bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Deuteronomy 15
Deuteronomy 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 16 →
1
Miaka saba itakapopita, mwachiliane madeni!
2
Nalo jambo hili la kuachaliana madeni liwe hivyo: kila mkopeshaji aliyemkopesha mwenziwe asimwendee kumdai huyo mwenziwe au ndugu yake, kwani maachilio ya Bwana yametangazwa.
3
Asiye wa Kiisiraeli utaweza kumwendea, umtoze, lakini aliye ndugu yako utamwachilia.
4
Kweli kwako asingekuwako mkopaji, kwani Bwana atakubariki sana katika hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa, uichukue, iwe fungu lako mwenyewe,
5
kama wewe ungeisikia tu sauti ya Bwana Mungu wako, uyaangalie na kuyafanya hayo maagizo yote, mimi ninayokuagiza leo.
6
Kwani Bwana Mungu wako atakubariki, kama alivyokuambia. Kwa hiyo utaweza kukopesha mataifa mengi, lakini mwenyewe hutakopa; hivyo utatawala mataifa mengi, lakini wewe hawatakutawala.
7
Itakapokuwa, ndugu yako mmoja aliopo malangoni pako pawapo pote katika nchi yako, Bwana Mungu wako atakayokupa, akose mali, usiushupaze moyo wako, wala usiufunge mkono wako ukimnyima ndugu yako anayetaka kukukopa.
8
Ila umfungulie mkono wako na kumkopesha yatoshayo kuukomesha ukosefu wake, alioukosa.
9
Jiangalie sana, moyoni mwako lisiingie shauri lisilofaa kabisa la kwamba: Mwaka wa saba, ndio mwaka wa kuachilia madeni, uko karibu, ukamtazama ndugu yako anayetaka kukukopa kwa macho yenye ubaya wa kumnyima; hili kosa litakukalia hapo, atakapomlilia Bwana kwa ajili yako.
10
Kwa hiyo sharti ujihimize kumpa, wala moyo wako usiwe mbaya kwa kumpa; kwani kwa jambo kama hili Bwana Mungu wako atakubarikia matendo yako yote na mapato yote ya mikono yako.
11
Kwani wenye kukosa mali hawatakoma katika nchi hii; kwa sababu hii mini ninakuagiza kwamba: Ndugu yako aliye mnyonge na mkosa mali kwako katika nchi yako umfungulie mkono wako kabisa!
12
Ndugu yako mume au mke wa Kiebureo akijiuza kwako, akakutumikia miaka sita, sharti umwache katika mwaka wa saba, atoke kwako kuwa mwungwana tena.
13
Tena ukimwacha, atoke kwako kuwa mwungwana tena, usimwache, ajiendee mikono mitupu!
14
Ila umgawie mali kwenda nazo, ukitoa mbuzi na kondoo na mapato ya purio lako, nayo ya kamulio lako. Kwa hivyo, Bwana Mungu wako alivyokubariki, umgawie naye.
15
Ukumbuke, ya kama ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, naye Bwana Mungu wako akakukomboa. Kwa sababu hii mimi ninakuagiza leo neno hili.
16
Lakini atakapokuambia: Sitaki kutoka kwako, kwani ninakupenda wewe nao waliomo nyumbani mwako, kwa kuwa ninaona mema kwako,
17
basi, uchukue shazia, ulitoboe sikio lake nalo, kisha umpigilie hivyo mlangoni; ndipo, atakapokuwa mtumwa wako kale na kale. Hata kijakazi utamfanyizia vivyo hivyo.
18
Usiyawazie kuwa magumu kumwacha, aondoke kwako kuwa mwungwana tena, kwani atakuwa amekutumikia miaka sita na kufanya kazi za watu wawili wa mshahara, naye Bwana Mungu wako atakubarikia yote, utakayoyafanya.
19
Wana wote wa kwanza watakaozaliwa, wao wa ng'ombe wako na wa mbuzi na wa kondoo wako, kama ni wa kiume, sharti uwatakase kuwa wake Bwana Mungu wako, usimtumie kazini mwana wa kwanza wa ng'ombe wako, wala usimkate manyoya mwana wa kwanza wa kondoo wako.
20
Ila utamla mbele ya Bwana Mungu wako, wewe pamoja nao waliomo nyumbani mwako, mwaka kwa mwaka mahali pale, Bwana atakapopachagua.
21
Lakini akiwa mwenye kilema, kama ni kiwete au kipofu au mwenye kilema kibaya cho chote, usimchinjie Bwana Mungu wako,
22
ila utamla malangoni pako, mwenye uchafu na mwenye kutakata pamoja, kama unavyokula paa au kulungu.
23
Damu yake tu usiile, ila uimwage mchangani kama maji.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34