bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 25
2 Kings 25
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
1
Ikawa katika mwaka wa 9 wa ufalme wake katika mwezi wa kumi siku ya kumi ya mwezi, ndipo, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, alipoujia Yerusalemu yeye na vikosi vyake vyote, wakapiga makambi huko, wakaujengea boma la kuuzungusha.
2
Mji ukaja kusongwa hivyo na kuzingwa mpaka mwaka wa 11 wa mfalme Sedekia.
3
Siku ya tisa ya mwezi wa nne njaa ikazidi mle mjini, watu wa nchi hii hawakuwa na vyakula.
4
Ndipo, mji ulipobomolewa, nao wapiga vita wote wakatoroka usiku huo kwa njia ya lango lililokuwa kati ya kuta mbili penye bustani ya mfalme, nao Wakasidi walikuwa wamelala na kuuzunguka mji, wale wakishika njia ya nyikani.
5
Kisha vikosi vya Wakasidi vikamfuata mfalme na kupiga mbio, vikampata katika nyika ya Yeriko, navyo vikosi vyake vyote vilikuwa vimetawanyika na kumwacha.
6
Wakamkamata mfalme, wakampeleka kwa mfalme wa Babeli huko Ribula, wakasema naye na kumhukumu.
7
Wanawe Sedekia wakawaua machoni pake, kisha wakayapofua macho yake Sedekia, wakamfunga kwa minyororo, wakampeleka Babeli.
8
Katika mwezi wa tano siku ya saba ya mwezi-ulikuwa mwaka wa 19 wa mfalme Nebukadinesari, mfalme wa Babeli-ndipo, Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, mtumishi wa mfalme wa Babeli, alipoingia Yerusalemu.
9
Akaiteketeza Nyumba ya Bwana na nyumba ya mfalme, nazo nyumba zote za Yerusalemu, nazo nyumba kubwa zote akaziteketeza kwa moto.
10
Kisha vikosi vyote vya Wakasidi waliokuwa na mkuu wao waliomlinda mfalme vikazibomoa kuta za boma lililouzunguka Yerusalemu.
11
Masao ya watu waliosalia mjini nao waliokuwa wamemwangukia mfalme wa Babeli na kurudi upande wake, hayo masao yote ya mtutumo wa watu Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, akawateka na kuwahamisha.
12
Lakini wanyonge wa nchi hii mkuu wao waliomlinda mfalme akawasaza, wengine waiangalie mizabibu, wengine walime tu.
13
Lakini zile nguzo mbili za shaba zilizokuwa penye Nyumba ya Bwana na vile vilingo vya kuwekea mitungi ya maji na bahari ya shaba iliyokuwa penye Nyumba ya Bwana Wakasidi wakazivunja, nazo zile shaba zao wakazipeleka Babeli.
14
Hata masufuria na majembe na makato ya kusafishia mishumaa na kata navyo vyombo vyote pia vya shaba vilivyotumiwa Nyumbani mwa Bwana wakavichukua.
15
Nazo sinia na vyano vilivyokuwa vya dhahabu tupu navyo vilivyokuwa vya fedha tupu, mkuu wao waliomlinda mfalme akavichukua.
16
Zile nguzo mbili na ile bahari moja na vile vilingo vya kuwekea mitungi ya maji, ambavyo mfalme Salomo alivitengenezea Nyumba ya Bwana, shaba zao hivi vyombo vyote hazikuwezekana kupimwa kwa mizani.
17
Nguzo moja urefu wake ulikuwa mikono kumi na nane, juu yake palikuwa na kilemba cha shaba, urefu wa kwenda juu wa hicho kilemba ulikuwa mikono mitatu; hicho kilemba kilikuwa kimezungukwa na misuko kama ya mkeka iliyokuwa yenye komamanga, yote pia ni ya shaba; nayo nguzo ya pili ilikuwa vivyo hivyo, nayo ilikuwa yenye misuko kama ya mkeka.
18
Mkuu wao waliomlinda mfalme akamchukua mtambikaji mkuu Seraya na mtambikaji wa pili Sefania nao walinda kizingiti watatu.
19
Namo mjini akachukua mtumishi mmoja wa nyumbani mwa mfalme aliyewekwa kuwa mkuu wa kuwasimamia wapiga vita na watu watano waliokuwa na kazi machoni pa mfalme waliopatikana mjini na mwandishi wa mkuu wa vikosi aliyewaandika watu wa nchi waliotakiwa uaskari na watu sitini wa shambani waliopatikana mle mjini.
20
Hao akawachukua Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, akawapeleka Ribula kwa mfalme wa Babeli.
21
Naye mfalme wa Babeli akawapiga na kuwaua huko Ribula katika nchi ya Hamati. Kisha akwahamisha Wayuda, waitoke nchi yao.
22
Wale watu waliosalia katika nchi ya Yuda, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, aliowasaza, akawawekea Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Safani, kuwasimamia.
23
Wakuu wote wa vikosi, wao na watu wao, waliposikia, ya kuwa mfalme wa Babeli amemweka Gedalia kuwasimamia, wakaja Misipa kwa Gedalia; ndio Isimaeli, mwana wa Netania, na Yohana, mwana wa Karea, na Seraya, mwana wa Tanumeti, wa Netofa, na Yazania, mwana wa mtu wa Maka, hao wenyewe na watu wao.
24
Waume hawa na watu wao Gedalia akawaapia na kuwaambia: Msiwaogope watumishi wa Wakasidi! Kaeni katika nchi hii na kumtumikia mfalme wa Babeli! Ndipo, mtakapoona mema.
25
Ikawa katika mwezi wa saba, ndipo, Isimaeli, mwana wa Netania, mwana wa Elisama wa kizazi cha kifalme, alipokuja pamoja na watu kumi, wakampiga Gedalia, naye kafa; wakawaua hata Wayuda na Wakasidi waliokuwa naye huko Misipa.
26
Kisha watu wote, wadogo kwa wakubwa, na wakuu wa vikosi wakaondoka, wakaja Misri, kwani waliwaogopa Wakasidi.
27
Ikawa katika mwaka wa 37 wa kuhamishwa kwake Yoyakini, mfalme wa Wayuda, katika mwezi wa kumi na mbili siku ya ishirini na saba, ndipo, Ewili-Merodaki, mfalme wa Babeli, alipomwonea uchungu Yoyakini, mfalme wa Wayuda; ikawa katika mwaka huohuo, alipoupata ufalme, akamtoa kifungoni,
28
akasema naye maneno mema, akampa kiti chake cha kifalme juu ya viti vya wafalme wengine waliokuwa naye huko Babeli.
29
Ndipo, alipoyavua mavazi ya kifungoni, akala chakula usoni pa mfalme pasipo kukoma siku zote, alizokuwapo.
30
Nazo mali za kujitunza kila siku akapewa na mfalme wa Babeli, siku kwa siku akapata yaliyompasa siku zote, alizokuwapo.
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25