bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 11
Jeremiah 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 12 →
1
Hili ndilo neno lililomjia Yeremia likitoka kwake Bwana kwamba:
2
Yasikieni maneno ya agano hili, myaambie watu wa Yuda nao wakaao Yerusalemu!
3
Utawaambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Ameapizwa kila asiyeyasikia maneno ya agano hili,
4
niliyowaagiza baba zenu siku ile, nilipowatoa katika nchi ya Misri katika tanuru ya kuyeyushia vyuma kwamba: Isikilizeni sauti yangu, myafanyize yote, nitakayowaagiza! Ndivyo, mtakavyokuwa ukoo wangu, nami nitakuwa Mungu wenu,
5
kusudi nikitimilize kiapo, ambacho niliwaapia baba zenu cha kwamba: Nitawapa nchi ichuruzikayo maziwa na asali, kama ilivyo na siku hii ya leo. Ndipo, nilipojibu nikisema: Amin, Bwana.
6
Bwana akaniambia: Yatangaze maneno haya yote katika miji ya Yuda namo barabarani mwa Yerusalemu kwamba: Yasikilizeni maneno ya agano hili, myafanyize!
7
Kwani nimeyashuhudia baba zenu siku ile, nilipowatoa katika nchi ya Misri, mpaka siku hii ya leo sikuchoka kuwashuhudia na kuwahimiza kwamba: Isikieni sauti yangu!
8
Lakini hawakuisikia, wala hawakuyatega masikio yao, wakaendelea kila mmoja kwa ushupavu wa mioyo yao mibaya, kwa hiyo nikawatimizia maneno yote ya hilo agano, nililowaagiza, walifanye, lakini hawakulifanya.
9
Bwana akaniambia: Yameonekana mapatano mabaya ya watu wa Yuda nao wakaao Yerusalemu:
10
wameyarudia mabaya ya baba zao wa kale walikataa kuyasikiliza maneno yangu, wakafuata miungu mingine, waitumikie. Walio mlango wa Isiraeli nao walio mlango wa Yuda wamelivunja agano langu, nililolifanya na baba zao.
11
Kwa hiyo Bwana anasema hivi: Kweli wataniona, nikiwaletea mabaya, wasiyoweza kuyatoka. Ndipo, watakaponililia, lakini sitawasikia.
12
Kisha miji ya Yuda nao wakaao Yerusalemu watakwenda kuililia miungu, waliyoivukizia, lakini haitawaokoa siku za kupatwa na mabaya.
13
Kwani kama miji yako ilivyo mingi, ndivyo, miungu yako, Yuda, ilivyo mingi nayo. Tena kama barabara za Yerusalemu zilivyo nyingi, ndivyo, palivyo pengi napo, mlipopatengeneza pa kuitambikia iliyo yenye soni, ndipo pa kumvukizia Baali.
14
Wewe nawe usiwaombee wao wa ukoo huu! Wala usipaze sauti kunilalamikia kwa ajili yao! Kwani mimi sisikii, wanaponiita, kwa ajili ya ubaya wao.
15
Waliokuwa wapenzi wangu wanataka nini Nyumbani mwangu? Mkiyafanya mawazo yenu mabaya yaliyo mengi, nyama takatifu zitayaondoa, yawatoke ninyi? Nanyi mnapofanya mabaya, ndipo, mnapofurahi.
16
Bwana alikuita jina lako mchekele wenye majani mengi wa kupendeza macho kwa kuzaa vizuri, lakini sasa wengi wanaupigia makelele makubwa, maana ameuwashia moto wa kuuchoma, nayo matawi yake yamevunjika.
17
Kwani Bwana Mwenye vikosi aliyekupanda amesema mabaya yatakayokujia kwa ajili ya mabaya, wao wa mlango wa Isiraeli nao wa mlango wa Yuda waliyonifanyizia, wanikasirishe, wakimvukizia Baali.
18
Bwana akanijulisha, ndipo, nilipojua, kisha akanionyesha matendo yao.
19
Mimi nikawa kama mwana kondoo mwanana anayepelekwa kuchinjwa, sikujua, ya kama walikuwa wameniwazia mimi mawazo ya kwamba: Na tuuangamize mti na matunda yake! Na tuung'oe katika nchi yao walio hai, jina lake lisikumbukwe tena!
20
Lakini wewe Bwana Mwenye vikosi, unakata mashauri yaongokayo, unajaribu mafigo na mioyo; na nione, jinsi unavyowalipiza, kwani nimekusukumia wewe shauri langu.
21
Kwa hiyo Bwana anasema hivyo kwa ajili ya watu wa Anatoti walioitafuta roho yako wakisema: Usitufumbulie kwa Jina la Bwana, usiuawe na mikono yetu!
22
Kwa hiyo Bwana Mwenye vikosi anasema hivi: Utaniona, nikiwapatiliza: vijana wao watakufa kwa panga, nao watoto wao wa kiume na wa kike watakufa kwa njaa.
23
Lakini masao hayatakuwako, kwani watu wa Anatoti nitawaletea mabaya mwaka ule, watakapopatilizwa.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52