bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jeremiah 18
Jeremiah 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 19 →
1
Hili ndilo neno lililomjia Yeremia likitoka kwake Bwana kwamba:
2
Inuka, ushuke kwenda nyumbani mwa mfinyanzi. Ndimo, nitakamokuambia maneno yangu.
3
Nikashuka kwenda nyumbani mwa mfinyanzi, nikamkuta, akifanya kazi kwenye kibao chake.
4
Chombo, mfinyanzi alichokifanya na mkono wake, kisipokuwa chema, basi, akakitengeneza kuwa chombo kingine, kama ilivyofaa machoni pake mfinyanzi kukifanya.
5
Neno lake Bwana likanijia kwamba:
6
Kama huyu mfinyanzi nami siwezi kuwafanyizia ninyi mlio mlango wa Isiraeli? ndivyo, asemavyo Bwana. Tazameni: kama udongo ulivyo mkononi mwa mfinyanzi. ndivyo, ninyi mlio mlango wa Isiraeli mlivyo mkononi mwangu.
7
Mara ninatisha taifa au ufalme kwamba: Nitawang'oa na kuwavunja na kuwaangamiza.
8
Lakini taifa hilo, nililolitisha, likigeuka na kuuacha ubaya wake, nami nitageuza moyo, nisiwafanyizie hayo mabaya, niliyoyawaza kuwafanyizia.
9
Mara ninaagiza taifa au ufalme kuwajenga na kuwapanda
10
Lakini wakifanya yaliyo mabaya machoni pangu, wasiisikie sauti yangu, basi, nitageuza moyo, nisiwafanyizie hayo mema, niliyoyasema, niwafanyizie.
11
Sasa uwaambie walio Wayuda nao wakaao Yerusalemu kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Tazameni, mimi ninawatengenezea mabaya kwa kuwawazia mawazo! Kwa hiyo rudini kila mtu katika njia yake mbaya, mshike njia zitakazowafaa, mfanye matendo mema!
12
Lakini hujibu: Ni kazi bure! Kwani tutaendelea kuyafuata mawazo yetu, tufanye kila mtu yaupasayo ushupavu wa moyo wake mbaya!
13
Kwa hiyo Bwana anasema hivyo: Ulizeni kwa wamizimu, kama yuko aliyesikia mambo kama hayo! Wanawali wa Isiraeli wamefanya mambo yazizimuayo kabisa.
14
Je? Theluji ya Libanoni inaondoka katika ile miamba iliyoko kileleni juu ya kondeni? Je? Yanakauka maji yenye baridi ya vijito vitokavyo mbali?
15
Lakini walio ukoo wangu wamenisahau, huvukizia miungu isiyo kitu, nayo ikawaangusha katika njia zao, walizozishika tangu kale, wakafuata mikondo isiyotengenezwa kuwa njia.
16
Wakaigeuza nchi yao kuwa mapori tu, izomelewe kale na kale; kila atakayeipita ataistukia, wataitingishia vichwa vyao.
17
Kama upepo utokao maawioni kwa jua unavyofanya, nitawatawanya machoni pa adui; ndio mgongo, sio uso, nitakaowaonyesha siku ya kuangamia kwao.
18
Wakasema: Njoni, tumlie Yeremia njama ya kumwazia mawazo! Kwani maonyo hayampotelei mtambikaji, wala mizungu haimpotelei mjanja, wala maneno hayampotelei mfumbuaji. Haya! Tumpige tukiyatumia, ulimi wake uliyoyasema! Tusiyasikilize maneno yake yote!
19
Bwana, nisikilize! Isikie sauti ya wapingani wangu!
20
Je? Mema yanalipwa na kufanyiziwa mabaya? Wamenichimbia mwina; kumbuka, jinsi nilivyosimama mbele yako na kuwasemea mema, niyatulize makali yako yenye moto, yasiwatokee!
21
Kwa hiyo watoe wana wao, wauawe na njaa, kawabwage kwenye panga, wanawake wao wawe pasipo watoto na pasipo waume! Waume wao na wauawe na kifo, vijana wao na wapigwe na panga za vitani!
22
Nyumbani na msikilike vilio, ukiwastusha kwa kuwaletea vikosi vya wapiga vita! Kwani wamenichimbia mwina, wanikamate, miguu yangu wakaitegea matanzi.
23
Wewe Bwana, unaijua njama yao yote ya kuniua; usizifunike manza zao, wala usiyafute makosa yao usoni pako, wawe wameangushwa usoni pako! Siku, makali yako yatakapowakia, wapigie shauri!
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52