bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Galatians 3
Galatians 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 4 →
1
Enyi Wagalatia, hamna akili? Ni uganga gani uliowashinda, msiyatii yaliyo ya kweli? Mmeonyeshwa Yesu Kristo, mmtazame kwa mambo yenu, alivyowambwa msalabani.
2
Neno hili tu nataka kuambiwa nanyi: Mmempokea Roho kwa kuyafanya Maonyo au kwa kuyategemea, mliyoyasikia?
3
Imekuwaje, akili zikiwapotea hivyo? Mliyoyaanza Rohoni, mwataka kuyamaliza sasa miilini?
4
Yale yote mmeteswa bure? Kweli siyo ya bure!
5
Ilikuwaje? Aliyewapa Roho na kufanya yenye nguvu kwenu aliyafanyia kwamba: Mmeyafanya Maonyo? au kwamba: Mmeyategemea, mliyoyasikia?
6
Ndivyo, yalivyokuwa nayo ya Aburahamu: Akamtegemea Mungu, kwa hiyo akawaziwa kuwa mwenye wongofu.
7
Kwa hiyo yatambueni: wenye kumtegemea Mungu hao ndio wana wa Aburahamu!
8
Lakini Maandiko yaliona kale, ya kuwa Mungu huwapatia wamizimu wongofu, wakiwa wanamtegemea. Kwa hiyo alimpigia Aburahamu kale mbiu ile njema: Mwako ndimo, mataifa yote yatakamobarikiwa.
9
Kwa hiyo wenye kumtegemea Mungu hubarikiwa pamoja na Aburahamu aliyekuwa mtegemevu.
10
Kwani wote walio wenye kuyafanya Maonyo hawajatoka bado kwenye kuapizwa. Kwani imeandikwa: Na awe ameapizwa kila mtu asiyeandamana nayo yote yaliyoandikwa katika chuo cha Maonyo, ayafanye!
11
Lakini neno hili ni waziwazi, ya kuwa hakuna mtu atakayepata wongofu kwake Mungu, kwa kuyafanya Maonyo, kwani: Mwongofu atapata uzima kwa kumtegemea Mungu.
12
Lakini Maonyo hayakutoka kwenye kumtegemea Mungu, ila: Atakayeyafanya atapata uzima kwa njia hiyo.
13
Kristo alitukomboa, tusiapizwe na Maonyo, alipoapizwa kwa ajili yetu, kwani imeandikwa: Kila aliyetundikwa mtini ameapizwa.
14
Hivyo mbaraka yake Aburahamu imewafikia wamizimu hapo, Yesu Kristo alipotokea, nasi tukipokee kiagio cha Roho tukiwa twamtegemea.
15
Ndugu, niseme kimtu: Agano la mtu aliyekufa hakuna alitanguaye, likiisha kusimikwa, wala aliongezaye neno.
16
Lakini Aburahamu alikuwa amepewa viagio vile yeye nao uzao wake. Hasemi: Wazao, kama ni wengi, ila kama ni mmoja, asema: Nao uzao wako, nao huo ndiye Kristo.
17
Kwa hiyo nasema: Agano limetangulia kusimikwa na Mungu, Maonyo yakatokea nyuma, miaka 430 ilipopita; hayawezi kulitangua agano, wala hayawezi kukikomesha nacho kiagio.
18
Kwani huo urithi kama ungalipatikana kwa kuyafanya Maonyo usingepatikana tena kwa kupewa kiagio. Lakini Mungu alimgawia Aburahamu huohuo alipompa kiagio.
19
Basi, Maonyo yako na maana gani? Yalitolewa siku za kati kwa ajili ya mapitano, mpaka atakapokuja yule mzao aliye mwenye kiagio. Nayo Maonyo hapo, yalipotolewa, yalitumikiwa na malaika, yakawekwa mkononi mwa mpatanishaji.
20
Lakini mpatanishaji siye wa mmoja tu, lakini Mungu ni mmoja.
21
Tena je? Maonyo huvikataa viagio vya Mungu? La, sivyo! Kwani kama yangekuwako Maonyo yaliyotolewa kuwa yenye nguvu ya kuwapa watu uzima, wongofu ungepatikana kweli kwa kuyafanya maonyo.
22
Lakini Maandiko yamewafunga wote pamoja kuwa watumwa wa makosa kwamba: Wote watakaomtegemea wapewe kile kiagio kitokacho kwenye kumtegemea Yesu Kristo.
23
*Lakini tegemeo lilipokuwa halijatokea bado, tulilindwa, tuyatii Maonyo, tukawa tumefungwa pamoja, tungoje, tegemeo litakapofunuliwa.
24
Hivyo ndivyo, Maonyo yalivyotuongoza kama watoto, yakatupeleka kwake Kristo, tupate wongofu kwa kumtegemea.
25
Lakini tangu hapo, tegemeo lilipotokea, hatushikwi tena na mwongozi.
26
Kwani ninyi nyote m wana wa Mungu kwa kumtegemea mkiwa wake Kristo Yesu.
27
Maana ninyi nyote mliobatiziwa Kristo mmemvaa Kristo.
28
Kwake yeye hakuna tena Myuda na Mgriki, wala mtumwa na mwungwana, wala mume na mke, kwani ninyi nyote m mmoja kwa kuwa wake Kristo Yesu.
29
Nanyi mkiwa wake Kristo, basi, mmekuwa hata uzao wake Aburahamu, tena m warithi kwa kiagio, mlichowekewa.*
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6