bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 8
2 Kings 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 9 →
1
Elisa alikuwa amesema na yule mwanamke, aliyemfufulia mwanawe, akamwambia: Ondoka, uende wewe na mlango wako, ukae ugenini kutakakokufalia kukaa ugenini! Kwani Bwana ameita njaa, ije kuiingia hata nchi hii miaka saba.
2
Ndipo, yule mwanamke alipoondoka, akafanya, kama yule mtu wa Mungu alivyomwambia, akaenda yeye na mlango wake, akakaa ugenini katika nchi ya Wafilisti miaka saba.
3
Hiyo miaka saba ilipokwisha pita, yule mwanamke akaondoka tena katika nchi ya Wafilisti, akarudi, akamtokea mfalme kumlilia kwa ajili ya nyumba yake na ya shamba lake.
4
Hapo mfalme alikuwa akisema na Gehazi aliyekuwa naye yule mtu wa Mungu kwamba: Nisimulie matendo makubwa yote, Elisa aliyoyafanya!
5
Naye akawa akimsimulia mfalme, jinsi alivyomrudisha yule mfu uzimani, mara yule mwanamke, aliyemfufulia mwanawe, akawako akimlilia mfalme kwa ajili ya nyumba yake na ya shamba lake. Ndipo, Gehazi alipomwambia: Bwana wangu mfalme, huyu ndiye yule mwanamke, naye huyu ndiye mwanawe, Elisa aliyemfufua.
6
Mfalme alipomwuliza huyu mwanamke, naye akamsimulia yote. Ndipo, mfalme alipompa mtumishi mmoja wa nyumbani, akamwagiza: Mrudishie yote yaliyokuwa yake nayo mapato yote ya shamba yaliyopatikana tangu sike ile, alipoiacha nchi hii, hata sasa.
7
Kisha Elisa akaja Damasko, naye Benihadadi, mfalme wa Ushami, alikuwa mgonjwa, akapashwa habari, ya kuwa yule mtu wa Mungu amefika huko.
8
Ndipo, mfalme alipomwambia Hazaeli: Chukua matunzo mkononi mwako, uende kuonana na yule mtu wa Mungu, umwombe, aniulizie kwa Bwana, kama nitapona ugonjwa huu.
9
Hazaeli akaenda kuonana naye akichukua mkononi mwake matunzo yote yaliyokuwa vitu vizuri vya Damasko, ya kuchukuliwa na ngamia 40. Alipofika akaja kusimama mbele yake, akamwambia: Mwanao Benihadadi, mfalme wa Ushami, amenituma kwako kukuuliza kwamba: Nitapona ugonjwa huu?
10
Elisa akamjibu: Nenda kumwambia: Kupona utapona; lakini Bwana amenionyesha, ya kuwa atakufa.
11
Kisha yule mtu wa Mungu akamng'arizia macho na kulia machozi, hata mwenyewe akiona soni kwa kufanya hivyo.
12
Hazaeli akamwuliza: Mbona bwana wangu analia machozi? Akajibu: Kwani ninajua, ya kama utawafanyizia wana wa Isiraeli mabaya, miji yao yenye maboma utaiteketeza kwa moto, vijana wao wenye nguvu utawaua kwa panga, wachanga wao utawaponda nao wanawake wao wenye mimba utawatumbua.
13
Hazaeli akasema: Mtumwa wako, huyu mbwa, ni mtu gani, aweze kufanya mambo makuu kama hayo? Elisa akasema: Bwana amenionyesha, ya kuwa wewe utakuwa mfalme wa Ushami.
14
Kisha akatoka kwake Elisa, akaja kwa bwana wake, naye akamwuliza: Elisa amekuambia nini? Akajibu: Ameniambia, ya kuwa utapona.
15
Kesho yake akachukua tandiko la kitanda, akalichovya majini, kisha akamfunika uso nalo, hata akafa. Naye Hazaeli akawa mfalme mahali pake.
16
Katika mwaka wa 5 wa Yoramu, mwana wa Ahabu, mfalme wa Waisiraeli, Yosafati alipomaliza kuwa mfalme wa Wayuda, Yoramu, mwana wa Yosafati, akapata kuwa mfalme wa Wayuda.
17
Alikuwa mwenye miaka 32 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 8.
18
Naye akaendelea katika njia za wafalme wa Waisiraeli, kama wale wa mlango wa Ahabu walivyofanya, kwani binti Ahabu alikuwa mkewe, akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana.
19
Lakini Bwana hakutaka kuwaangamiza Wayuda kwa ajili ya mtumishi wake Dawidi, kwa kuwa alimwambia, ya kama atampa yeye na wanawe kuwa taa iwakayo siku zote.
20
Katika hizo siku zake Waedomu wakalivunja agano wakijitoa mikononi mwa Wayuda, wakajiwekea mfalme wa kuwatawala.
21
Ndipo, Yoramu alipoondoka kwenda Sairi akiyachukua magari yote; ikawa, alipoondoka usiku, akawapiga Waedomu waliomzunguka yeye na wakuu wa magari lakini watu walikuwa wameyakimbilia mahema yao.
22
Lakini Waedomu wakalivunja agano tena, wakajitoa mikononi mwa Wayuda mpaka siku hii ya leo. Kisha nao wa Libuna wakalivunja agano siku zilezile.
23
Mambo mengine ya Yoramu nayo yote, aliyoyafanya, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
24
Yoramu akaja kulala na baba zake, akazikwa kwa baba zake mjini mwa Dawidi, naye mwanawe Ahazia akawa mfalme mahali pake.
25
Katika mwaka wa 12 wa Yoramu, mwana wa Ahabu, mfalme wa Waisiraeli, Ahazia, mwana wa Yoramu, akapata kuwa mfalme wa Wayuda.
26
Ahazia alikuwa mwenye miaka 22 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu mwaka mmoja. Jina la mama yake ni Atalia, binti Omuri, mfalme wa Waisiraeli.
27
Naye akaendelea katika njia ya mlango wa Ahabu, akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kama mlango wa Ahabu. Kwani yeye alikuwa mkwe wao wa mlango wa Ahabu.
28
Akaenda pamoja na Yoramu, mwana wa Ahabu, kumpelekea Hazaeli, mfalme wa Ushami, vita huko Ramoti wa Gileadi, lakini Washami wakamwumiza Yoramu.
29
Kwa hiyo mfalme Yoramu akarudi Izireeli, apate watakaomponya vidonda, Washami walivyompiga kule Rama, alipopigana na Hazaeli, mfalme wa Ushami. Ndipo, Ahazia, mwana wa Yoramu, mfalme wa Wayuda, aliposhuka kumtazama Yoramu, mwana wa Ahabu, huko Izireeli, kwani ndiko, alikougulia.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25