bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Corinthians 4
2 Corinthians 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 5 →
1
Kwa sababu tumepewa utumishi huo, nasi kwa hivyo, tulivyohurumiwa, hatuchoki;
2
tukayakataa mambo ya kufichaficha, maana ni yenye soni, kwani hatuendelei kwa werevu mbaya, wala hatuchanganyi Neno la Mungu na uwongo. Ila kwa hivyo, tunavyoyafumbua yaliyo ya kweli, twajitokeza waziwazi mioyoni mwa watu wote, wajue, ya kuwa tupo machoni pa Mungu.
3
*Lakini Utume wetu mwema ukiwa umefunikwa, uko umefunikwa kwao walio wenye kuangamia;
4
maana kwao ndiko, mungu wa nchini alikopofusha mawazo yao wasiomtegemea Mungu, wasiangazwe na mwangaza wa Utume mwema wa utukufu wake Kristo aliye mfano wa Mungu.
5
Kwani hatujitangazi sisi wenyewe, ila twatangaza kwamba: Kristo Yesu ni Bwana, nasi tu watumwa wenu kwa ajili ya Yesu.
6
Kwani Mungu aliyesema: Penye giza pamulike mwanga! ndiye aliyeiangaza mioyo yetu, ndani yao utokee mwanga unaotambulisha hata wengine utukufu wa Mungu uliopo usoni pake Kristo.*
7
Hiki kilimbiko chetu tunacho, lakini kimo katika vyombo vya udongo, kusudi zile nguvu nyingi zilizomo zijulike kwamba: Ndizo zake Mungu, kwamba: Hazotoki kwetu sisi.
8
Po pote twaumizwa, lakini hatusongeki; twahangaishwa, lakini hatuhangaikiki,
9
twakimbizwa, lakini hatuachwi peke yetu; twaangushwa chini, lakini hatuangamiki.
10
Po pote, tunapozunguka, twakujulisha kuuawa kwake Yesu miilini mwetu, kwamba nako kuishi kwake Yesu kupate kutokea miilini mwetu.
11
Kwani sisi tunaoishi hutolewa kila siku, tuuawe kwa ajili ya Yesu kwamba: Nako kuishi kwake Yesu kupate kutokea katika miili yetu iliyo yenye kufa.
12
Kwa hivyo kufa hupata nguvu mwetu, nako kuishi mwenu.
13
Lakini tulivyo wenye Roho yule yule wa kumtegemea Mungu, hutimia kwetu lililoandikwa la kwamba: Nilikuwa nimemtegemea Mungu, kwa hiyo nilisema. Nasi tunamtegemea Mungu, kwa hiyo husema.
14
Kwani twajua: Aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua hata sisi pamoja na Yesu, kisha atatuweka mahali, tutakapokuwa pamoja nanyi.
15
Kwani yote hutupata kwa ajili yenu, maana wenye kugawiwa kipaji wakiwa wengi, hao wengi nao watakazana kuutukuza utukufu wake Mungu.
16
Kwa hiyo hatuchoki, maana ikiwa miili yetu huchakaa, mioyo yetu hupata upya siku kwa siku.
17
Kwani maumivu yetu yaliyo ya sasa hivi tu, yapitayo upesi, huzidi kutupatia utukufu usiopimika, usio na mwisho,
18
tusipoyatazama yaonekanayo, ila yale yasiyoonekana. Kwani yaonekanayo hukaa siku chache tu, lakini yasiyoonekana ni ya kale na kale.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13