bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Corinthians 3
2 Corinthians 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 4 →
1
Je? Tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunatumia kama wengine barua za kusifiwa za kuwapelekea au za kupewa nanyi?
2
Ninyi m barua yetu iliyoandikwa mioyoni mwetu, inatambulikana, maana inasomwa nao watu wote.
3
Vyajulikana, ya kuwa m barua ya Kristo iliyotungwa na sisi, tulipowatumikia; haikuandikwa kwa wino, ila kwa Roho ya Mungu aliye Mwenye uzima; tena haikuandikwa katika vibao vya mawe, ila katika vibao vilivyo mioyo ya watu.
4
*Lakini Kristo ndiye aliyetupa shikizo kama hili kwake Mungu.
5
Huku siko kwamba: Twafaa kuwaza neno lo lote kwa kulitoa mioyoni mwetu; kama liko, tuliwezalo, tutagawiwa na Mungu.
6
Naye ndiye aliyetupa kuwa watumishi wafaao wa Agano Jipya lisilo la andiko, ila la Roho. Kwani andiko huua, lakini Roho hutupatia uzima.
7
Nao utumishi wa mambo yenye kuua, yaliyokuwa yameandikwa na kuchorwa maweni, ulikuwa na utukufu wake, ukawazuia wana wa Isiraeli kuutazama uso wake Mose kwa ajili ya utukufu wa uso wake uliokuwa wa kutoweka tena.
8
Je? Utumishi wa Roho hautakuwa na utukufu kuupita ule?
9
Kwani utumishi utupatiao hukumu ukiwa na utukufu, utumishi utupatiao wongofu utakuwa na utukufu ulio mkuu zaidi kuliko ule.*
10
Kwani utukufu ule uliokuwa wa kifungufungu tu tukiufananisha na utukufu huu uzidio kabisa tutasema: Ule sio utukufu!
11
Kwani chenye kutoweka kikiwa na utukufu, chenye kuwapo kitakuwa na utukufu uupitao ule.
12
*Kwa kuwa wenye kingojeo kama hiki sisi hutumia mioyo isiyojua woga kamwe.
13
Nasi hatufanyi kama Mose aliyeufunika uso wake kwa mharuma, wana wa Isiraeli wasipate kuutazama mwisho wa yale yaliyo yenye kutoweka.
14
Lakini mawazo yao yakashupazwa. Kwani mpaka siku ya leo wakilisoma Agano la Kale, liko limefunikwa vivyo hivyo, lisiwafunukie kwamba: Limetimilia katika Kristo.
15
Ila mpaka leo mioyo yao iko imefunikwa, Mose akisomwa.
16
Lakini hapo, watakapomgeukia Bwana, ndipo, kile kifuniko kitakapoondolewa.
17
Naye Bwana ndiye Roho; napo, Roho ya Bwana ilipo, ndipo, vyote vinapofunguliwa.
18
Lakini nasi sote tunautazama utukufu wa Bwana kwa macho yasiyofunikwa, kama twauona katika kioo; ndivyo, tunavyogeuzwa, tufanane naye, tukipewa utukufu kwa utukufu, tuwe kama watu waliogeuzwa na Bwana mwenyewe aliye Roho.*
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13