bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 3
2 Kings 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 4 →
1
Yoramu, mwana wa Ahabu, akapata kuwa mfalme wa Waisiraeli huko Samaria katika mwaka wa 18 wa Yosafati, mfalme wa Wayuda, akawa mfalme miaka 12.
2
Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, lakini hakuzidi kama baba yake na mama yake, akaiondoa nguzo ya mawe ya kumtambikia Baali, baba yake aliyoitengeneza.
3
Lakini makosa ya Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Waisiraeli, aligandamana nayo, hakuyaacha.
4
Mesa, mfalme wa Wamoabu, aliyekuwa mfuga kondoo alikuwa akimletea mfalme wa Waisiraeli wana kondoo 100000 na manyoya ya madume ya kondoo 100000.
5
Lakini Ahabu alipokufa, mfalme wa Wamoabu akamvunjia mfalme wa Waisiraeli hayo maagano.
6
Siku hiyo mfalme Yoramu akatoka Samaria kuwakagua Waisiraeli wote.
7
Kisha akatuma kwa Yosafati, mfalme wa Wayuda, kumwuliza hivyo: Mfalme wa Wamoabu amenivunjia maagano; utakwenda pamoja na mimi vitani kupigana na Wamoabu? Akasema: Nitapanda kwenda huko; mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, nao farasi wangu ni kama farasi wako.
8
Alipouliza: Tupande na kushika njia ipi? akasema: Njia ya nyika ya Edomu.
9
Basi, wakaenda mfalme wa Waisiraeli na mfalme wa Wayuda na mfalme wa Waedomu. Walipokwenda na kuzunguka njia ya siku saba, walikuwa hawana maji ya vikosi vya makambini wala ya nyama waliozifuata nyayo zao.
10
Ndipo, mfalme wa Waisiraeli aliposema: Yoi! Bwana amewaita hawa wafalme watatu, awatie mikononi mwa Wamoabu!
11
Yosafati akauliza: Je? Hakuna mfumbuaji wa Bwana wa kumwuliza Bwana, yatakayokuwa? Ndipo, mmoja wao watumishi wa mfalme wa Waisiraeli akajibu: Yuko Elisa, mwana wa safati, aliyemmiminia Elia maji mikononi pake.
12
Yosafati akasema: Kwake yeye neno la Bwana liko. Ndipo, mfalme wa Waisiraeli na Yosafati na mfalme wa Waedomu waliposhuka kuja kwake.
13
Elisa akamwambia mfalme wa Waisiraeli: Tuna bia gani mimi na wewe? Nenda kwa wafumbuaji wa baba yako na kwa wafumbuaji wa mama yako! Mfalme wa Waisiraeli akamwambia: La! Kweli Bwana amewaita hawa wafalme, awatie mikononi mwa Wamoabu.
14
Elisa akasema: Hivyo, Bwana Mwenye vikosi alivyo Mwenye uzima, ambaye ninasimama mbele yake, kama nisingeutazama uso wa Yosafati, mfalme wa Wayuda, wewe nisingekuelekezea macho, nisikuone!
15
Sasa nileteeni mpiga zeze! Ikawa, huyu mpiga zeze alipolipiga zeze lake, mara mkono wa Bwana ukamjia,
16
akasema: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Chimbeni humu bondeni mashimo po pote!
17
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: hamtaona upepo, wala hamtaona mvua, lakini bonde hili litajazwa maji, mpate kunywa ninyi nao mlio nao na nyama wenu.
18
Nayo haya ni mepesi machoni pake Bwana, maana nao wamoabu atawatia mikononi mwenu.
19
Ninyi mtaiteka miji yote yenye maboma na miji yote iliyochaguliwa. Mtaikata miti mizuri yote, navyo visima vyote vya maji mtavifukia na mashamba mazuri yote mtayaharibu kwa kuyatupia mawe.
20
Ikawa asubuhi, walipotolea vipaji vya tambiko, ndipo, walipoona, maji yakija katika njia ya kutoka Edomu, mara nchi hiyo ikajaa maji.
21
Wamoabu wote waliposikia, ya kuwa hao wafalme wanawapandia kupigana nao, wakakusanywa wote walioweza kujivika mata nao walio wazee, wakajipanga kuusimamia mpaka.
22
Wakaamka na mapema, jua lilipochomoza juu ya yale maji; ndipo, Wamoabu walipoyaona yale maji mbele yao kuwa mekundu kama damu.
23
Wakasema: Ni damu hizo; kumbe hao wafalme wamekosana, wakauana kila mtu na mwenzake. Sasa ninyi Wamoabu, haya! Chukueni nyara!
24
Walipofika kwenye makambi ya Waisiraeli, Waisiraeli wakawaondokea, wakawapiga Wamoabu, nao wakawakimbia, kisha wakaendelea kuingia kwao wakiwapiga Wamoabu.
25
Wakaibomoa miji, tena penye mashamba mazuri wakayatupia kila mtu jiwe lake, hivyo wakayajaza mawe, navyo visima vyote vya maji wakavifukia, hata miti mizuri yote wakaikata, hawakusaza mji, ni boma la mawe la Kiri-Hareseti peke yake tu. Huu nao wapiga makombeo wakauzunguka, waupige.
26
Mfalme wa Wamoabu alipoona, ya kuwa mapigano hayo yatamshinda, asiyaweze, akachukua watu 700, kila mmoja akiuchomoa upanga wake, wajivunjie njia ya kwenda kwa mfalme wa Waedomu, lakini hawakuweza.
27
Ndipo, alipomchukua mwanawe wa kwanza aliyetaka kumpokea ufalme, mwenyewe atakapokufa, akamtumia kuwa ng'ombe ya tambiko, akamteketeza ukutani juu. Ndipo, machafuko makubwa yalipowainukia Waisiraeli, wakaondoka huko, wakarudi kwao katika nchi yao.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25