bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 16
Jeremiah 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 17 →
1
Neno la Bwana likanijia kwamba:
2
Usijichukulie mke, usizae wana wa kiume wala wa kike mahali hapa!
3
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya wana wa kiume na wa kike wanaozaliwa mahali hapa na kwa ajili ya mama zao waliowazaa na kwa ajili ya baba zao waliowazaa katika nchi hii:
4
Watakufa kwa magonjwa mabaya, hawataombolezewa, wala hawatazikwa, ila watakuwa tu kama kinyesi juu ya nchi; wengine watauawa kwa panga na kwa njaa, nayo mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na cha nyama wa porini.
5
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Usiingie nyumbani mwenye maombolezo, wala usiende kuwalilia, wala usiwakalie matanga! Kwani nimeuondoa utengemano wangu kwao walio ukoo huu, nisiwagawie chema, wala nisiwahurumie; ndivyo, asemavyo Bwana.
6
Watakufa wakubwa na wadogo katika nchi hii pasipo kuzikwa, tena hakuna watakaowalilia wala watakaojikata chale wala watakaonyoa vichwa.
7
Wala hakuna watakaowagawia vyakula, wakikaa matanga, wala watakaowatuliza mioyo kwa ajili ya mfu, wala hakuna watakaowanywesha vikombe vya kuwatuliza mioyo wakifiwa na baba au mama.
8
Namo nyumbani mwenye karamu usimwingie kukaa nao, mkila, mkinywa!
9
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Mtaniona na macho yenu siku hizi zenu, nikikomesha mahali hapa sauti za vicheko na sauti za furaha, hata sauti za wachumba wa kiume na wa kike.
10
Itakuwa, utakapowapasha wao wa ukoo huu habari hizi zote, watakuuliza: Kwa sababu gani Bwana anatutakia haya mabaya yote yaliyo makuu? Tumekora manza gani? Bwana Mungu wetu, tumekosa makosa gani?
11
Ndipo, utakapowaambia: Ndivyo, asemavyo Bwana: Kwa kuwa baba zenu waliniacha, wakafuata miungu mingine, wakaitumikia na kuiangukia, lakini mimi waliniacha, hawakuyashika Maonyo yangu.
12
Nanyi hamkufanya mabaya kuliko baba zenu? Ninawaona, mkiufuata kila mtu ushupavu wa moyo wake mbaya pasipo kunisikia mimi.
13
Kwa hiyo nitawaondoa katika nchi hii na kuwabwaga katika nchi, msiyoijua ninyi wala baba zenu! Ndiko, mtakakoweza kuitumikia miungu mingine mchana na usiku, kwa kuwa sitaki kuwahurumia tena.
14
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaona kweli, siku zikija, watu watakapoacha kuapa wakisema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima aliyewatoa wana wa Isiraeli katika nchi ya Misri!
15
Ila wataapa wakisema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima aliyewatoa wana wa Isiraeli katika nchi ya upande wa kaskazini na katika nchi zote, alikowatupia! Maana nitawarudisha katika nchi yao, niliyowapa baba zao.
16
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaniona, nikituma wavuvi wengi, wawavue! Kisha nitatuma wawinda wengi, wawawinde katika milima yote na katika vilima vyote na katika nyufa zota za miamba.
17
Kwani macho yangu huziona njia zenu zote, hazifichiki usoni pangu, wala manza zao, walizozikora, hazifunikiki machoni pangu.
18
Lakini kwanza nitawalipisha mara mbili manza zao na makosa yao, kwa kuwa wameichafua nchi yangu kwa mizoga ya matapisho yao, fungu langu wakalijaza machukizo yao.
19
Bwana ndiwe nguvu yangu na ngome yangu na kimbilio langu siku ya masongano; wewe watakujia wamizimu wakitoka mapeoni kwa nchi, watakuambia: Baba zetu waliyokuwa nayo, ni mambo ya uwongo tu yasiyo maana, yasiyowafalia kitu.
20
Je? Mtu atawezaje kujitengenezea miungu? Kweli siyo miungu!
21
Mtaona kweli, nikiwajulisha mara hii, nikiwapa kuujua mkono wangu na uwezo wangu; ndipo, watakapojua, ya kuwa Jina langu ni Bwana.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52