bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Corinthians 8
2 Corinthians 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 9 →
1
Ndugu, twawatambulisha kipaji cha Mungu, wateule wa Makedonia walichogawiwa:
2
maana walipojaribiwa na maumivu yao mengi wameshinda, wakachangamka sana; kwa hiyo hao walio wenye umaskini usiopimika wakajikaza kuonyesha wingi wa mali zilizomo katika mioyo yenye neno moja tu.
3
Kwani nawashuhudia kwamba: Wenyewe walipendezwa na kuchanga, kama walivyoweza, na kupapita hapo, walipoweza.
4
Wakatubembeleza sana na kutuomba, tusiwakataze kulitoa fungu lao la kuingia katika bia hiyo ya kuwatumikia watakatifu.
5
Tena hawakutoa, kama tulivyowangojea, ila kwanza walijitoa wenyewe kumtumikia Bwana na sisi; hivyo wameyamaliza, Mungu ayatakayo.
6
Kwa hiyo tulimhimiza Tito, aitimize hata kwenu kazi hiyo ya vipaji, kama alivyoianza kwanza.
7
Lakini kama mwapitavyo wengine katika mambo yo yote, ikiwa kumtegemea Mungu au kupiga mbiu au kutaka utambuzi au kujihimiza kufanya mema yo yote au kutupenda kwa moyo, kama tunavyowapenda ninyi, hivyo sharti mwapite hata katika vipaji hivi.
8
Sisemi, kwamba niwatolee nguvu, lakini kwa hivyo, wengine walivyojihimiza, nataka, upendo wenu nao utambulike, ya kama ni wa kweli.
9
Kwani mmekitambua kipaji, tulichopewa na Bwana wetu Yesu Kristo: Huyu alikuwa mwenye mali nyingi, akawa maskini kwa ajili yenu, kwamba umaskini wake yeye uwapatie ninyi mali nyingi.
10
Nami niliyoyatambua humu, ndiyo, ninayowatolea, kwani yanawafalia ninyi: mwaka wa jana mlitangulia kuifanya kazi hiyo; tena siko kuifanya tu, mlianza hata kuiitikia.
11
Lakini sasa sharti mmalize kuifanya, maana kama mapenzi yenu ya kuiitikia yalivyotokea upesi, vivyo hivyo mtokeze nayo mapenzi ya kuifanya mkichanga kwa vile, mlivyo navyo.
12
Kwani kama yako mapenzi, mtu hupendezeka akivitoa, alivyo navyo, asivitoe, asivyo navyo.
13
Kwani hatuchangii kwamba: Wengine wapate kutulia, ninyi mkiumizwa, ila sharti yalinganike:
14
mapato mengi yenu yao wale sharti yapunguze makosekano yenu ya siku nyingine; hivyo yatalinganika,
15
kama ilivyoandikwa kwamba: Aliyeokota nyingi hakufurikiwa; wala aliyeokota chache hakupungukiwa.
16
Lakini na tumshukuru Mungu aliyempa Tito kujihimiza vivyo hivyo moyoni mwake kwa ajili yenu.
17
Kwani tulipombembeleza, akaitikia. Lakini kwa hivyo, alivyokaza kujihimiza, aliondoka kwenda kwenu kwa mapenzi yake mwenyewe.
18
Tukatuma pamoja naye ndugu mmoja anayesifiwa kwenye wateule wote hivyo, anavyoutangaza Utume mwema.
19
Lakini sivyo hivyo tu, ila hata kuchaguliwa amechaguliwa nao wateule kuwa mfuasi wetu wa kutusaidia katika kazi hii ya vipaji, tutumikiayo sisi, tumtukuze Bwana, tukijulikana kuwa wenye kumpendeza.
20
Hivyo twajikinga, mtu asitusengenye kwa ajili ya machango haya makubwa yatumikiwayo nasi.
21
Kwani twajilindia, yaendelee vizuri, sipo mbele ya Bwana tu, ila napo mbele ya watu.
22
Tena pamoja nao tulituma ndugu yetu, tuliyemwona mara nyingi katika mambo mengi, anavyojihimiza. Lakini sasa anakaza kujihimiza, kwa sababu yako mengi, anayoyatazamia kwenu.
23
Basi, Tito mwamjua kuwa mwenzangu anayenisaidia kazi za kwenu; nao hao ndugu zetu ni mitume wa wateule, maana wampatia Kristo utukufu.
24
Basi, hao waonyesheni upendo wenu, tuliojivunia tulipowatukuza ninyi! Uonyesheni mbele yao wateule!
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13