bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Corinthians 6
2 Corinthians 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 7 →
1
*Nasi tulio wenziwe wa kazi twawaonya, msigawiwe bure kipaji cha Mungu.
2
Kwani anasema: Nimekuitikia, siku zilipokuwa za kupendezwa, nikakusaidia siku ya wokovu. Tazameni, siku za kupendezwa kweli ndizo za sasa hivi! Tazameni, leo ni siku ile ya wokovu!
3
Hakuna hata mmoja, tumkwazaye kwa jambo lo lote, utumishi wetu usibezwe.
4
Ila po pote twajitokeza kwamba: Sisi humtumikia Mungu, kwa hivyo twavumilia mengi; maumivu, mahangaiko, masongano,
5
mapigo, mafungo, mashambulio, masumbuko, kukesha na kufunga.
6
Twataka kujijulisha kuwa wenye utakato, utambuzi, uvumilivu, utu, Roho takatifu, upendo usiojua ujanja,
7
neno la kweli, nayo nguvu ya Mungu. Mata yanayotupa kushinda kuumeni na kushotoni ndiyo ya wongofu,
8
ikiwa twatukuzwa, au ikiwa twabezwa; ikiwa twasingiziwa, au ikiwa twashangiliwa. Tuko kama wapotezaji, lakini tu wa kweli;
9
tuko kama wasiojulika, lakini tumetambulikana; tuko kama wenye kufa, lakini tazameni, tu wenye kuishi! Tuko kama wenye kupondwa, lakini hatuuawi;
10
tuko kama wenye kusikitika, lakini twafurahi po pote; tuko kama maskini, lakini twagawia wengi mali nyingi; tuko kama wasio na kitu cho chote, lakini vyote tunavyo.*
11
Enyi Wakorinto, tumewafumbulia vinywa vyetu, tena mioyo yetu nayo imewafungukia kabisa.
12
Humu ndani yetu penu sipo padogo, lakini mioyoni mwenu mnasongeka.
13
Nasema nanyi kama na watoto wangu, nikiwaambia: Tulipeni vivyo hivyo, mkitupatia nasi pakubwa mioyoni mwenu!
14
*Msiingie utumwa wa mwingine pamoja nao wasiomtegemea Mungu! Je? Yako magawio wongufu na upotovu unayoyagawiana? Au iko bia ya mwanga na ya giza?
15
Yako mapatano ya Kristo na ya Beliali? Au liko fungu lililo lake amtegemeaye Mungu nalo lake asiyemtegemea Mungu?
16
Au iko nyumba yake Mungu inayofanana napo penye mizimu? Kwani sisi tu nyumba yake Mungu aliye Mwenye uzima; kama Mungu alivyosema: Nitakaa katikati yao, tena nitatembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa ukoo wangu.
17
Kwa hiyo Bwana anasema: Tokeni kati yao, mjitenge, msiguse yenye uchafu, nami nipate kuwapokea!
18
Ndipo, nitakapokuwa Baba yenu, nanyi mtakuwa wanangu wa kiume na wa kike. Hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mwenyezi.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13