bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 17
2 Kings 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 18 →
1
Katika mwaka wa 12 wa Ahazi, mfalme wa Wayuda, Hosea, mwana wa Ela, akapata kuwa mfalme wa Waisiraeli mle Samaria miaka 9.
2
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, lakini hakuzidi kama wafalme waliokuwa mbele yake.
3
Yeye ndiye, Salmaneseri, mfalme wa Asuri, aliyemjia, naye Hosea, hakuwa na budi kumtumikia na kumtolea mahongo.
4
Kisha mfalme wa Asuri akamwona Hosea kuwa mwenye njama mbaya, kwa kuwa alituma wajumbe kwa So, mfalme wa Misri, akaacha kumpelekea mfalme wa Asuri mahongo, aliyoyapeleka mwaka kwa mwaka; ndipo, mfalme wa Asuri alipomfunga na kumtia kifungoni.
5
Kisha mfalme wa Asuri akaipandia hiyo nchi yote akiupandia mji wa Samaria, akausonga kwa kuuzinga miaka mitatu.
6
Katika mwaka wa tisa wa Hosea mfalme wa Asuri akauteka mji wa Samaria, akawahamisha Waisiraeli kwenda Asuri, akawakalisha katika miji ya Hala, tena Habori penye mto wa Gozani na katika miji ya Wamedi.
7
Ikawa hivyo, kwa kuwa wana wa Isiraeli walimkosea Bwana Mungu wao aliyewatoa utumwani katika nchi ya Misri mkononi mwa Farao, mfalme wa Misri, lakini wao wakacha miungu mingine.
8
Wakaendelea na kuyafuata maongozi ya wamizimu, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Isiraeli, nayo maongozi, wafalme wa Waisiraeli waliyoyatoa.
9
Hivyo wana wa Isiraeli walimkosea Bwana Mungu wao na kufanya mafichoni mambo yasiyopasa kuyafanya, wakijijengea pa kutambikia vilimani katika miji yao yote iliyokuwa yenye minara tu ya kungojea, namo mijini mlimo na maboma.
10
Wakajisimamishia nguzo za kutambikia na miti ya Ashera katika vilima virefu vyote na chini ya kila mti wenye majani mengi,
11
wakavukiza vilimani po pote pa kutambikia kama wamizimu, Bwana aliowaondoa mbele yao. Kweli walifanya mambo mabaya ya kumkasirisha Bwana,
12
wakiitumikia migogo ya kutambikia, naye Bwana alikuwa amewakataza kwamba: Msilifanye jambo hilo!
13
Tena Bwana aliwashuhudia Waisiraeli na Wayuda vinywani mwa wafumbuaji wote na wachunguzaji wote kwamba: Rudini na kuziacha njia zenu mbaya, myaangalie maagizo yangu na maongozi yangu na kuyafuata Maonyo yote, niliyowaagiza baba zenu, niliyoyatuma kwenu vinywani mwa watumishi wangu waliokuwa wafumbuaji.
14
Lakini hawakusikia, ila walizishupaza kosi zao kuwa kama kosi za baba zao wasiomtegemea Bwana Mungu wao.
15
Wakayakataa maongozi yake na Agano lake, aliloliagana na baba zao, nao ushuhuda wake, aliowashuhudia, wakafuata mambo yasiyo na maana wakifanya yaliyo ya bure kabisa, wakawafuata wamizimu waliokaa na kuwazunguka pande zote, naye Bwana alikuwa amewaagiza, wasifanye kama wao.
16
Wakayaacha maagizo yote ya Bwana Mungu wao, wakajitengenezea vinyago viwili vya ndama kwa shaba zilizoyeyushwa, tena wakajitengenezea vinyago vya Ashera, wakaviangukia navyo vikosi vyote vya mbinguni, wakamtumikia hata Baali.
17
Hata wana wao wa kiume na wa kike wakawatumia kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa motoni, wakaagua maaguaji kwa kutabana, wakajiuza katika utumwa wa kuyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, wamkasirishe.
18
Ndipo, Bwana alipowachafukia sana Waisiraeli, akawaondoa usoni pake, hakusalia mtu, ila shina la Wayuda peke yake.
19
Lakini Wayuda nao hawakuyaangalia maagizo ya Bwana, nao wakaendelea kuyafuata maongozi, Waisiraeli waliyoyatoa.
20
Ndipo, Bwana alipokikataa kizazi chote cha Isiraeli, akawatesa na kuwatia mikononi mwa wanyang'anyi, mpaka akiwatupa, waondoke kabisa usoni pake.
