bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Kings 9
2 Kings 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 10 →
1
Mfumbuaji Elisa akamwita mmoja wao wanafunzi wa wafumbuaji, akamwambia: Jifunge viuno vyako, kisha kichukue kichupa hiki cha mafuta mkononi mwako, uende Ramoti wa Gileadi!
2
Utakapofika huko, umtazame huko Yehu, mwana wa Yosafati, mwana wa Nimusi, kisha ingia mwake, umwondoe kwenye ndugu zake na kumwingiza katika chumba cha ndani!
3
Kisha kichukue hicho kichupa cha mafuta, uyamimine kichwani pake na kumwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Nimekupaka mafuta, uwe mfalme wa Waisiraeli. Kisha fungua mlango, ukimbie pasipo kukawia!
4
Ndipo, yule kijana aliyekuwa mfumbuaji kijana alipokwenda Ramoti wa Gileadi.
5
Alipofika akawakuta wakuu wa vikosi, wakikaa pamoja, akasema: Niko na neno la kukuambia wewe mkuu. Yehu alipomwuliza: Mkuu gani kwetu sisi sote? akajibu: Wewe mkuu.
6
Ndipo, alipoondoka, akaingia nyumbani; humo akayamimina yale mafuta kichwani pake na kumwambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Nimekupaka mafuta, uwe mfalme wao Waisiraeli walio ukoo wake Bwana.
7
Utawaua walio wa mlango wa bwana wako Ahabu, nipate kuzilipiza damu za wafumbuaji waliokuwa watumishi wangu, nazo damu za watumishi wote wa Bwana nikizitaka mkononi mwa Izebeli.
8
Mlango wote wa Ahabu utaangamia, nitakapowatowesha kwao wa Ahabu wote walio wa kiume, kama watakuwa wamefungwa au kama watakuwa wamefunguliwa kwao Waisiraeli.
9
Nitautoa mlango wa Ahabu, uwe kama mlango wa Yeroboamu, mwana wa Nebati, na kama mlango wa Basa, mwana wa Ahia.
10
Naye Izebeli mbwa watamla shambani kwa Izireeli, pasiwepo atakayemzika. Kisha akafungua mlango, akakimbia.
11
Yehu alipotokea kwao watumishi wa bwana wake, wakamwuliza: Ni habari njema? Mbona huyo mwenye wazimu ameingia mwako? Akawajibu: Mnamjua yule mtu na maneno yake.
12
Wakamwambia: Uwongo huu! Tupashe habari zake! Ndipo, aliposema: Amesema hivi na hivi, akaniambia kwamba: Hivi ndivyo, anavyosema Bwana: Nimekupaka mafuta, uwe mfalme wa Waisiraeli.
13
Ndipo, wote walipozivua nguo zao upesi, wakaziweka miguuni pake juu ya vipago, zivifunike, wakapiga baragumu kwamba: Yehu ni mfalme!
14
Kisha Yehu, mwana wa Yosafati, mwana wa Nimusi, akamlia Yoramu njama. Ni hapo, Yoramu alipokuwa akiulinda mji wa Ramoti wa Gileadi, yeye na Waisiraeli wote, usichukuliwe na Hazaeli, mfalme wa Ushami.
15
Lakini mfalme Yoramu alikuwa amerudi Izireeli, apate watakaomponya vidonda, Washami walivyompiga, alipopigana na Hazaeli, mfalme wa Ushami. Basi, Yehu akawaambia: Kama ndivyo, roho zenu nazo zinavyotaka, asiponyoke mtu wa kutoka humu mjini kwenda Izireeli na kuzipeleka habari hizi.
16
Kisha Yehu akalipanda gari lake kwenda Izireeli, kwani ndiko, Yoramu alikougulia, naye Ahazia, mfalme wa Wayuda, alikuwa ameshuka kumtazama Yoramu.
17
Mlinzi aliyesimama mnarani juu kule Izireeli alipoliona kundi zima la Yehu, likija, akasema: Mimi naona kundi zima la watu! Ndipo, Yoramu alipomwambia: Chukua mpanda farasi, mtume kuwaendea njiani, awaulize: Mwaleta habari njema?
18
Kwa hiyo mpanda farasi akamwendea njiani, akamwambia: Hivi ndivyo, mfalme anavyouliza: Waleta habari njema? Yehu akajibu: Unatuulizaje habari? Zunguka, unifuate! Ndipo, mlinzi alipoleta habari kwamba: Yule mjumbe amefika kwao, lakini hakurudi.
