bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Corinthians 7
2 Corinthians 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 8 →
1
Basi, wenzangu, kwa sababu tumepewa viagio kama hivyo, na tujitakase na kuondoa madoa yote ya miili na ya roho! Hivyo tutautimiza utakatifu, maana tutamwogopa Mungu.*
2
Tupatieni kao mioyoni mwenu! Hakuna tuliyempotoa, hakuna tuliyemponza, hakuna tuliyemdanganya.
3
Siyasemei kwamba: Niwapatilize. Kwani nimesema kwanza, ya kuwa mmo mioyoni mwetu, tufe pamoja, kisha tupate kuishi pamoja.
4
*Nikisema nanyi nasema waziwazi kabisa, tena yako mengi yenu, ninayojivunia. Moyo wangu umetulia wote, ukafuliza kuchangamka, hata tukipatwa na maumivu mengi.
5
Kwani tulipofika Makedonia, miili yetu haikuweza kupumzikia kwa ajili ya maumivu yaliyotupata po pote, nje yalikuwako magombano, ndani mahangaiko.
6
Lakini Mungu anayewatuliza wanyenyekevu mioyoni mwao, alitutuliza sisi kwa kuja kwake Tito.
7
Lakini kulikotutuliza siko kuja kwake tu, ila nao utulivu, mwenyewe aliotulizwa nao alipowaona, mlivyo. Naye akatusimulia, mnavyotunukia kutuona, mnavyosikitika, mnavyofanya bidii kwa ajili yangu mimi. Hivi vikanifurahisha kuliko vingine.
8
Nami ikiwa nimewasikitisha na barua yangu sijuti sasa. Na kama nalijuta hapo, nilipoona, ya kuwa ile barua imewasikitisha kitambo,
9
sasa nafurahi, si kwa sababu mmesikitishwa, ila kwa sababu masikitiko, mliyoyapata, yamewafundisha majuto. Kwani mmesikitishwa Kimungu, maana msiponzwe na jambo lo lote litokalo kwetu.
10
Kwani sikitiko la Kimungu humpeleka mtu penye wokovu, likimpatia majuto yasiyojutika tena. Lakini sikitiko la kiulimwengu humpeleka mtu penye kufa.*
11
Kwani tazameni, kule kusikitishwa Kimungu kuko huko ndiko kulikowahimiza hivyo, mjikanie kwa kuona machukivu na woga, mkatunukia kulilipiza lile neno upesi. Mlipoyafanya hayo yote mmejitokeza wenyewe, ya kuwa hammo katika jambo lile.
12
Nami hapo, nilipowaandikia, sikuandika kwa ajili yake aliyepotoa, wala kwa ajili yake aliyepotolewa, ila naliandikia kwamba: Kwenu kuonekane, ninyi mnavyojihimiza kwa ajili yetu mbele ya Mungu.
13
Kwa hiyo tumetulizwa mioyo; na kwa hivyo, mioyo yetu ilivyotulia, furaha yetu ikaongezwa na furaha, Tito aliyokuwa nayo, kwani roho yake imepozwa kwenu po pote.
14
Kama liko jambo la kwenu, nililojivunia kwake, halikunitokeza kuwa mwongo; lakini kama tulivyowaambia nanyi yote yaliyo ya kweli, vivyo hivyo hata yale, tuliyojivunia kwake Tito, yaliyokuwa ya kweli.
15
Ndipo, moyo wake ulipowageukia, ukafuliza kuwapenda, akiwakumbuka, ninyi nyote mlivyomtii, mlivyompokea, woga ukiwatetemesha.
16
Nafurahi, ya kuwa ninaweza kuwatazamia ninyi katika mambo yo yote.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13