bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 22
2 Kings 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 23 →
1
Yosia alikuwa mwenye miaka 8 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 31 mle Yerusalemu; jina la mama yake ni Yedida, binti Adaya, wa Boskati.
2
Akayafanya yanyokayo machoni pake Bwana, akaendelea na kuzishika njia zote za baba yake Dawidi, hakuziacha na kujiendea, wala kuumeni, wala kushotoni.
3
Ikawa katika mwaka wa 18 wa ufalme wake Yosia, ndipo, mfalme alipomtuma mwandishi Safani, mwana wa Asalia, mwana wa Mesulamu, kwenda Nyumbani mwa Bwana akimwambia:
4
Nenda kwa mtambikaji mkuu Hilkia, azijumlishe fedha zilizoletwa Nyumbani mwa Bwana, walinzi wa vizingiti wanazozikusanya kwa watu.
5
Kisha wazitie mikononi mwa wenye kazi waliowekwa kuzisimamia kazi za Nyumbani mwa Bwana, nao wawape wazifanyao kazi hizo za Nyumbani mwa Bwana za kupatengeneza, Nyumba ilipobomoka,
6
maseremala na mafundi wengine na waashi, tena wazitumie za kununua miti na mawe ya kuchonga ya kuitengeneza hiyo Nyumba.
7
Lakini wakipewa hizo fedha mikononi mwao, zisihesabiwe nao, kwani walifanya kazi zao kwa welekevu.
8
Ndipo, mtambikaji mkuu Hilkia alipomwambia mwandishi Safani: Nimeona kitabu cha Maonyo Nyumbani mwa Bwana. Kisha Hilkia akampa Safani hicho kitabu, akakisoma.
9
Mwandishi Safani akaja kwa mfalme, akampasha mfalme habari na kumwambia: watumishi wako wamezimimina fedha zilizoonekana Nyumbani mwa Bwana, wakazitia mikononi mwao wenye kazi waliowekwa kuisimamia Nyumba ya Bwana.
10
Kisha mwandishi Safani akamsimulia mfalme kwamba: Mtambikaji Hilkia amenipa kitabu; kisha Safani akakisoma mbele ya mfalme.
11
Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya kitabu cha maonyo, akazirarua nguo zake.
12
Kisha mfalme akamwagiza mtambikaji Hilkia na Ahikamu, mwana wa Safani, na Akibori, mwana wa Mikaya, na mwandishi Safani na Asaya aliyekuwa mtumishi wa mfalme kwamba:
13
Nendeni kuniulizia Bwana mimi na ukoo huu na Wayuda wote kwa ajili ya maneno ya hiki kitabu kilichooneka! Kwani makali ya Bwana yenye moto ni makuu, nayo yanatuwakia sisi, kwa kuwa baba zetu hawakuyasikia maneno ya kitabu hiki na kuyafanya yote, tuliyoandikiwa humo.
14
Ndipo, mtambikaji Hilkia na Ahikamu na Akibori na Safani na Asaya walipokwenda kwa mfumbuaji wa kike Hulda, mkewe Salumu, mwana wa Tikwa, mwana wa Harihasi aliyeyaangalia mavazi; naye alikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili, wakasema naye.
15
Akawaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Mwambieni yule mtu aliyewatuma kwangu:
16
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mtaniona, nikileta mabaya makali hapa, yawapate wenyeji wa hapa, ndiyo yote, kile kitabu kinayoyasema, alichokisoma mfalme wa Wayuda,
17
Kwa kuwa wameniacha, wakavukizia miungu mingine, wanikasirishe kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo makali yangu yenye moto yatapawakia mahali hapa, nayo hayatazimika.
18
Naye mfalme wa Wayuda aliyewatuma kumwuliza Bwana mwambieni haya: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Kwa kuwa hapo, ulipoyasikia maneno yale,
19
moyo wako umelegea, ukajinyenyekeza mbele ya Bwana papo hapo, ulipoyasikia, niliyoyasema ya mahali hapa na ya wenyeji wake kwamba: Patakuwa maangamizo na maapizo, basi, kwa kuwa umeyararua mavazi yako na kunililia mimi, mimi nami nimekusikia; ndivyo, asemavyo Bwana.
20
Kwa sababu hii utaniona, nikikuita, uje kukutana na baba zako; ndipo, utakapopelekwa kulala kaburini mwako na kutengemana, macho yako yasiyaone hayo mabaya yote, mimi nitakayopaletea mahali hapa. Kisha wakampelekea mfalme majibu haya.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25