19
Basi, akatuma mpanda farasi wa pili; naye alipofika kwao akasema: Hivi ndivyo, mfalme anavyouliza: Waleta habari njema? Yehu akajibu: Unatuulizaje habari? Zunguka, unifuate!
20
Mlinzi akapasha habari tena kwamba: Amefika kwao, lakini hakurudi. Lakini ile namna ya kuendesha gari ni kama ya Yehu, mwana wa Nimusi, kwani analiendesha gari lake kama mwenye wazimu.
21
Ndipo, Yoramu alipoagiza, wafunge farasi penye magari; walipokwisha kulifungia gari lake farasi, Yoramu, mfalme wa Waisiraeli, akatoka pamoja na Ahazia, mfalme wa Wayuda, kila mmoja katika gari lake, kumwendea Yehu njiani; wakamkuta penye shamba la Naboti wa Izireeli.
22
Yoramu alipomwona Yehu akamwuliza: Waleta habari njema, Yehu? Akajibu: Ni habari gani njema? Ugoni wa mama yako Izebeli na uchawi wake si mwingi?
23
Ndipo, Yoramu alipoligeuza gari kwa mikono yake, akakimbia na kumwambia Ahazia: Tumedanganyika, Ahazia.
24
Yehu akaushika upindi kwa mkono wake, akauvuta kwa nguvu, akampiga Yoramu katikati ya mabega yake, mshale ukatokea moyoni mwake, akaangukia magotini garini mwake.
25
Kisha akamwagiza Bidekari aliyekuwa mkuu wa askari thelathini: Mchukue, umtupe penye shamba la Naboti wa Izireeli! Kumbuka, mimi na wewe tulipomfuata baba yake Ahabu na kupanda farasi sisi wawili, hapo Bwana alilitoa tamko lile la kumtisha kwamba:
26
Ndivyo, asemavyo Bwana: Damu ya Naboti nazo damu za wanawe, nilizoziona jana, nitakulipisha huku kwenye shamba hili; ndivyo, asemavyo Bwana. Sasa mchukue, umtupe katika shamba hilo, kama Bwana alivyosema.
27
Ahazia, mfalme wa Wayuda, alipoviona akakimbia na kuishika njia ya Beti-Hagani (Nyumba ya Bustani), Yehu akamfuata mbiombio, akaagiza: Naye mpigeni katika gari lake! Wakampiga hapo pa kupandia Guri karibu ya Ibileamu; akakimbia hata Megido, ndiko alikokufa.
28
Watumishi wake wakampeleka Yerusalemu katika gari lake, wakamzika katika kaburi lake kwa baba zake mjini mwa Dawidi.
29
Huyu Ahazia alikuwa ameupata ufalme wa Wayuda katika mwaka wa 11 wa Yoramu, mwana wa Ahabu.
30
Kisha Yehu akaja Izireeli. Izebeli alipoyasikia, akatia wanja machoni pake, akakipamba nacho kichwa chake vizuri, kisha akachungulia dirishani.
31
Yehu alipoingia langoni mwa mji, akamwuliza: Zimuri aliyemwua bwana wake hajambo?
32
Ndipo, alipouelekeza uso wake kwenye lile dirisha na kuuliza: Yuko nani aliye upande wangu? Alipowaona watumishi wa nyumbani wawili au watatu, wakimchungulia,
33
akaagiza: Msukumeni! Wakamsukuma na kumbwaga chini, ukuta ukaenea damu yake, nao farasi vilevile, nao wakamkanyaga.
34
Yehu alipokwisha kuingia, akala, akanywa, kisha akaagiza: Haya! Mtazameni yule mwanamke aliyeapizwa, mmzike, kwani ni binti mfalme.
35
Walipokwenda kumzika hawakumwona, ni kichwa tu na miguu na viganja vya mikono.
36
Wakarudi kumpasha hizi habari; ndipo, aliposema: Hivi ndivyo, Bwana alivyosema kinywani mwa Elia wa Tisibe kwamba: Shambani kwa Izireeli mbwa watazila nyama za mwili wake Izebeli.
37
Nao mzoga wake Izebeli utakuwa kama kinyesi cha shambani katika viwanja vya Izireeli, watu wasiweze kusema: Huyu hapa ni Izebeli.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25