bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ephesians 3
Ephesians 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 4 →
1
Hayo yamenipeleka mimi Paulo kifungoni kuwa mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi wamizimu.
2
Labda mmesikia, Mungu alivyonipa utunzaji wa magawio yake, niwagawie nanyi.
3
Nilifumbuliwa, niyatambue yale yaliyofichwa tangu kale, kama nilivyowaandikia kidogo hapo kwanza.
4
Mkiyasoma mwaweza kuuona ujuzi wangu wa fumbo la Kristo.
5
Siku zilizopita zote wana wa watu hawajatambulishwa fumbo hilo, ambalo mitume na wafumbuaji wake watakatifu walifunuliwa sasa na Roho,
6
hilo la kwamba: Wamizimu nao ndio wenye urithi pamoja nasi, kwamba: Nao wamo pamoja nasi mwilini mwake, kwamba: Nao ni wenye kiagio, tulichopewa katika Kristo Yesu tulipotangaziwa Utume mwema.
7
Ndio, niutumikiao nami kwa hivyo, Mungu alivyonigawia kipaji changu, nilichopewa hapo, niliposhindwa na nguvu zake.
8
Mimi niliye mdogo kuliko watakatifu wote nikapewa gawio hili, niwapigie wamizimu mbiu njema ya mema yote ya Kristo yaliyo mengi, yasiwezekane kupelelezeka yote;
9
kisha niueleze vema utunzaji wa lile fumbo lililokuwa limefichwa tangu zamani zote kwake Mungu aliyeviumba vyote.
10
Maana siku hizi sharti wakubwa na wanguvu wote walioko mbinguni watambulishwe na wateule, ujuzi wake Mungu ulivyo mwingi sana.
11
Mwenyewe aliviweka hivyo kale kabisa moyoni mwake, vitimie katika Kristo Yesu, Bwana wetu;
12
kisha akatuongoza njia ya kumwendea pasipo woga wowote, mpaka tumfikie tukiwa tumejishikizia kwake yeye kwa kumtegemea.
13
Kwa hiyo naomba, msichoke kwa ajili ya maumivu yangu, niliyopatwa nayo kwa ajili yenu, maana yanawapatia utukufu.
14
Kwa sababu hii nampigia Baba na Bwana wetu Yesu Kristo magoti;
15
kwani kila aliye baba, kama yuko mbinguni au yuko nchini, hujiita na jina hili la baba.
16
Nawaombea, kwa wingi wa utukufu wake awape, mtu wenu wa ndani apate nguvu akikuzwa na Roho wake.
17
Tena awape, Kristo akae mioyoni mwenu kwa hivyo, mnavyomtegemea, mpate kushusha mizizi katika upendo, mshikizwe nayo!
18
Kisha awape, mweze kupima pamoja na watakatifu wote, upendo ulivyo mpana na mrefu, tena unavyoingia chini, hata unavyokwenda juu;
19
ndivyo, mtakavyoutambua upendo wake Kristo, ya kuwa unaupita utambuzi wote, mpate kuujaa katika mambo yote, kama Mungu alivyoujaa.
20
Lakini yeye kwa hivyo, nguvu yake inavyokaza mwetu, anaweza kufanya kuyapita yote, tuyaombayo nayo tuyawazayo,
21
yeye atukuzwe kwao wateule walio wake Kristo Yesu siku zote zitakazokuwapo kale na kale pasipo mwisho! Amin.*
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6