bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Corinthians 5
2 Corinthians 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 6 →
1
Kwani twajua, ya kuwa hivi vijumba vyetu, tupangamo nchini, vitakapobomolewa, tunayo majengo yaliyojengwa na Mungu, ni nyumba zisizojengwa na mikono ya watu, nazo hukaa kale na kale huko mbinguni.
2
Kwani hii ndiyo itupigishayo kite, tukitunukia, tuvikwe makao yetu yatokayo mbinguni;
3
maana tukiwa tumeyavika hatutaonekana kuwa wenye uchi.
4
Kwani sisi tuliomo humu kibandani hupiga kite kwa kulemewa, kwa sababu hatutaki kuvuliwa, ila hutaka kuvikwa, maana iliyo yenye kufa imezwe nayo yenye uzima.
5
Lakini aliyetutengenezea yaya haya ndiye Mungu aliyetupa Roho, awe rehani yetu.
6
Kwa hiyo yako, tunayoyatazamia siku zote tukijua, ya kuwa tukiwa mwetu miilini twamkalia Bwana mbali.
7
Kwani sisi hufanya mwendo kwa kumtegemea Mungu, siko kwa kuona.
8
Lakini kwa hayo, tunayoyatazamia, hupenda sana kuhama miilini, tupate kukaa kwetu kwa Bwana.
9
Kwa sababu hii twajihimiza, tumpendeze yeye, ikiwa tuwe bado mwetu miilini, au tuwe tumekwisha kuitoka.*
10
Kwani sisi sote sharti tutokee mbele ya kiti cha uamuzi cha Kristo, kila mmoja alipwe, aliyoyafanyiza alipokuwa mwilini, yakiwa mema au maovu.
11
Kwa sababu twajua, ya kuwa Bwana huogofya, twawaonya watu, lakini Mungu ndiye, tumtokeaye hivyo, tulivyo. Lakini ninacho kingojeo cha kwamba: Mioyo yenu inajua, ya kuwa nayo tumeitokea hivyo, tulivyo.
12
Hatujisifu tena mbele yenu, ila twataka kuwapa ninyi sababu ya kujivuna kwa ajili yetu, mpate kuwajibu wale wanaojivunia yaliyo machoni tu, yasiyo namo mioyoni.
13
Kwani tulipokuwa kama wenye wazimu, ni kwa ajili ya Mungu; tena tunapoerevuka, ni kwa ajili yenu.
14
*Kwani upendo wa Kristo hutuhimiza sisi, tukawaza hivyo: Mmoja alipokufa kwa ajili yao wote, kwa hiyo wote wamekwisha kufa.
15
Naye alipokufa kwa ajili yao wote alitaka, walio hai wasijikalie wenyewe, ila wamkalie yeye aliyekufa kwa ajili yao, kisha akafufuliwa.
16
Kwa hiyo tangu sasa hakuna, tunayemjua kimwili. Ikiwa tulimtambua Kristo kimwili, sasa hatumtambui tena hivyo.
17
Kwa hiyo mtu akiwa anaye Kristo, amekuwa kiumbe kipya. Yake ya kale yamepita; ukimtazama, yote yamekuwa mapya.
18
Nayo yote hutoka kwa Mungu; ndiye aliyetupatanisha sisi naye yeye, Kristo alipojitoa. Kisha akatupa kuyatumikia hayo mapatano
19
kwamba: Mungu alikuwa katika Kristo, akawapatanisha wa ulimwengu naye yeye, asiwahesabie maanguko yao; akaweka kwetu wenye kuyatangaza hayo mapatano.
20
Hivyo sisi tu wajumbe mahali pake Kristo; ndivyo Mungu mwenyewe anavyowaonya kwa vinywa vyetu sisi. Maana twawabembeleza mahali pa Kristo: Yapokeeni hayo mapatano yake Mungu!
21
Asiyetambua kosa alimgeuza kuwa mwenye makosa kwa ajili yetu, sisi tugeuzwe naye kuwa wenye wongofu wa Kimungu.*
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13