bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 16
2 Kings 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 17 →
1
Katika mwaka wa 17 wa Peka, mwana wa Remalia, Ahazi, mwana wa Yotamu, mfalme wa Wayuda, akapata kuwa mfalme.
2
Ahazi alikuwa mwenye miaka 20 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 16. Hakuyafanya yanyokayo machoni pake Bwana kama baba yake Dawidi,
3
ila akaendelea kuzishika njia za wafalme wa Waisiraeli, hata mwanawe akamtumia kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa motoni akiyafuata hayo matapisho ya wamizimu, Bwana aliowafukuza mbele yao Waisiraeli.
4
Akatambika na kuvukiza vilimani pa kutambikia napo pengine palipoinukia juu, hata chini yake kila mti uliokuwa wenye majani mengi.
5
Hapo Resini, mfalme wa Ushami, na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Waisiraeli, wakaupandia Yerusalemu kupiga vita, wakamsonga Ahazi kwa kumzinga, lakini hawakuweza kumshinda vitani.
6
Wakati huo Resini, mfalme wa Ushami, akaurudisha mji wa Elati kwa Washami, nao Wayuda akawafukuza mle Elati; ndipo, washami wlipokuja kukaa Elati, wakakaa humo mpaka siku hii ya leo.
7
Ahazi akatuma wajumbe kwa Tiglati-Pileseri, mfalme wa Asuri, kumwambia: Mimi ni mtumwa wako na mtoto wako; panda, uniokoe mkononi mwa mfalme wa Ushami namo mkononi mwa mfalme wa Waisiraeli walioniinukia!
8
Ahazi akazichukua fedha na dhahabu zilizopatikana Nyumbani mwa Bwana namo katika vilimbiko vya nyumbani mwa mfalme, akazituma kwa mfalme wa Asuri kuwa matunzo.
9
Mfalme wa Asuri akamwitikia; kisha mfalme wa Asuri akaupandia mji wa Damasko, akauteka, nao watu akawahamisha kwenda Kiri, lakini Resini akamwua.
10
Mfalme Ahazi akaenda Damasko kuonana na Tiglati-Pileseri, mfalme wa Asuri. Alipoiona meza ya kutambikia iliyoko Damasko mfalme Ahazi akatuma mfano wa hiyo meza ya kutambikia kuionyesha namna yake, ilivyotengenezwa kazi zake zote, akaupeleka kwa mtambikaji Uria.
11
Ndipo, mtambikaji Uria alipojenga kutambikia, pote pawe sawa na ule mfano, mfalme Ahazi alioutuma toka Damasko; ndivyo, mtambikaji Uria alivyovifanya, mfalme Ahazi alipokuwa hajarudi bado toka Damasko.
12
Mfalme aliporudi toka Damasko, mfalme akaiona hiyo meza ya kutambikia; ndipo, mfalme alipoikaribia hiyo meza ya kutambikia, akateketeza juu yake ng'ombe ya tambiko
13
pamoja na kuivukizia na kutoa vilaji vya tambiko, akaimwagia vinywaji vya tambiko nazo damu za ng'ombe za tambiko za shukrani, alizozitoa kuzinyunyizia ile meza ya kutambikia.
14
Nayo ile meza ya shaba ya kutambikia iliyokuwako mbele ya Bwana akaiondoa mahali pake mbele ya Nyumba, isiwe tena katikati ya hiyo meza mpya ya kutambikia na Nyumba ya Bwana, akaiweka upande wa kaskazini wa hiyo meza mpya ya kutambikia.
15
Kisha mfalme Ahazi akamwagiza mtambikaji Uria kwamba: Katika hii meza kubwa utachoma ng'ombe za tambiko za asubuhi na vilaji vya tambiko vya jioni na ng'ombe za tambiko za mfalme na vilaji vyake vya tambiko na ng'ombe za tambiko za watu wote wa nchi hii na vilaji vyao vya tambiko na vinywaji vyao vya tambiko, nazo damu zote za ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima nazo damu za ng'ombe nyingine za tambiko uinyunyizie. Nayo mambo ya ile meza ya shaba ya kutambikia nitayafikiri, yatakavyokuwa.
16
Mtambikaji Uria akayafanya yote, kama mfalme Ahazi alivyomwagiza.
17
Mfalme Ahazi akavivunja navyo vibao vya kufungia vya vile vilingo, akaiondoa nayo ile mitungi ya shaba iliyowekwa humo, nayo bahari ya shaba akaiondoa juu ya zile ng'ombe za shaba zilizokuwa chini yake, akaiweka juu ya mawe yaliyopangwa.
18
Nao ukumbi wa siku ya mapumziko, walioujenga penye Nyumba hiyo, nao mlango wa nje wa kuingilia mfalme akauondoa na kuuweka pengine penye Nyumba hiyo kwa ajili ya mfalme wa Asuri.
19
Mambo mengine ya Ahazi, aliyoyafanya, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
20
Ahazi alipokwenda kulala na baba zake, akazikwa kwa baba zake mjini mwa Dawidi, naye mwanawe Hizikia akawa mfalme mahali pake.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25