21
Kwani Waisiraeli walipojitenga nao wa mlango wa Dawidi na kumfanya Yeroboamu, mwana wa Nebati, kuwa mfalme wao, Yeroboamu akawahimiza Waisiraeli, wasimfuate Bwana, akawakosesha kosa kubwa mno.
22
Wana wa Isiraeli wakaendelea kuyafanya makosa yote, Yeroboamu aliyoyafanya, hawakuyaepuka,
23
mpaka Bwana akiwaondoa Waisiraeli usoni pake, kama alivyosema vinywani mwa watumishi wake wafumbuaji, akawatoa Waisiraeli katika nchi yao na kuwahamisha kwenda Asuri mpaka siku hii ya leo.
24
Kisha mfalme wa Asuri akatoa watu mle Babeli na Kuta na Awa na Hamati na Sefarwaimu, akawakalisha katika miji ya Samaria mahali pao wana wa Isiraeli, wakaitwaa nchi ya Samaria, iwe yao, wakakaa katika miji yao.
25
Ikawa, walipoanza kukaa huko, hawakumcha Bwana, naye Bwana akatuma simba kwao, wakaua watu wengine wengine.
26
Ndipo, walipotuma kumwambia mfalme wa Asuri kwamba: Wamizimu, uliowahamisha na kuwakalisha katika miji ya Samaria, hawayajui yampasayo Mungu wa nchi hii, kwa sababu hii ametuma simba kwao, nao wakawaua, kwa kuwa hawajui yampasayo Mungu wa nchi hii.
27
Mfalme wa Asuri akaagiza kwamba: Pelekeni huko mmoja wao watambikaji, mliowatoa huko na kuwahamisha! Na aende, akae huko na kuwafundisha yampasayo Mungu wa nchi hiyo.
28
Ndipo, mmoja wao watambikaji, waliowatoa Samaria na kuwahamisha, alipokuja, akakaa Beteli, akawa akiwafundisha njia za kumcha Bwana.
29
Lakini kila kabila moja wakajitengenezea miungu ya kwao, wakaiweka katika zile nyumba, Waisiraeli walizozijenga vilimani za kutambikia mle; kila kabila moja wakafanya hivyo katika miji yao, walimokaa.
30
Watu wa Babeli wakatengeneza vinyago vya Sukoti-Benoti, watu wa Kuta wakatengeneza vinyago vya Nergali, watu wa Hamati wakatengeneza vinyago vya Asima,
31
watu wa Awa wakatengeneza vinyago vya Nibuhazi na vya Tarkati, nao wa Sefarwaimu wakawateketeza wana wao motoni, wawe ng'ombe za tambiko za Adarameleki na za Anameleki, ndiyo miungu yao wa Sefarwaimu.
32
Basi, hivyo walikuwa wakimcha Bwana, lakini wakajipatia miongoni mwao watambikaji wa vilimani, ndio waliowafanyia kazi za kutambika katika nyumba za vilimani.
33
Hivyo walikuwa wenye kumcha Bwana pamoja na kuitumikia miungu ya kwao, kama ilivyowapasa wamizimu wa kwao, walikotolewa na kuhamishwa kuja huku.
34
Hata siku hii ya leo hufanya, kama hizo desturi zao za kwanza zilivyokuwa: hawamchi Bwana kwa kweli, wala hawafanyi kwa kweli, maongozi yao na desturi zao zilivyo, wala hawaishiki njia ya Maonyo na ya maagizo, Bwana aliyowaagiza wana wa Yakobo, aliyempa jina la Isiraeli.
35
Naye Bwana alikuwa amefanya agano nao na kuwaagiza kwamba: Msiche miungu mingine, wala msiiangukie, wala msiitumikie, wala msiitambikie!
36
Ila Bwana aliyewatoa katika nchi ya Misri kwa nguvu kuu za mkono wake, alioukunjua, yeye sharti mmche, mmwangukie na kumtambikia!
37
Nayo maongozi na maamuzi na Maonyo na maagizo, aliyowaandikia ninyi, sharti myaangalie, myafanye siku zote! Msiche kabisa miungu mingine!
38
Wala msilisahau Agano, nililolifanya nanyi, wala msiche miungu mingine!
39
Ila Bwana Mungu wenu sharti mmche! Naye atawaponya mikononi mwa adui zenu wote.
40
Lakini hawakusikia, ila wao wakafanya, kama hizo desturi zao za kwanza zilivyokuwa.
41
Hivyo ndivyo, hao wamizimu walivyomcha Bwana pamoja na kuvitumikia vinyago vyao. Hata wana wao na wana wa wana wao wakayafanya mpaka siku hii ya leo, kama baba zao walivyoyafanya.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25