bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Galatians 5
Galatians 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 6 →
1
*Kristo ametukomboa, tuwe waungwana. Kwa hiyo simameni, msijitie tena katika mafungo ya utumwa!
2
Tazameni, mimi Paulo nawaambiani: Kristo hatawafaa kitu, mkitahiriwa.
3
Tena namshuhudia kila mtu aliyetahiriwa, ya kuwa ni mdeni wa kuyafanya Maonyo yote.
4
Ninyi mtakao kupata wongofu kwa kuyafanya Maonyo mmetengwa na Kristo, mmeanguka na kuyaacha magawio.
5
Kwani sisi kwa nguvu ya Roho twakishika kingojeo cha kwamba: Tutapata wongofu kwa kumtegemea Mungu.
6
Maana tukiwa naye Kristo Yesu, kunakotupa nguvu siko kutahiriwa, wala kutotahiriwa, ila kumtegemea Mungu kutimilikako katika kupendana.
7
Mlianza kushika njia nzuri; yuko nani aliyewakwaza, msiyatii yaliyo ya kweli?
8
Kazi hii ya kuwavutavuta hivyo haikutoka kwake yeye aliyewaita.
9
Chachu kidogo hulichachusha donge lote.
10
Hivyo, mlivyo naye Bwana, mimi huwawazia kuwa welekevu kwamba: Hamtaigeuza mioyo. Lakini aliyewahangaisha hivyo ataiona hukumu yake, awaye yote.
11
Lakini mimi, ndugu, kama ningetangaza hata sasa, watu watahiriwe, ningekuwa mwenye kufukuzwa? Nayo makwazo ya msalaba yangekuwa yameondolewa.
12
Ingefaa, wale wenye kuwatukusa wakatwe na kutengwa.
13
Ndugu, ninyi mliitiwa kuwa waungwana. Lakini uungwana huo msiugeuze kuwa tokeo la tamaa za miili yenu, ila mtumikiane na kupendana!
14
Kwani Maonyo yote hutimilika katika neno moja, ndilo hili: Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe!
15
Lakini mkiumana, mkilana ninyi kwa ninyi, angalieni, msimezwe kabisa kwa kule kulana.*
16
*Lakini nasema, mwendelee Kiroho! Hivyo hamtaweza kuzitimiza tamaa za miili.
17
Kwani miili huyatamani yanayokataliwa na Roho, naye Roho huyatamani yanayokataliwa na miili; hawa wawili hupingana, msipate kuyafanya, myatakayo.
18
Lakini mkiongozwa na Roho ham tena watumwa wa Maonyo.
19
Nayo matendo ya miili yako waziwazi, ndiyo ugoni, uchafu, uasherati,
20
kutambikia vinyago, uchawi, uchukivu, ugomvi, wivu, mifundo ya mioyo, machokozi, matengano, vyama,
21
kijicho, ulevi, ulafi, nayo mambo mengine yaliyofanana nayo. Kama nilivyowaambia kale, vivyo hivyo nawaambia tena: Wafanyizao mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu.
22
Lakini mazao ya Roho ndiyo haya: upendano, furaha, utengemano, uvumilivu, utu, wema, welekevu,
23
utulivu, kuzishinda tamaa. Mambo kama hayo hayakataliwi na Maonyo.
24
Lakini wa Kristo Yesu huiua miili na kuiwamba msalabani pamoja na mawazo mabaya na tamaa.*
25
*Tukiwa wa Kiroho na tuendelee Kiroho!
26
Tusitafute utukufu ulio wa bure, tukichokozana, tena tukioneana kijicho!
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6