bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 17
Jeremiah 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 18 →
1
Ukosaji wa Yuda umeandikwa kwa kalamu ya chuma yenye ncha kali kama ya jiwe la almasi; mbao ulimochorwa ni mioyo yao na pembe za meza za kutambikia.
2
Kwa hiyo wana wao huzikumbuka meza zao za kutambikia na vinyago vyao vya Ashera, wanapoona mti wenye majani mengi au wanapofika vilimani juu.
3
Mlima wangu ulioko shambani na mali zako na vilimbiko vyako vyote vilivyoko vilimani nitavitoa, vipokonywe, kwa ajili ya makosa yako, uliyoyakosa katika mipaka yako yote.
4
Nawe kwa ajili yako mwenyewe huna budi kulihama fungu lako, nililokupa, nami nitakutumikisha, uwatumikie adui zako katika nchi, usiyoijua, kwani makali yangu nimeyawakisha moto, usizimike kale na kale.
5
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Ameapizwa kila mtu amwegemeaye mtu mwenziwe akimtumia mwenye mwili kuwa mkono wake na kumwondoa Bwana moyoni mwake!
6
Atakuwa kama mti wa jangwani usio na majani, hataona jema lo lote, likimjia; atakaa nyikani pakavu penyewe penye chumvi, pasipokaa mtu.
7
Amebarikiwa kila mtu amwegemeaye Bwana, Bwana akiwa egemeo lake!
8
Atakuwa kama mti uliopandwa penye maji upelekao mizizi yake mpaka mtoni; hauogopi, ijapo jua kali liufikie; majani yake hustawi vivyo hivyo; ijapo mwaka ukose mvua, hausumbuki, wala haukomi kuzaa matunda.
9
Moyo wa mtu hudanganya kuliko mengine yote, tena huponza; yuko nani aujuaye?
10
Mimi Bwana ninauumbua moyo nikiyajaribu mafigo, nimpe kila mtu yazipasayo njia zake na mapato ya matendo yake.
11
Kama kwale anayelalia mayai, asiyoyataga, ndivyo, alivyo apataye mali kwa kupotoa watu; siku zake zitakapofika kati, zitampotelea, naye mwisho atapumbaa tu.
12
Wewe kiti chenye utukufu umetukuka tangu mwanzo, ndipo mahali petu patakatifu,
13
wewe Bwana u kingojeo cha Waisiraeli; wote wakuachao hupatwa na soni, waondokao kwako huandikwa wakingaliko nchini, ya kuwa wamemwacha Bwana aliye kisima chenye maji ya uzima.
14
Niponye, Bwana! Ndivyo, nitakavyopona. Niokoe! Ndivyo, nitakavyookoka; kwani wewe ndiwe shangilio langu.
15
Watazame wanaoniambia: Neno lake Bwana liko wapi? Na lije!
16
Mimi sikujitoa katika uchungaji, nisikufuate, wala sikutaka, siku yenye uchungu iwajie, kama wewe unavyojua; yaliyotoka midomoni mwangu yako wazi usoni pako.
17
Usiniangamize, wewe uliye kimbilio langu, siku ikiwa mbaya!
18
Na wapatwe na soni wanikimbizao, nisipatwe na soni mimi! Na waangamie wao, nisiangamie mimi! Uwaletee wao siku mbaya! Mara mbili uwavunje, wavunjike kweli!
19
Hivi ndivyo, Bwana alivyoniambia: Nenda kusimama langoni mwao walio wazaliwa wa ukoo huu, wafalme wa Yuda walimopitia wakiingia au wakitoka, hata malangoni mote mwa Yerusalemu,
20
kawaambie: Lisikieni neno la Bwana, ninyi wafalme wa Yuda nanyi Wayuda nyote nanyi nyote mkaao Yerusalemu mnaopitia humu malangoni!
21
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Ziangalieni roho zenu, msichukue mzigo siku ya mapumziko mkiuingiza humu malangoni mwa Yerusalemu!
22
Wala msitoe mzigo nyumbani mwenu siku ya mapumziko! Wala msifanye kazi yo yote! Ila itakaseni siku ya mapumziko, kama nilivyowaagiza baba zenu!
23
Lakini hawakusikia, wala hawakuyatega masikio yao, wakazishupaza kosi zao, wasisikie, wasionyeke.
24
Ndivyo, asemavyo Bwana: Sasa ninyi nisikieni, msiingize mzigo malangoni mwa mji huu siku ya mapumziko! Ila itakaseni siku ya mapumziko, msipoifanyizia kazi yo yote!
25
Ndipo, watakapoingia humu malangoni mwa mji huu wafalme wanaokikalia kiti cha kifalme cha Dawidi na wakuu wanaopanda magari na farasi, wao wenyewe na wakuu wao, Wayuda nao wakaao Yerusalemu, nao mji huu utakaa kale na kale.
26
Tena watakuja wakitoka katika miji ya Yuda na katika nchi zizungukazo Yerusalemu na katika nchi ya Benyamini, kwenye mbuga na kwenye milima, hata upande wa kusini, wataleta ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za kuchinjwa na vipaji vingine vya tambiko na uvumba, wataviingiza Nyumbani mwa Bwana, wamshukuru.
27
Lakini msiponisikia mkiacha kuitakasa siku ya mapumziko, mkaingia malangoni mwa Yerusalemu na kuchukua mizigo siku ya mapumziko, basi, nitawasha moto malangoni mwake, nao utayala majumba ya Yerusalemu pasipo kuzimika.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52