bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Galatians 2
Galatians 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 3 →
1
Kisha miaka kumi na minne ilipopita, nikapanda tena kwenda Yerusalemu pamoja na Barnaba, nikamchukua naye Tito, aende pamoja nami.
2
Lakini nalipanda kwa kutumwa na ufunuo, nilioupata. Nikawaelezea Utume mwema, ninaowapigia wamizimu. Kupita wengine naliwaelezea wale waliowaziwa kuwa wenye cheo, wavione hivyo, ninavyovikimbilia sasa, navyo nilivyovikimbilia mbele, kama ni vya bure.
3
Lakini hata Tito aliyekuwa pamoja nami hakushurutishwa kutahiriwa, angawa ni Mgriki.
4
Lakini kulikuwako ndugu wa uwongo waliokuwa wamejiingiza na kufichaficha; hao waliingia tu, watupeleleze, tunavyomkalia Yesu Kristo pasipo mwiko wo wote, waturudishe katika utumwa wa miiko.
5
Nasi hatukushindika, tuwatii hao, hata saa moja tu, kwamba huo Utume mwema ufulize kujulikana kuwa wa kweli.
6
Lakini waliowaziwa kuwa wenye cheo hivyo, walivyo kale, si kitu kwangu, maana Mungu hatazami uso wa mtu. Nasema: Nao hao walioambiwa kuwa wenye cheo hawakuniongezea jambo;
7
lakini wakaona kweli, ya kuwa mimi nimepewa kuutangaza Utume mwema kwao wasiotahiriwa, kama Petero alivyopewa kuutangaza kwao waliotahiriwa.
8
Kwani aliyempa Petero nguvu ya kuwa mtume wao waliotahiriwa ndiye aliyenipa nami nguvu ya kuwa mtume wao wamizimu.
9
Walipokitambua kipaji, nilichogawiwa, ndipo, Yakobo na Kefa na Yohana wanaowaziwa kuwa nguzo walipotupa mimi na Barnaba mikono kwamba: Tu mmoja, sisi tuipige hiyo mbiu kwao wamizimu, lakini wao kwao waliotahiriwa.
10
Walitutakia hilo moja tu, tuwakumbuke maskini wao; nami nimejipingia kulitimiza hili.
11
Lakini Kefa alipofika Antiokia, nikambishia usoni pake, kwani alichongewa.
12
Maana kulikuwako waliotumwa na Yakobo; hao walipokuwa hawajaja bado, alikula pamoja na wamizimu. Lakini walipokuja, akatoweka na kujitenga, kwani aliwaogopa wale waliotahiriwa.
13
Nao wenzake wa Kiyuda waliokuwako wakaufuata huo ujanja wake, naye Barnaba akaponzwa na huo ujanja wao.
14
Lakini nilipowaona, ya kuwa hawaishiki njia nyofu wakiifuata kweli ya Utume mwema, nikamwambia Kefa mbele yao wote: Wewe u Myuda; tena mwenendo wako ni wa kimizimu, sio wa Kiyuda; imekuwaje, wewe ukiwashurutisha wamizimu kufanya mwenendo wa Kiyuda?
15
Sisi tumezaliwa kuwa Wayuda, hatu wakosaji waliotoka kwao wamizimu.
16
Lakini twajua: mtu hapati wongofu akiyafanya Maonyo, ila hupata wongofu akimtegemea Kristo Yesu; nasi tukamtegemea Kristo Yesu, tupate wongofu kwa kumtegemea Kristo, siko kwa kuyafanya Maonyo. Kwani hakuna aliye wa kimtu atakayepata wongofu kwa kuyafanya Maonyo.
17
Lakini sisi tunaotaka kupata wongofu kwa kuwa wake Kristo, sasa wenyewe tukionekana kuwa wakosaji, je? Kristo naye siye mwenye kutumikia makosa? La, sivyo!
18
Kwani nikiyajenga tena yale, niliyoyajengua, naonyesha, ya kama sipatani na mimi mwenyewe.
19
Kwani hapo, niliposhindwa na Maonyo, ndipo, nilipoyafika Maonyo, nipate kumkalia Mungu, maana nimewambwa msalabani pamoja na Kristo.
20
Tena ninaishi, lakini sasa si mimi tena ninayeishi, ila Kristo ndiye anayeishi mwilini mwangu. Maana hivyo, ninavyoishi sasa mwilini, ninaishi kwa kumtegemea Mwana wake Mungu aliyenipenda, akajitoa kwa ajili yangu.
21
Gawio la Mungu silitangui. Kwani kama wongofu ungepatikana kwa kuyafanya Maonyo, basi, Kristo angekuwa amekufa bure.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6