bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ephesians 2
Ephesians 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 3 →
1
Nanyi mlikuwa mmekufa kwa ajili ya maanguko na makosa yenu,
2
mliyoendelea nayo kale kwa desturi za watu walio wa ulimwengu huu tu; ndivyo, mwenye kuzitawala nguvu za angani atakavyo, ni yule pepo anayetenda nguvu hata sasa mwao waliokataa kutii.
3
Nasi sote kale tulikuwa wenzao tulipoendelea na kuzifuata tamaa za miili yetu na kuyafanya, miili na mioyo yetu iliyoyataka, nasi kwa hivyo, tulivyokuwa hapo, tulikuwa wana waliomkasirisha kama wale wengine.
4
*Lakini Mungu alikuwa ametulimbikia huruma kwa kuwa na upendo mwingi wa kutupenda;
5
kwa sababu hiyo akaturudisha uzimani pamoja na Kristo hapo, tulipokuwa tumekufa kwa ajili ya maanguko; hivyo wokovu wenu ni gawio tu.
6
Alipokwisha kutufufua pamoja naye akatukalisha mbinguni pake Kristo Yesu.
7
Maana siku zitakazokuja anataka kuonyesha, magawio yake yanavyokuwa mengi, yasipimike akituendea kwa utu tu katika Kristo Yesu.
8
Kwani wokovu wenu ni gawio tu, mlilopewa kwa ajili ya kumtegemea, nako hakukutoka mwenu, maana nako ni kipaji chake Mungu,
9
nacho hamkukipata kwa kazi zenu, mtu asipate kujivuna.
10
Kwani sisi tu kazi yake yeye, namo mwake Kristo Yesu ndimo, tulimoumbiwa, tufanye matendo mema, Mungu aliyotutengenezea kale, tuyafuate.*
11
Kwa hiyo yakumbukeni: kale mlikuwa wamizimu kwa hivyo, miili yenu ilivyo; mkaitwa mapumbavu nao wale waliojiita makungwi, kwa sababu walikuwa wametahiriwa na mikono ya watu miilini mwao.
12
Kumbukeni: siku zile mlikuwa hamnaye Kristo, tena mlikuwa mmekatazwa kuwa wenyeji kwao Waisiraeli, mkawa wageni, msiyajue maagano, waliyoagiwa kuyapata. Mlikuwa hamnacho kingojeo, wala hamnaye Mungu huku ulimwenguni.
13
Lakini sasa kwa kuwa wake Kristo Yesu nanyi mliokuwa kale mbali mmeletwa na damu ya Kristo, mfike karibu.
14
Kwani yeye ni utengemano wetu, maana yale makundi mawili aliyageuza kuwa moja, akiuvunja ukingo uliotutenga, tuchukizane.
15
Ilikuwa hapo, alipoyatangua mwilini mwake yale maonyo na maagizo yaliyokuwa ya miiko tu. Akataka kuwaumba hao wote wawili kuwa mtu mmoja mpya aliye wake yeye; kwa hiyo aliwapatanisha,
16
akawa kole yao wote wawili alipomlipa Mungu madeni yao yeye mmoja mwilini mwake, alipowambwa msalabani; huko ndiko, alikoyaua yale machukivu.
17
Kisha akaja kuipiga hiyo mbiu njema ya utengemano kwenu ninyi mliokuwa mbali, nako kwao waliokuwa karibu.
18
Kwani kwake yeye sote wawili tumepata njia ya kumfikia Baba, tukiwa wenye Roho moja.
19
*Kwa hiyo sasa ham wageni tena, wala wenye kukaa kando, ila m wenyeji pamoja nao watakatifu, tena m wa nyumbani mwake Mungu.
20
Mmejengwa juu ya msingi wao mitume na wafumbuaji, ambao Kristo Yesu ni jiwe lake la pembeni.
21
Kwa nguvu yake yeye jengo lote linaunganishwa, lipate kukua, mpaka liwe nyumba takatifu, Bwana alimo.
22
Humu nanyi mnajengwa pamoja na wengine, mwe kao lake Mungu la Kiroho.*
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6