bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Corinthians 9
2 Corinthians 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 10 →
1
Kwa ajili ya hayo matumikio yanayochangiwa watakatifu hainipasi kuwaandikia ninyi.
2
Kwani najua, yalivyowapendeza; nami ninajivunia kwa ajili yenu kwa wamakedonia kwamba: Waakea wamejitengeneza tangu mwaka wa jana. Nako kujihimiza kwenu kumehimiza wengine wengi.
3
Lakini nimewatuma hao ndugu, maana hivyo, tulivyojivuna kwa ajili yenu, visipungukiwe katika jambo hili, ila mjulikane, ya kuwa mmejitengeneza, kama nilivyosema.
4
Maana kama Wamakedonia wanakuja pamoja nami, wakawaona ninyi, hamkujitengeneza, tutakuwa waongo sisi, nisiseme: Ninyi, kwa ajili ya hayo majivuno yetu.
5
Kwa hiyo nalijishurutisha kuwaonya ndugu waliotangulia kufika kwenu, waanze kuvichanga vipaji vya upendo wenu, mlivyotuagia kale, tuvikute, vimekwisha kuchangwa kuwa vipaji vya upendo wa kweli, sivyo vya choyo.
6
*Twajua hayo: Mwenye kupanda kwa choyo huvuna yenye choyo; naye mwenye kupanda kwa kubariki huvuna yenye mbaraka.
7
Kila mtu atoe, kama alivyoanza kupima moyoni, asitoe akiwa na mafundo au akishurutishwa! Kwani Mungu humpenda mwenye kutoa na kushangilia.
8
Naye Mungu anaweza kuwapatia matunzo yote, kwamba hayo, mpaswayo nayo, siku zote yawatoshee kabisa, tena yasalie ya kutolea kazi njema zote,
9
kama ilivyoandikwa: Alizimwaga, akawagawia wao waliozikosa; huu wongofu wake hukaa kale na kale.
10
Lakini yeye anayemtolea mpanzi mbegu hutoa nao mkate wa kula; yeye ataziongeza nazo mbegu zenu, ziwe nyingi, kisha atayachipuza mazao ya wongofu wenu.
11
Hivyo mtakuwa wenye mali katika mambo yote, mpate mioyo yenye neno moja tu; hii ndiyo inayomfanyia Mungu kazi na kutupa mikononi vipaji vya kumtukuza.*
12
Kwani kazi hii ya kuchanga vipaji, tunayoitumikia, siyo ya kuyaondoa tu mapungufu ya watakatifu, ila kupita hapo inatimilika kwao wengi, wakimtolea Mungu vipaji vya kumshukuru.
13
Kazi hii, tunayoitumikia, ikijulikana kuwa ya upendo wa kweli, watamtukuza Mungu, maana mmeyatii hayo, mnayoyaungama kuwa Utume mwema wa Kristo, nayo mioyo yenu ikajulika kwao kuwa yenye neno moja tu kwa hivyo, mlivyowagawia hao nao wengine wote.
14
Kwa ajili hii watawaombea ninyi wakitunukia kuwaona, kwa sababu Mungu aliwapa makuu kuliko wengine.
15
Na tumshukuru Mungu, kwani ametupa kipaji kisichowezekana kusimuliwa chote!
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13