bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Corinthians 2
2 Corinthians 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 3 →
1
Lakini moyoni naliwaza hivi: Nisije tena kwenu mwenye sikitiko!
2
Kwani mimi nikiwasikitisha ninyi, yuko nani atakayenichangamsha, asipokuwa yule aliyesikitishwa nami?
3
Kwa sababu hii naliyaandika yale ya kwamba: Nitakapokuja nisisikitishwe nanyi mliopaswa na kunifurahisha; kwa maana ninyi nyote mmenipa moyo wa kwamba: Furaha yangu ni furaha yenu nyote.
4
Kwani naliwaandikia kwa maumivu mengi, moyo ukanipotelea, vikanitoa machozi mengi, siko kwamba msikitishwe, ila mpate kuutambua upendo unaonikaza kuwapenda ninyi kuliko wengine.
5
Lakini kama yuko aliyesikitisha, hakunisikitisha mimi; ila fungufungu, maana nisiseme na kuyapita ya kweli, amewasikitisha ninyi nyote.
6
Aliye hivyo inamtosha, akionywa hivyo na wenzake walio wengi.
7
Kisha imewapasa ninyi kumwendea kwa upole na kumtuliza moyo, asididimizwe, masikitiko yakimshinda.
8
Kwa hiyo nawabembeleza ninyi, mmwonyeshe, ya kuwa mwampenda.
9
Kwani kwa hiyo naliwaandikia, nipate kuutambua welekevu wenu, kama mnatii katika mambo yote.
10
Lakini mmwachiliaye neno, hata mimi humwachilia. Kwamba hata mimi, ikiwa nimemwachilia mtu neno, nimemwachilia kwa ajili yenu machoni pa Kristo,
11
maana tusidanganywe na Satani; kwani mizungu yake hatukosi kuijua.
12
Hapo, nilipofika Tiroa kuutangaza Utume mwema wa Kristo, nikafunguliwa mlango kwa nguvu ya Bwana;
13
lakini sikuona utulivu moyoni mwangu, kwa kuwa sikumkuta ndugu yangu Tito; kwa hiyo nikaagana nao, nikatoka kwenda Makedonia.
14
Lakini Mungu atukuzwe anayetupa kushinda siku zote, tukiwa katika Kristo! Kwa hivyo, tunavyomtumikia yeye, hutokeza po pote waziwazi, ya kuwa wenye kumtambua wafanana na maua yanukayo vizuri.
15
Kwani tukawa mbele yake Mungu kama manukato mazuri ya Kristo kwao wanaookoka, nako kwao wanaoangamia:
16
hao tunawanukia kama wenye kutoka kufani wanaorudi kufani, lakini wale tunawanukia kama wenye kutoka uzimani wanaorudi uzimani. Yuko nani atakayeyaweza hayo.
17
Kwani sisi hatufanani nao wale wengi wanaolichuuzia Neno la Mungu, ila kwa ung'avu wa mioyo, tulioupata kwa Mungu, tunasema kama watu walio pamoja na Kristo mbele yake Mungu.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13