bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 39
Ezekiel 39
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 38
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 40 →
1
Nawe mwana wa mtu, mfumbulie Gogi yatakayompata na kusema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Utaniona, nikikujia, Gogi uliye mkuu wa Rosi na wa Meseki na wa Tubali!
2
Nitakugeuza na kukushika kwa kamba, nikutoe huko kaskazini mbali na kukupandisha, uende, mpaka nikufikishe kwenye milima ya Isiraeli.
3
Nitakupiga, upindi wako uanguke mkononi mwako mwa kushoto, nayo mishale yako nitaiangusha mkononi mwako mwa kuume.
4
Milimani kwa Waisiraeli utaanguka wewe na vikosi vyako vyote nayo makabila, uliyo nayo; nitakutoa, uliwe nao ngusu na wote wenye mabawa na nyama wa porini.
5
Utaanguka penye mapori, kwani mimi nimeyasema; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
6
Nayo nchi ya Magogi nitaitupia moto nao wakaao salama katika visiwa; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
7
Lakini Jina langu takatifu watalijulisha kwao walio ukoo wangu wa Isiraeli, nami sitanyamaza tena, Jina langu takatifu likipatiwa uchafu; ndipo, wamizimu watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana aliye Mtakatifu kwao Waisiraeli.
8
Ndivyo, asemavyo Bwana: Hayo mtayaona, yakija kutimia siku ileile, niliyoisema.
9
Ndipo, wakaao katika miji ya Waisiraeli watakapotoka, wavitumie vile vyombo vya vita kuwa kuni za kuwasha moto, zile ngao ndogo na kubwa, nazo pindi na mishale, nazo rungu na mikuki, wataitumia kuwa kuni za moto miaka saba.
10
Hawataokota kuni za moto mashambani, wala hawatazikata misituni, kwani vyombo vya vita vitakuwa kuni zao. Hivyo watateka vitu kwao walioviteka vitu vyao na kuwanyang'anya mali zao; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
11
Siku hiyo nitampa Gogi mahali pa kaburi kwao Waisiraeli katika bonde la wapitaji lililoko upande wa maawioni kwa jua kwenye bahari, nayo makaburi hayo yatawakinga wapitaji; ndiko, watakakomzika Gogi nao watu wake waliokuwa wengi, kisha watapaita Bonde la Wingi wa Gogi.
12
Nao wa mlango wa Isiraeli watawazika muda wa miezi saba, kusudi waondoe uchafu katika nchi hiyo.
13
Nao watu wote wa nchi hiyo watakuwa wakizika; hivyo watajipatia jina la kuwasifu siku ile, nitakapojitukuza; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
14
Kisha watachagua watu wa kushika kazi hiyo siku zote, watembee katika nchi, wawazike wapitaji wale waliosazwa juu ya nchi, wauondoe uchafu huo. Ile miezi saba itakapopita, ndipo, watakapochunguza,
15
watembezi wakitembea katika hiyo nchi; napo hapo, watakapoona mifupa ya mtu, watapajenga kando yake kichuguu, mpaka wazishi wamzike katika Bonde la Wingi wa Gogi.
16
Hata mji utakaokuwako utaitwa Hamona (Wingi wa Watu). Hivyo ndivyo, watakavyoundoa huo uchafu wa hiyo nchi.
17
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nawe mwana wa mtu, waambie ndege wote wenye mabawa nao nyama wote wa porini: Kusanyikeni! Njoni mkitoka pande zote, mkutane penye ng'ombe zangu za tambiko, nitakazowachinjia kuwa karamu kubwa ya nyama za tambiko milimani kwa Waisiraeli, mle nyama na kunywa damu!
18
Mtakula nyama za wapiga vita wenye nguvu, mtakunywa damu za wakuu wa nchi, ndio madume ya kondoo na wana kondoo na mbuzi na ng'ombe, wote ni manono ya Basani.
19
Mtakula mafuta, mshibe, mtakunywa damu, mlewe kwa hizo ng'ombe zangu za tambiko, nitakazowachinjia.
20
Mtashiba mezani pangu kwa nyama za farasi nazo zao waliowapanda, kwa nyama za wapiga vita wenye nguvu nazo zao wote waliojiendea tu kupigana; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
21
Ndivyo, nitakavyoutokeza utukufu wangu kwa wamizimu, nao wamizimu wote watayaona mapatilizo yangu, nitakayowapatia, nao mkono wangu, nilioutoa kuwakamata.
22
Ndipo, walio mlango wa Isiraeli watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu wao, tangu siku ile hata siku zitakazokuja.
23
Nao wamizimu watajua, ya kuwa walio mlango wa Isiraeli walihamishwa kwa ajili ya manza, walizokora walipoyavunja maagano yangu; kwa hiyo naliuficha uso wangu, wasiuone, nikawatia mikononi mwao waliowasonga, wao wote wauawe kwa panga.
24
Hivyo, walivyojipatia uchafu kwa mapotovu yao, ndivyo, nilivyowafanyizia nilipouficha uso wangu, wasiuone.
25
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Sasa nitayafungua mafungo yake Yakobo, niwahurumie wote walio mlango wa Isiraeli kwa kutenda wivu kwa ajili ya Jina langu takatifu.
26
Nao watashikwa na soni iwapasayo kwa hivyo, walivyoyavunja maagano yangu yote, watakapokaa salama katika nchi yao, kwani hatakuwako atakayewastusha.
27
Nitakapowarudisha kwao na kuwatoa kwenye makabila mengine na kuwakusanya, wazitoke nchi za adui zao, ndipo, nitakapojitokeza kwao kuwa Mtakatifu machoni pa wamizimu wengi;
28
nao watajua, ya kuwa mimi Bwana Mungu wao kweli naliwahamisha kwenda kwa wamizimu, lakini nitawakusanya tena, warudi katika nchi yao, sitasaza hata mmoja wao huko.
29
Wala sitauficha uso wangu tena, wasiuone, kwani nitawamwagia walio mlango wa Isiraeli Roho yangu; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
← Chapter 38
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 40 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48