivyo hivyo nayo mawazo yenu yataangamizwa, msiweze tena kuandamana na Kristo peke yake tu na kumng'alia.
4
Kwani mtu anapokuja kwenu na kutangaza Yesu mwingine, tusiyemtangaza sisi, au mnapopata roho nyingine, msiyoipata, au mnapotangaziwa Utume mwema mwingine, msioupokea, basi, ninyi huvumilia vizuri.
5
Lakini nadhani, hakuna nishindwacho nao wale wajipao macheo yote ya utume.
6
Hata nikiwa mpumbavu wa kusema, si mpumbavu wa kutambua, nanyi mmetuona kuwa hivyo po pote katika mambo yote.
7
Au nimekosa, nilipojinyenyekeza, ninyi mpate kuwa wakubwa? Au nimekosa, kwa kuwa nimewatangazia Utume mwema wa Mungu pasipo malipo?
8
Wateule wengine nimewapokonya na kutwaa matunzo, nipate kuwatumikia ninyi.
9
Napo, nilipokuwako kwenu, nikawa nimekosa vyakula, hakuna, niliyemsumbua. Kwani ndugu waliokuja toka Makedonia waliniongezea, nilivyovikosa. Katika mambo yote nimejiangalia, nikae kwenu pasipo kuwasumbua, navyo ndivyo, nitakavyojiangalia.
10
Kwa hivyo ukweli wake Kristo ulivyomo mwangu, hayo majivuno yangu hayatavunjika katika nchi za Akea.
11
Kwa sababu gani? Kwamba siwapendi ninyi? Mungu amevijua!
12
Lakini nifanyalo nitafuliza kulifanya, niiumbue mizungu yao wale wanaotafuta mizungu ya kujivunia kwamba: Sisi tulivyo, nao huonekana kuwa vivyo hivyo.
13
Kwani hao ndio mitume wa uwongo na wafanya kazi wajanja, hujigeuza kuwa mitume wa Kristo.
14
Nalo hili silo la kustaajabu. Kwani Satani mwenyewe hujigeuza kuwa malaika mwenye mwanga.
15
Kwa hiyo si neno kubwa, watumishi wake nao wakijigeuza kuwa watumishi wenye wongofu, lakini mwisho wao utakuwa umepatana na kazi zao.
16
Nasema tena, mtu asiniwazie kuwa mpuzi. Kama hamtaki, vilevile nipokeeni kama mpuzi, nijivune nami kidogo!
17
Ninayoyasema sasa, siyasemi kuwa maneno ya Bwana, ila nayasema kama ya upuzi tu kwa hivyo, tulivyoyafikia majivuno.
18
Kwa sababu wengi hujivuna kimtu, nami nitajivuna.
19
Kwani ninyi mlio wenye akili hupenda kuwavumilia wapuzi.
20
Mwavumilia, mtu akiwafanya watumwa, akiwala, akiyatwaa yaliyo yenu, akijikuza, akiwapiga usoni.
21
Naona soni nikisema: Hayo hatuyawezi, tu wanyonge; lakini jambo lo lote, mtu alilojipa moyo wa kujivunia, (nasema kipuzi) nami najivunia lilo hilo.
22
Ni Waebureo? Hata mimi. Ni Waisiraeli? Hata mimi. Ni uzao wake Aburahamu? Hata mimi.
23
Ni watumishi wa Kristo? Mimi nawapita; nasema kama mwenye wazimu. Nimesumbuka kuwapita, nimefungwa kuwapita, nimepigwa kuwapita kabisa, mara nyingi nimetakiwa kufa.
24
Mara tano nalipata kwa Wayuda fimbo 40 kupungua moja,
25
mara tatu nalipigwa viboko, mara moja nalipigwa mawe, mara tatu chombo changu kimevunjika baharini, nikawamo kilindini usiku na mchana.
26
Safari zangu ni nyingi, nikapata masumbuko ya mito na masumbuko ya wanyang'anyi na masumbuko ya watu wa ukoo wetu na masumbuko ya wamizimu na masumbuko ya mijini na masumbuko ya nyikani na masumbuko ya baharini na masumbuko yaliyoko kwenye ndugu wa uwongo.
27
Nimeumia, mpaka nikachoka, nikikesheshwa mara nyingi, nikiumizwa na njaa na kiu, nikinyimwa mara nyingi vyakula, nikiwekwa penye baridi pasipo nguo.
28
Hayo ya nje hupitwa nayo yanijiayo kila siku, nikiwasumbukia wateule wote.
29
Yuko mnyonge asiyenitia unyonge nami? Yuko anayekwazwa, nisipoumizwa nami?
30
Nikishurutishwa kujivuna nitajivunia unyonge wangu.
31
Mungu, Baba wa Bwana Yesu, atukuzwaye kale na kale anajua: sisemi uwongo.
32
Huko Damasko mtawala watu wa mfalme Areta aliulinda mji wa Damasko, apate kunikamata.
33
Nami nikatolewa dirishani, nikashushwa katika kapu ukutani, nikaokoka mikononi mwake.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13