bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezra 10
Ezra 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
1
Ezera alipoomba na kuungama hivyo akilia na kujiangusha chini mbele ya Nyumba ya Mungu, ndipo, walipokusanyika kwake Waisiraeli, ukawa mkutano mkubwa mno, waume na wake na wana, nao hao watu wakalia kilio kikubwa.
2
Kisha akasema Sekania, mwana wa Yehieli, wa wana wa Elamu, akamwambia Ezera: Sisi tumemvunjia Mungu maagano kwa kuoa wanawake wageni wa makabila ya nchi hizi; lakini tena kiko kingojeo, Waisiraeli walicho nacho kwa ajili ya jambo hili.
3
Sasa tufanye agano na Mungu wetu, tuwatoe hao wanawake pamoja na wana waliozaliwa nao kwa shauri lako, bwana wangu, na kwa shauri lao wanaoyaogopa maagizo ya Mungu wetu, kisha na yafanywe, kama Maonyo yanavyoyataka.
4
Inuka! Kwani jambo hili linakupasa wewe, sisi nasi tutakuwa upande wako; jipe moyo, uyafanye!
5
Ndipo, Ezera alipoinuka, akawaapisha wakuu wa watambikaji nao wa Walawi na watu wote wa Isiraeli kufanya hivyo, nao wakaapa.
6
Kisha Ezera akaondoka hapo mbele ya Nyumba ya Mungu, akaingia chumbani mwa Yohana, mwana wa Eliasibu; alipofika humo, hakula chakula, wala hakunywa maji, kwani alikuwa amesikitika kwa hilo kosa lao waliorudi kwenye kutekwa, kwani waliyavunja maagano.
7
Kisha wakapiga mbiu katika nchi ya Yuda namo Yerusalemu kwamba: Wote waliorudi kwenye kutekwa wakusanyike Yerusalemu!
8
Kila asiyekuja katika muda wa siku tatu kwa shauri hili lao wakuu na wazee, basi, mali zake zote zitatiwa mwiko wa kuwa mali ya mtu, naye mwenyewe atatengwa katika mkutano wao waliorudi kwenye kutekwa.
9
Ndipo, walipokusanyika Yerusalemu waume wote wa Yuda na wa Benyamini katika muda wa siku tatu, ikawa siku ya ishirini ya mwezi wa tisa. Watu wote wakakaa uwanjani penye Nyumba ya Mungu, wakatetemeka kwa ajili ya jambo hilo, tena kwa kunyewa na mvua nyingi.
10
Hapo mtambikaji Ezera akaondokea, akawaambia: Mmevunja maagano mlipooa wanawake wageni, mkaziongeza manza za Waisiraeli.
11
Sasa mwungamieni Bwana Mungu wa baba zenu! Kisha mfanye yampendezayo, mkijitenga na makabila ya nchi hii, mkijitenga nao wanawake wageni.
12
Mkutano wote pia wakamwitikia na kupaza sauti sana kwamba: kweli inatupasa kuyafanya, uliyoyasema;
13
Lakini watu ni wengi, tena sasa ni masika, watu wasiweze kusimama nje, nayo kazi hii si ya siku moja au mbili, kwani tumezidisha kufanya maovu katika jambo hili.
14
Wakuu wetu na waondokee kuupigia mkutano wote shauri hili, kisha wote waliooa wanawake wageni mijini mwetu na waje siku zitakazowekwa; tena pamoja nao na waje hata wazee na waamuzi wa kila mji, mpaka watakapoyatuliza makali hayo ya Mungu wetu yawakayo moto kwa ajili ya jambo hili, yakatuacha.
15
Waliovibishia hivi walikuwa Yonatani tu, mwana wa Asaheli, na Yahazia, mwana wa Tikwa, naye Mesulamu na Mlawi Sabutai wakawasaidia.
16
Lakini wao wengine waliorudi kwenye kutekwa wakafanya hivyo; wakachaguliwa mtambikaji Ezera na wakuu wa milango ya baba zao, nao wote wakaandikwa majina. Kisha siku ya kwanza ya mwezi wa kumi wakaja kukaa pamoja, walichunguze jambo hili,
17
wakayamaliza mashauri haya ya watu wote waliooa wanawake wageni mpaka siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza.
18
Kwao wana wa watambikaji waliooneka, ya kuwa walioa wanawake wageni, ndio hawa: kwa wana wa Yesua, mwana wa Yosadaki, na kwa ndugu zake: Masea na Eliezeri na Yaribu na Gedalia.
19
Hawa wakaapa na kupeana mikono, ya kuwa watawaondoa wake zao, tena kwa manza zao, walizozikora, wakatoa dume la kondoo kuwa ng'ombe yao ya tambiko ya upozi.
20
Nako kwa wana wa Imeri: Hanani na zebadia.
21
Nako kwa wana wa Harimu: Masea na Elia na Semaya na Yehieli na Uzia.
22
Nako kwa wana wa Pashuri: Eliyoenai, Masea, Isimaeli, Netaneli, Yozabadi na Elasa.
23
Tena kwa Walawi: Yozabadi na Simei na Kelaya aitwaye Kelita, Petaya, Yuda na Eliezeri.
24
Nako kwa waimbaji: Eliasibu; nako kwa walinda malango: Salumu na Telemu na Uri.
25
Nako kwa Waisiraeli wengine: kwa wana wa Parosi: Ramia na Izia na Malkia na Miyamini na Elazari na Malkia na Benaya.
26
Nako kwa wana wa Elamu: Matania, Zakaria na Yehieli na Abudi na Yeremoti na Elia.
27
Nako kwa wana wa Zatu: Eliyoenai, Eliasibu, Matania na Yeremoti na Zabadi na Aziza.
28
Nako kwa wana wa Bebai: Yohana, Hanania, Zabai, Atilai.
29
Nako kwa wana wa Bani: Mesulamu, Maluki na Adaya, Yasubu na Sali, Yeremoti.
30
Nako kwa wana wa Pahati-Moabu: Adina na Kelali, Benaya, Masea, Matania, Besaleli na Binui na Manase.
31
Nako kwa wana wa Harimu: Eliezeri, Isia, Malkia, Semaya, Simeoni,
32
Benyamini, Maluki, Semaria.
33
Kwa wana wa Hasumu: Matinai, Matata, Zabadi, Elifeleti, Yeremai, Manase, Simei.
34
Kwa wana wa Bani: Madai, Amuramu na Ueli,
35
Benaya, Bedia, Keluhi,
36
Wania, Meremoti, Eliasibu,
37
Matania, Matinai na Yasai,
38
na Bani na Binui, Simei,
39
na Selemia na Natani na Adaya,
40
Makinadebai, Sasai, Sarai,
41
Azareli na Selemia, Semaria,
42
Salumu, Amaria, Yosefu.
43
Kwa wana wa Nebo: Yieli, Matitia, Zabadi, Zebina, Yadai na Yoeli na Benaya.
44
Hawa wote walikuwa wamechukua wanawake wageni, namo mwao hao walikuwamo wanawake waliozaa watoto.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10