bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 14
Jeremiah 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 15 →
1
Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Yeremia kwa ajili ya kupotea kwa mvua:
2
Yuda huomboleza, nao waliomo malangoni mwake wamefifia kwa kukaa mchangani na kuvaa nguo nyeusi, navyo vilio vya Yerusalemu hupanda juu.
3
Wakuu wao huwatuma walio wadogo kwao kwenda majini; lakini wakifika visimani hawaoni maji, hurudi wenye mitungi mitupu, huona soni na masikitiko, hufunika vichwa vyao,
4
kwani nchi imeatukaatuka; kwa kuwa haikuwako mvua katika nchi, wakulima huona soni, huvifunika vichwa vyao.
5
Kwani kulungu nao wakizaa porini huwaacha watoto, kwa kuwa hakuna majani.
6
Navyo vihongwe husimama vilimani juu, hutwetea upepo kama mbwa wa mwitu, macho yao huzimia kwa kuwa hakuna majani.
7
Kweli manza, tulizozikora, zimetusuta; lakini, Bwana, yafanye yalipasayo Jina lako! Kwani tumekuacha mara nyingi, tukarudi nyuma, tumekukosea kweli.
8
Wewe ndiwe, Waisiraeli wamngojeaye, ndiwe mwokozi wao, siku zinapokuwa mbaya. Mbona unataka kuwa kama mgeni katika nchi hii au kama mpitaji apigaye kambi tu kulala usiku?
9
Mbona unataka kuwa kama mtu aliyeshindwa au kama fundi wa vita asiyeweza kuokoa? Wewe, Bwana, uko kwetu katikati, nasi huitwa kwa Jina lako, usituache!
10
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya watu wa ukoo huu: Hupenda kwenda huko na huko, hawaizuii miguu yao; kwa hiyo Bwana hapendezwi nao, sasa anayakumbuka mabaya yao, waliyoyafanya, ayapatilize makosa yao.
11
Naye Bwana akaniambia: Usiwaombee wao wa ukoo huu, niwafanyizie mema!
12
Wakifunga mfungo, siwasikii malalamiko yao; hata wakitoa ng'ombe au vipaji vingine vya tambiko, sipendezwi nao. Kwani mimi nitawamaliza kwa panga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya.
13
Nikasema: E Bwana Mungu, tazama! Wako wafumbuaji wanaowaambia: Hamtaona upanga, wala njaa haitakuwa kwenu, kwani nitawapa kutengemana kweli mahali hapa!
14
Bwana akanijibu: Ni uwongo tu, hao wafumbuaji wanaofumbua katika Jina langu sikuwatuma, wala sikuwaagiza neno, wala sikusema nao. Wanayoyafumbua ni ndoto za uwongo na maaguaji ya bure na madanganyifu ya mioyo yao.
15
Kweli hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Wafumbuaji hao wanaofumbua katika Jina langu mimi sikuwatuma, wao wanaosema: Hakuna upanga wala njaa itakayokuwa katika nchi hii, basi, wafumbuaji hao watamalizwa kwa panga na kwa njaa!
16
Hata watu waliofumbuliwa nao watakuwa wametupwa barabarani mwa Yerusalemu wakiuawa kwa njaa na kwa panga, hatakuwako atakayewazika wao na wake zao na wana wao wa kiume na wa kike; ndivyo, atakavyowamwagia mabaya yao.
17
Nawe na uwaambie neno hili: Macho yangu yanachuruzika machozi usiku na mchana, hayakomi, kwani wanawali walio wazaliwa wa ukoo wangu wamevunjika mavunjiko makuu, ni pigo lisilopona kabisa.
18
Nikitoka kwenda shambani ninaona waliouawa na panga; nikiingia mjini ninaona waliozimia kwa njaa. Kwani nao wafumbuaji pamoja na watambikaji wanahamia nchi, wasiyoijua.
19
Umemtupa Yuda kabisa? Roho yako imetapishwa na Sioni? Mbona umetupiga? Lakini hakuna atakayetuponya. Tunangojea utengemano, lakini hakuna chema; tunangojea siku za kupona, lakini tunayoyaona ni mastuko.
20
Tunajua, Bwana, ya kuwa hatukukucha, tukakora manza, baba zetu walizozikora; kweli tumekukosea wewe.
21
Lakini kwa ajili ya Jina lako usitukatae na kututweza! Usiache, kiti cha utukufu wako kibezwe! Likumbuke Agano lako, ulilolifanya na sisi, usilivunje!
22
Je? Katika miungu ya wamizimu isiyo kitu imo iwezayo kunyesha mvua? Au ni mbingu zitoazo zenyewe manyunyu tu? Si wewe, Bwana Mungu wetu? Kwa hiyo tunakungojea, kwani wewe ndiwe ayafanyaye haya yote.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52