bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 13
Jeremiah 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 14 →
1
Hivi ndivyo, Bwana alivyoniambia: Nenda kujinunulia mshipi wa amerekani, ujifunge viunoni! Lakini usiutie majini!
2
Nikaununua mshipi, kama Bwana alivyoniagiza, nikajifunga viunoni.
3
Neno la Bwana likanijia mara ya pili kwamba:
4
Uchukue mshipi, ulioununua, ulio viunoni pako! Kisha inuka, uende kwenye Furati, uufiche kule katika ufa wa mwamba!
5
Nikaenda, nikauficha kule Furati, kama Bwana alivyoniagiza.
6
Ikawa, siku nyingi zilipopita, ndipo, Bwana aliponiambia: Inuka, uende Furati, uuchukue kule mshipi, niliokuagiza kuuficha huko.
7
Nikaenda Furati, nikauchimbua, nikauchukua ule mshipi mahali hapo, nilipouficha; lakini nilipoutazama ule mshipi, ulikuwa umeharibika, haukufaa kitu cho chote.
8
Ndipo, neno la Bwana liliponijia kwamba:
9
Bwana anasema hivi: Hivi ndivyo, nitakavyoyaharibu majivuno ya Yuda nayo majivuno ya Yerusalemu yaliyo mengi.
10
Watu wa ukoo huu mbaya wamekataa kuyasikia maneno yangu, wakajiendea kwa ushupavu wa mioyo yao, wakafuata miungu mingine wakiitambikia na kuiangukia; basi, watakuwa kama mshipi huu usiofaa kitu cho chote.
11
Kwani kama mshipi unavyoambatana na viuno vya mtu, ndivyo, nilivyowaambatanisha na mimi wote walio wa mlango wa Isiraeli nao wote walio wa mlango wa Yuda, wawe ukoo wangu wa kulikuza Jina langu, wakilishangilia na kulitukuza, lakini hawakusikia; ndivyo, asemavyo Bwana.
12
Basi, utawaambia neno hili: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Viriba vyote na vijazwe mvinyo! Wakikuuliza: Hatujui, ya kuwa viriba vyote hujazwa mvinyo?
13
ndipo, utakapowaambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mtaniona, nikiwajaza ulevi wote wakaao katika nchi hii, wafalme wanaokikalia kiti cha kifalme cha Dawidi na watambikaji na wafumbuaji nao wote wakaao Yerusalemu.
14
Kisha nitawaponda kila mtu kwa ndugu yake, hata wababa na wana pamoja, sitawaonea uchungu, wala sitawachagulia, wala sitawahurumia, nisiwaangamize; ndivyo, asemavyo Bwana.
15
Sikieni na kusikiliza vema! Msijikweze! Kwani Bwana anasema:
16
Mtukuzeni Bwana Mungu wenu, akingali hajaleta giza bado, mkingali hamjajikwaa miguu yenu milimani penye giza! Maana mtangoja, pawe mwanga, naye ataugeuza kuwa kivuli kiuacho akiufunikiza mawingu meusi.
17
Lakini msiposikia, roho yangu itayalilia majivuno yenu mafichoni, nayo macho yangu yatachuruzika machozi pasipo kukoma, kwa kuwa kundi la Bwana limetekwa.
18
Mwambie mfalme na mama yake: Jinyenyekezeni, mkae chini! Kwani vichwani penu vilemba vya urembo vimeanguka chini!
19
Miji ya upande wa kusini imefungwa, tena hakuna anayeifungua, Wayuda wote wametekwa, kweli wote pia wametekwa.
20
Yainueni macho yenu, mwaone wanaokuja toka kaskazini! Kundi ulilopewa liko wapi, wale kondoo wako wenye utukufu?
21
Utasemaje, akikuwekea wale kuwa wakuu wako, uliowazoeza kuwa rafiki zako wapendwa? Wao watakapokuwa wakuu, hautakushika uchungu kama wa mwanamke anayetaka kuzaa?
22
Kama unauliza moyoni mwako: Mbona haya yamenitukia? ujue: Kwa mabaya yako mengi, uliyoyafanya, nguo zako zenye mapindo marefu zimefunuliwa, hata miguu yako ikatokezwa nje kwa kukorofishwa hivyo.
23
Je? Mtu mweusi anaweza kuigeuza ngozi yake? Au chui anaweza kuyaondoa madoadoa yake? Kama ndivyo, mngeweza kufanya mema nanyi mliofundishwa kufanya mabaya.
24
Kwa hiyo nitawatawanya kama makapi yapeperushwayo na upepo wa nyikani.
25
Haya ndiyo, uliyopatiwa na kura, ni fungu lako, ulilopimiwa na mimi, kwa kuwa umenisahau, ukaegemea mambo ya uwongo; ndivyo, asemavyo Bwana.
26
Kwa hiyo mimi nami nitazipandisha nguo zako zenye mapindo marefu na kuziweka usoni pako, yako yenye soni yaoneke.
27
Uzinzi wako na vilio vyako vya utongozi na uovu wako wa kuziwaza njia za ugoni za kwenda vilimani au mashambani, nimeyaona hayo matapisho yako. Yatakupata, wewe Yerusalemu, usieuliwe! Yatakuwa hivyo mpaka lini?
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52