bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ephesians 4
Ephesians 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 5 →
1
*Mimi niliyefungwa kwa ajili ya Bwana nawaonya ninyi, mfanye mwenendo unaopatana na wito, mlioitiwa.
2
Mwe wenye unyenyekevu wote na upole na uvumilivu, mvumiliane mkipendana!
3
Kwa hivyo, Roho alivyowageuza kuwa mmoja, mjikaze kujiunga kwa mapatano!
4
Mwili ni mmoja, nayo Roho ni moja, nacho kingojeo cha wito wenu, mlichoitiwa, ni kimoja.
5
Bwana ni mmoja, nalo tegemeo ni moja, nao ubatizo ni mmoja,
6
naye Mungu ni mmoja, ndiye Baba yao wote, ni mwenye kuwatawala wote, ni mwenye kuwaendesha wote, ni mwenye kuwakalia wote.*
7
Lakini sote tumegawiwa kipaji, kila mmoja chake yeye, kama Kristo alivyompimia cha kumpa.
8
Kwa hiyo yamesemwa: Alipopaa juu aliteka mateka, akawapa watu vipaji.
9
Basi, neno hili: “alipaa” ni kwambaje isipokuwa kwamba: Alishuka kwanza kwenda pande za kuzimuni kwa nchi?
10
Aliyeshuka ndiye yule yule aliyepaa kuzipita mbingu zote, apate kuyatimiza yote.
11
*Naye akawapa wengine kuwa mitume, wengine wafumbuaji, wengine wapiga mbiu njema, wengine wachungaji na wafunzi,
12
maana watakatifu watengenezwe, wajue kuzifanya kazi za utumishi; ndizo kazi za kuujenga mwili wake Kristo,
13
mpaka sisi sote tutakapofikia kuwa mmoja wa kumtegemea na wa kumtambua Mwana wa Mungu; huko ndiko kukua kwenyewe na kuutimiza umri unaoweza kuutambua wingi wote wa vipaji vya Kristo.
14
Hivyo hatutakuwa tena wachanga wanaochukuliwa kama mawimbi na kupelekwa huko na huko na mafunzo ya watu yanayogeukageuka kama upepo, maana ni ya uwongo na ya udanganyi wa watu wanaotaka kutupoteza kwa werevu mbaya.
15
Ila tutakuwa wenye kupendana kweli, katika mambo yote tumkalie yeye Kristo aliye kichwa chetu.
16
Naye ndiye mwenye kuunganisha mwili wote, ukishikamizwa na mafundo yote yanayoutia nguvu, kila fundo moja, kama lilivyopimiwa kazi yake; hivyo mwili hukua, ukijengwa kuwa mzuri kwa kupendana.*
17
Neno hili sasa nalisema na kumtaja Bwana, awe shahidi wangu: Msiendelee tena, kama wamizimu nao wanavyoendelea na kufuata mambo wasiyoyajua maana!
18
Mawazo yao yameguiwa na giza, uzima wa Mungu ukawa kitu kigeni kwao kwa ajili ya ujinga, walio nao, na kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao.
19
Hivyo, walivyokufa ganzi la mioyo, wakajitia katika uasherati, wakayafanya machafu yote wakijipatiamo mali.
20
Lakini ninyi hamkufundishwa mambo ya Kristo kuwa hivyo.
21
Kwani mmesikia, mkafundishwa Neno lake kwamba: Iliyo ya kweli imo mwake Yesu.
22
*Kwa hivyo, mlivyoendelea kale, mvueni mtu wa kale aliyejiponza kwa kuzifuata tamaa za udanganyifu!
23
Kisha mawazo ya mioyo yenu yarudishiwe upya wa Kiroho,
24
mmvae mtu mpya aliyeumbwa kuwa wa Kimungu mwenye wongofu na utakatifu wa kweli!
25
Kwa hiyo uvueni uwongo, mwambiane yaliyo ya kweli kila mtu na mwenzake! Kwani tu viungo, kila mmoja kiungo cha mwenzake.
26
Mioyo inapojaa makali, msikose! Jua lisiwachwee, mkingali na makali yenu,
27
wala msimpe Msengenyaji mahali pa kukaa mwenu!
28
Aliyekwiba asiibe tena! Ila sharti ajisumbue na kufanya kazi kwa mikono yake mwenyewe, ajipatie mema, naye aone ya kumgawia mwenye kuyakosa!
29
Maneno yo yote yaliyo maovu yasitoke vinywani mwenu! Ila kama liko neno zuri lifaalo la kujenga palipojenguka lisemeni, liwapendeze wenye kulisikia!
30
Msimsikitishe Roho Mtakatifu wa Mungu! Kwani ndiye, mliyepewa kuwa muhuri yenu ya siku ya ukombozi.
31
Uchungu wo wote na mifundo ya mioyo na makali na mateto na matusi na yaondoke kwenu pamoja na uovu wote!
32
Mwendeane kwa utu na kwa upole, mkiacha kulipishana, kama Mungu naye alivyoacha kuwalipisha ninyi kwa kuwa wake Kristo!*
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6